Telewolth bin champion
JF-Expert Member
- Dec 11, 2018
- 2,386
- 6,473
Ndio hivyo inabidi waTanzania waelewe ukweli[emoji23]Mwingine anapita tu[emoji1787][emoji1787],hata interview hafanyi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio hivyo inabidi waTanzania waelewe ukweli[emoji23]Mwingine anapita tu[emoji1787][emoji1787],hata interview hafanyi.
Unajikuta kutafuta kazi kunageuka ndio kazi🤣🤣🤣Ndio hivyo inabidi waTanzania waelewe ukweli[emoji23]
Inasikitisha sana asee..interview yangu ya kwanza ilikua kwenye NGO , tulikua watu watano na walitaka watu watatu, nilikua najuana na watu watatu kati ya hao tano, na ndo tuliopita after 3 days tukapewa hadi job offer letters, wakasema watatuambia lini tukareport kazini, tulikaa miezi na miezi tukajasikia tu mbona watu washaanza kazi kitambo na hawakuepo hata kwenye interview , kazi tulioifanyia sisi interview ikaishiwa kufanywa na watu ambao hawakuepo kabisa. [emoji706][emoji706]
Sent from my SM-G9550 using JamiiForums mobile app
Halafu kuna pimbi anakwambia vijana wasiona ajira wazembeAcha kabisa mkuu, nafasi zinatangazwa zimeshajaa.
Hizo fani za uhandisi zina tatizo gani boss?Pilot
Aircraft engineer
Marine and nautical engineer
Drilling Engineer
Well completion engineer
Fishing engineer
Mining Engineer
Robotic and Automation engineer.
Cyber security expert.
Software developer.
Artificial Intelligence expert.
Reliability and Mechanical Engineer.
ROV operator.
Automation engineer.
Instrumentatio engineer
Electric Engineer.
Mechanical Engineer.
Civil Engineer
nk, nk, nk.
Taifa halitoi direction kwa vijana wasome nini, matokeo yake vijana huishia kutia huruma na kunyenyekea wapumbavu.
Hizo fani za uhandisi zina tatizo gani boss?
Mambo ya Usahili yanatishaNawasalimu wote kwa jina la Jamhuri ya Muungano.
Vijana tunapitia mengi ya kukatisha tamaa, lakini leo niwape machache ya vituko vya sahili nilivyowahi kuviona kwa macho yangu.
1. Tuliitwa kwenye usahili mikoa ya nyanda za juu kusini, basi kwa furaha na kujiamini nikapaki vitu huyooo nikafika siku moja kabla nikaripoti na nikakuta watu wengine, siku ya pili yake tukawahi sana tu,basi wakati tunaendelea kusubili wasahili wakafika na gari aina ya cruiser wakashuka kama saba hivi, sisi tukajua wote ni wasahili, lahaula kumbe wengine ni wasahiliwa kama sisi na tuligundua baada ya kuona wanakuja kukaa kwa wasahiliwa. Baada ya usahili matokeo nakuachia utabiri mwenyewe.
2. Tuliitwa kwenye usahili wa serikali basi wakati tunaendelea kusahiliwa basi kuna kijana sijui wa mkubwa gani akawa ameondoka eneo lile, basi unaambiwa alitafutwa balaa na mwisho wa siku matokeo yumo.
3. Kuna siku tunasubiri usahili,kuna vijana wakawa wanasema wameagizwa kuja hapo kama utani vile,aisee haikuwa utani matokeo yalitujulisha.
4. Tumefanya usahili,matokeo watu ambao hawakuwepo kwenye usahili ndio waajiliwa.
Dah mambo ni mengi sana,ushauri wangu vijana msio na connection mkaze sana na kumuomba Mungu,lakini naamini kila kitu kinawezekana.
Kama una kisa ni ruhusa kuweka.
Sipati picha ulivyo vunjika moyo.Miaka 10 iliyopita nilifanya interview TANROAD Kili, baada ya interview one of the panelist alinijulisha kwa simu kuwa nimepita lakini ningepigiwa simu na wahusika ili uje uanze kazi.
Nilivyokuja kufuatilia nikaambiwa kuna vidada vilikuwa field 3 yrs pale ndio wamechukuliwa na infact tulikuwa nao siku ya interview.
Wanataka jamii ione wanatangaza nafasi za kazi kumbe kazi zenyewe zimejaa.Aisee inahuzunisha kusumbuana hata mahali pa interviews huku wengine wakitoka mbali safari ndefu+fares, huku ukijua kabisa una watu wako(interviewers) wana dhambi sana.
Sana tu.Inasikitisha sana asee..
#MaendeleoHayanaChama
We acha tu,ashibaye hamjui mwenye njaa.Halafu kuna pimbi anakwambia vijana wasiona ajira wazembe
Vijana wasikate tamaa.sa itakuaje
Heri wewe kama unatenda haki,ubarikiwe na kizazi chako,ila huku nje ni moto.Kwa uzoefu wangu katika saili nyingi ambazo nimesaili vijana, Taifa hili tuna changamoto kubwa sana ya uelewa wa mambo unakuta mtu kasoma special school na ana Bachelor ya Computer Engineering unamuuliza swali what is Operating System anabaki anashangaa akitoka njee anasema wana watu wao, Binafsi nimeapa nilipata kazi kwa haki na nitatenda haki siku zote japo majaribu ni Mengi na Mikuki ni Mingi, ila kuna vijana wana ufaulu mzuri ila interview wanachemka sana, sikatai uwepo wa upendeleo katika baadhi ya taasisi mbalimbali lakini rai yangu kwa vijana fanya maandalizi vizuri kafanye usaili notion za kusingizia watu wamepangwa achana nazo.
Sent from my SM-N950N using JamiiForums mobile app
Huko nadhani sio sana,lakini mambo haya yapo kila mahali kwa sasa,japo ukubwa unatofautiana.Ina maana hata hizo za sekretarieti ndio zilivyo au??