Vituko nilivyowahi kuviona kwenye sahili (interviews) vya kukatisha tamaa

Vituko nilivyowahi kuviona kwenye sahili (interviews) vya kukatisha tamaa

Kuna interview tulifanya pale Tambaza Sec. Tuli itwa interview na utumishi watu 98. B4 kuingia ilipaswa tukaguliwe vyeti na tuna saini mbele ya majina yetu.
Mm kwenda kusaini nika kuta tume fika 105. Daah. Bongo bhana[emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Watu hawakuitwa interview na Utumishi. Ila wame andika majina kwa mkono na kufanya Interview.
Matokeo ya Interview namuachia Haji Manara atangaze.
 
Mmoja wa delinquent member wa JF ni wewe, soma tena uelewe wapi nimeandika hayo uliyoyaandika?,mpumbavu na I can't help labda ungekua mjinga ningekuelewesha,uchunguzi wa tigo ni mmoja ya vigezo kabla hujapita kuwa jet fighter pilot cadet
Humu jf huwa kuna watu ni mashetani anataka akukere ili afurahi

Malezi mabovu waliyopata kutoka kwa mzazi wa hovyo ndo tatzo
 
Siji kuomba kazi taasisi binafsi Mimi nakomaa na ajila portal ukitaka kupoteza mda wako na pesa omba hizi taasisi.

Arusha city college mungu anawaona choma nauli mbeya to arusha na maladhi juu ila ata feed back amna dah maisha aya kama laki mbili imekatika. Mungu mwm ipo siku yangu inakuja.
 
2008 kuna jamaa tulikutana kwenye usaili wa JKT . Dogo kwa muonekano alitokea familia flani ivi duni afu za kidini sana mana alikuwa mnyenyekevu mpaka anaboa . Mimi tayari uhakika wa kupita ulikuwepo japo sikupenda kuwa mjeshi hivyo nilifata maelekezo tu.

Basi dogo umefika muda wakuhojiwa akatumwa sigara ile anarudi anaambiwa kachelewa dogo alilia mpaka makamasi kumbe ashaliwa pesa kibao toka wilayani then mkoani anakaziwa kijinga afu bosi mmoja akamwambia amepunguwa urefu fut3 wakati toka mwanzo ashapimwa na akapita. Dah! Ile hali ilinigusa sana nikajaribu kumshauri na kumpa moyo ndo akanambia kuwa mama yake kawekeza Sana ili ye aende jeshi mpaka kauza baadhi ya vitu vyake kuweka mazingira sawa. Basi nilichokifanya nikaongea na wakubwa walotamani niende jeshi kuwa me sivutiwi kwenda jeshi ila nafasi yangu kuna mtoto wamsaidie, basi wakanielewa wakampitisha ,aisee dogo hajaniangusha kapambana mpaka akapata nafasi na leo ni miongoni mwa connection zangu zinazonifanya nivimbe mjini apa.

My point : kama ipo ipo tu msikate tamaa ukiona umekosa ujue sio liziki yako ila kama ni liziki yako itakuja kwa njia yyt ile
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Nawasalimu wote kwa jina la Jamhuri ya Muungano.

Vijana tunapitia mengi ya kukatisha tamaa, lakini leo niwape machache ya vituko vya sahili nilivyowahi kuviona kwa macho yangu.

1. Tuliitwa kwenye usahili mikoa ya nyanda za juu kusini, basi kwa furaha na kujiamini nikapaki vitu huyooo nikafika siku moja kabla nikaripoti na nikakuta watu wengine, siku ya pili yake tukawahi sana tu,basi wakati tunaendelea kusubili wasahili wakafika na gari aina ya cruiser wakashuka kama saba hivi, sisi tukajua wote ni wasahili, lahaula kumbe wengine ni wasahiliwa kama sisi na tuligundua baada ya kuona wanakuja kukaa kwa wasahiliwa. Baada ya usahili matokeo nakuachia utabiri mwenyewe.

2. Tuliitwa kwenye usahili wa serikali basi wakati tunaendelea kusahiliwa basi kuna kijana sijui wa mkubwa gani akawa ameondoka eneo lile, basi unaambiwa alitafutwa balaa na mwisho wa siku matokeo yumo.

3. Kuna siku tunasubiri usahili,kuna vijana wakawa wanasema wameagizwa kuja hapo kama utani vile,aisee haikuwa utani matokeo yalitujulisha.

4. Tumefanya usahili,matokeo watu ambao hawakuwepo kwenye usahili ndio waajiliwa.

5.Umetoka umejiandaa na kile ulichosomea mfano mechanical engineering na vile vitu vinavyoendana na umejiandaa haswaa,unaingia wanaanza kukuzodoa,mara huyu aulize mambo ya demokrasi yaani ni ujinga tuu maadamu wakukere tu maana hawana mpango na wewe ni vile umekuja acha wapoteze tu muda,inakera acha tu.

Dah mambo ni mengi sana,ushauri wangu vijana msio na connection mkaze sana na kumuomba Mungu,lakini naamini kila kitu kinawezekana.

Kama una kisa ni ruhusa kuweka.
Katika life langu nimefanya sahili tatu tu na zote za kawaida tu ila moja nilienda kupiga usahili kampuni moja ya wa Israel, niliulizwa tu unajua nn kuhusu hiyo ishu niliyoenda kupga usahili hakuna cha umesoma wapi wala umezaliwa lini au leta sijui cv yako
 
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Niliwahi kuhudhuria interview moja miaka ya nyuma. Sasa nilipofika eneo la interview nilibahatika kubaini ya kwamba kuna watu tayari walishachaguliwa.

