Vituko nilivyowahi kuviona kwenye sahili (interviews) vya kukatisha tamaa

Vituko nilivyowahi kuviona kwenye sahili (interviews) vya kukatisha tamaa

Nawasalimu wote kwa jina la Jamhuri ya Muungano.

Vijana tunapitia mengi ya kukatisha tamaa, lakini leo niwape machache ya vituko vya sahili nilivyowahi kuviona kwa macho yangu.

1.
Tuliitwa kwenye usahili mikoa ya nyanda za juu kusini, basi kwa furaha na kujiamini nikapaki vitu huyooo nikafika siku moja kabla nikaripoti na nikakuta watu wengine, siku ya pili yake tukawahi sana tu,basi wakati tunaendelea kusubili wasahili wakafika na gari aina ya cruiser wakashuka kama saba hivi, sisi tukajua wote ni wasahili, lahaula kumbe wengine ni wasahiliwa kama sisi na tuligundua baada ya kuona wanakuja kukaa kwa wasahiliwa. Baada ya usahili matokeo nakuachia utabiri mwenyewe.

2. Tuliitwa kwenye usahili wa serikali basi wakati tunaendelea kusahiliwa basi kuna kijana sijui wa mkubwa gani akawa ameondoka eneo lile, basi unaambiwa alitafutwa balaa na mwisho wa siku matokeo yumo.

3. Kuna siku tunasubiri usahili,kuna vijana wakawa wanasema wameagizwa kuja hapo kama utani vile,aisee haikuwa utani matokeo yalitujulisha.

4. Tumefanya usahili,matokeo watu ambao hawakuwepo kwenye usahili ndio waajiliwa.

Dah mambo ni mengi sana,ushauri wangu vijana msio na connection mkaze sana na kumuomba Mungu,lakini naamini kila kitu kinawezekana.

Kama una kisa ni ruhusa kuweka.
2008 kuna jamaa tulikutana kwenye usaili wa JKT . Dogo kwa muonekano alitokea familia flani ivi duni afu za kidini sana mana alikuwa mnyenyekevu mpaka anaboa . Mimi tayari uhakika wa kupita ulikuwepo japo sikupenda kuwa mjeshi hivyo nilifata maelekezo tu.

Basi dogo umefika muda wakuhojiwa akatumwa sigara ile anarudi anaambiwa kachelewa dogo alilia mpaka makamasi kumbe ashaliwa pesa kibao toka wilayani then mkoani anakaziwa kijinga afu bosi mmoja akamwambia amepunguwa urefu fut3 wakati toka mwanzo ashapimwa na akapita. Dah! Ile hali ilinigusa sana nikajaribu kumshauri na kumpa moyo ndo akanambia kuwa mama yake kawekeza Sana ili ye aende jeshi mpaka kauza baadhi ya vitu vyake kuweka mazingira sawa. Basi nilichokifanya nikaongea na wakubwa walotamani niende jeshi kuwa me sivutiwi kwenda jeshi ila nafasi yangu kuna mtoto wamsaidie, basi wakanielewa wakampitisha ,aisee dogo hajaniangusha kapambana mpaka akapata nafasi na leo ni miongoni mwa connection zangu zinazonifanya nivimbe mjini apa.

My point : kama ipo ipo tu msikate tamaa ukiona umekosa ujue sio liziki yako ila kama ni liziki yako itakuja kwa njia yyt ile
 
Aisee hongera sana kwa kumhurumia,wenye mioyo hiyo ni wachache.
 
🤣🤣🤣🙏🙏 hadi usangoma ni connection muulize Mshana Jr

Anyways kuna interview jamaa walienda mkoani basi kabla ya chochote wakaambiwa wapashe misuli moto kidogo wakimbie kama umbali wa kama viwanja viwili vya mpira na kurudi. Basi unaambiwa wakati wa kurudi wakakuta wale wasaili wameweka kamba mithili ya watu wa riadha so wasailiwa walio wahi kuingia kwenye kamba ndio wakawa wameshinda usaili hivyo
 
Kwel chief.
Kwakifupi mimi hakuna Interview ambayo nimeshawah kuitwa second round.

Huwa naishia kwanye ile ya woteee ile ya kupiga paper [emoji23][emoji23][emoji23]

Nimehangaika sana kwenye hili nikajikubali kwamba AM NOT SPECIAL FOR INTERVIEWS[emoji16]
Nishaombaga sana kazi za u developer na u system admin mpaka nikachoka then i decided to create that job for myself..

Hahaha, mkuu japo sio mazuri, ila komenti yako imenichekesha sana.
 
ile tumemaliza chuo tu mimi na mwanangu milandu tukapewa mchongo na sista..sista yeye kasoma masomo ya ras simba tu mixer na vyuo vya mtaani..sisi tuna gamba, NGO ipo mikocheni ..kuna engineer pale ndo kampa mchongo..sista hakua hata na cv tukasema tumchoree cv fastaa asbuhi ya kuzugia,maana sisi zetu zipo zimeshiba.. tumeingia tumepiga sana yai baba..hahaha jioni me na mwanangu tumekalia kuti kavu sista huyo kapita kisa engineer ambaye pia panelist anamuelewa sista
 
Anyways kuna interview jamaa walienda mkoani basi kabla ya chochote wakaambiwa wapashe misuli moto kidogo wakimbie kama umbali wa kama viwanja viwili vya mpira na kurudi. Basi unaambiwa wakati wa kurudi wakakuta wale wasaili wameweka kamba mithili ya watu wa riadha so wasailiwa walio wahi kuingia kwenye kamba ndio wakawa wameshinda usaili hivyo
Angalau hao walikua fair.
 
ile tumemaliza chuo tu mimi na mwanangu milandu tukapewa mchongo na sista..sista yeye kasoma masomo ya ras simba tu mixer na vyuo vya mtaani..sisi tuna gamba, NGO ipo mikocheni ..kuna engineer pale ndo kampa mchongo..sista hakua hata na cv tukasema tumchoree cv fastaa asbuhi ya kuzugia,maana sisi zetu zipo zimeshiba.. tumeingia tumepiga sana yai baba..hahaha jioni me na mwanangu tumekalia kuti kavu sista huyo kapita kisa kuna engineer panelist kamuelewa.
🤣🤣Mkafa na cv zenu,mambo haya yanachekesha na kuhudhunisha kwa pamoja.
 
Kaka yani umeenda kufanya interview ya public relations halafu kabla huja ingia kwenye oral uambiwe pasheni misuli kidogo kisha mrudi halafu wakati wakurudi ghafla wasaili wanasema walio rudi KWANZA ndio wameshinda usaili hiyo unaita fair?
Unaweza ishiwa nguvu,daa!.
 
Ni wiki Tatu zilizopita niliitwa kwenye Interview KCB BANK MAKAO MAKUU DAR nafasi ya CORPORATE AFFAIRS MANAGER,kufika pale tupo Wasailiwa 12 na mmoja yeye anafanyia Usaili akiwa Mwanza(huyu ni staff wa KCB BANK MWANZA)!!![emoji1787]na katika 11 tulio Dar Wasailiwa wawili nao wadada ni wa palepale ndani KCB BANK Maka Makuu[emoji1787]Usaili tuliambiwa saa 8 mchana lakini ukaanza saa 10 jioni(ilikuwa ni Written Interview).Yaani tangu tumefika pale wale wadada(wa HR na Head wa Communications)wakawa wanajizungushazungusha weeee nikajua tu hapa USANII unachezwa!!!kuja kuleta hiko ki-swali Chao chenyewe eti (I)WHAT IS EVENT PLANNING??(II)PROCEDURES ZA EVENT PLANNING(III) EXPLAIN SHORTY ON THOSE PROCEDUCES OF EVENT PLANNING??
yaani ni ki-swali ambacho nilikijibu ndani ya dakika 10 japo wao walisema dakika 30!!!juzi napokea Email kutoka kwa huyo Dada HR anaitwa MONDE LUSHAKO eti nilipata below PASS MARK hivyo sijachaguliwa kwa Oral nilicheka mpaka nikapaliwa na Wine yangu!! [emoji1787][emoji1787] yaani ni wasanii walikuwa na mtu wao wahuni wale[emoji1787][emoji1787]na mimi nina uhakika kile ki-swali chao nilikipata chote 100 kwa 100!!nilimjibu kwenye Email yake kwamba WAMUOGOPE MUNGU na waache tabia ya kusumbua watu waje kwenye Interview wakati nafasi tayari wana mtu wao!!!hebu imagine wengine mpo Dar mnafanya Interview na mwingine(staff wa ndani KCB Bank humohumo) anafanyia Usaili akiwa Mwanza peke yake [emoji1787][emoji1787]na kwa tuliofanyia Dar tulifanya pia na wadada wawili wa palepale KCB BANK tena wakiwa na Uniform za KCB [emoji1787][emoji1787]Nchi ngumu sana hii
Mm siku hiz naenda kuoga maji ya bahari Kwa muda wa mwezi alafu ntaanza kuomba ajira rasmi 😆
 
Back
Top Bottom