Sisi kumbe ilikuwa ni danganya toto. Nilishikwa na hasira sana.
Zamu yangu ilipofika nikaitwa kwenye panel kwa ajili ya kuulizwa maswali.

Baada ya utambulisho niliwachana live wale panelist. Niliwaambia hv nakumbuka "Samahani ndugu zangu nimekuja kimakosa hapa sikupaswa kuwepo kwasababu tayari mna watu wenu mifukoni" kisha nikatoka kwa speed. Kugeuka nyuma nikaona kuna karani amekaza mwendo kunifuata akiniita nikakaza mwendo nikapotelea kusikojilikana mpaka leo
 
Niliwahi kuhudhuria interview moja miaka ya nyuma. Sasa nilipofika eneo la interview nilibahatika kubaini ya kwamba kuna watu tayari walishachaguliwa.

Sisi kumbe ilikuwa ni danganya toto. Nilishikwa na hasira sana.
Zamu yangu ilipofika nikaitwa kwenye panel kwa ajili ya kuulizwa maswali.

Baada ya utambulisho niliwachana live wale panelist. Niliwaambia hv nakumbuka "Samahani ndugu zangu nimekuja kimakosa hapa sikupaswa kuwepo kwasababu tayari mna watu wenu mifukoni" kisha nikatoka kwa speed. Kugeuka nyuma nikaona kuna karani amekaza mwendo kunifuata akiniita nikakaza mwendo nikapotelea kuaikojilikana mpaka leo

ulifanya vizuri na ulipaswa kuwaambia live A,B,D zote waelewe ujinga wanaoufanya ni ujinga tu kama maujinga mengine.
 
Unaita mamia ya watu kwenye interview, watoto wa wenzio, huku ukijua kabisa ni formality tu mnafanya, ni dhambi kubwa sana.

Hizi kazi ambazo sio proffesional kiviile na zinahitaji hasa graduates au wenye uzoefu kidogo sana, huhitaji kuleta ujanjaujanja baadala yake wapime watu chukua wale wenye uwezo.
 
Hahahah! nimekumbuka kuna sehemu nilikuwa nafanya kazi kama "project coordinator" huu mradi ulikuwa unadhaminiwa na waitaliano....sasa kukawa kunahitajika mtu wa kufanya kazi ya kutoa elimu ya mazingira shule za msingi. Wale waitalianowakasema kuna jamaa walikuwa wanafanya nae kazi hapo kabla ila kwa muda huo alikuwa Dar aifundisha shule ya msingi, so walimemuita ili aje kufanya kazi hiyo, ila jamaa alikuwa anazingua kila akipigiwa simu anasema anakuja ila hatokei, basi wakaniomba nitangaza nafasi hiyo! basi ile nafasi nikaitangaza na siku ya Interview yule jamaa aliyekuwa akipigiwa simu mwanzo akatokea ( hiyo ni baada ya kumpigia tena simu). Sasa kumbe wakati wanasubiri kuingia kwenye chumba cha ushahili, huyu jamaa alikuwa akiwaambia wenzie kuwa ile kazi ni yake maana ameitwa kutoka Dar (walikuwa watu kama nane hivi), bahati mbaya siku ile usahili uliahirishwa! ila ukaendelea siku iliyofuata, sasa kutokana na tambao za yule jamaa siku ya pili walitokea watu wanne tu! Baada ya usahili aliajiriwa mtu mwingine na sio yule tuliyemuita kwa kumpigia simu! Kilichofuata sasa jamaa alinipigia simu na kuniwakia kinoma eti tumempotezea muda wake na nauli na kama vipi nimrudishie nauli yake! Mimi nilimmuliza tu kuwa kwani tulivyokupigia simu, tulikuambia tunakuja kukuajiri au kufanya usahili? jamaa kasema mlisema kuja kufanya usahili...nikamwambia basi umeharibu mwenyewe.....jamaa alinitukana na kukata simu!
 
Kaka yani umeenda kufanya interview ya public relations halafu kabla huja ingia kwenye oral uambiwe pasheni misuli kidogo kisha mrudi halafu wakati wakurudi ghafla wasaili wanasema walio rudi KWANZA ndio wameshinda usaili hiyo unaita fair?
Huo fair kabisa mkuu,kuliko mkimbie afu wengine wako ndani wametulia ndo wanapata kazi
 
Nawasalimu wote kwa jina la Jamhuri ya Muungano.

Vijana tunapitia mengi ya kukatisha tamaa, lakini leo niwape machache ya vituko vya sahili nilivyowahi kuviona kwa macho yangu.

1. Tuliitwa kwenye usahili mikoa ya nyanda za juu kusini, basi kwa furaha na kujiamini nikapaki vitu huyooo nikafika siku moja kabla nikaripoti na nikakuta watu wengine, siku ya pili yake tukawahi sana tu,basi wakati tunaendelea kusubili wasahili wakafika na gari aina ya cruiser wakashuka kama saba hivi, sisi tukajua wote ni wasahili, lahaula kumbe wengine ni wasahiliwa kama sisi na tuligundua baada ya kuona wanakuja kukaa kwa wasahiliwa. Baada ya usahili matokeo nakuachia utabiri mwenyewe.

2. Tuliitwa kwenye usahili wa serikali basi wakati tunaendelea kusahiliwa basi kuna kijana sijui wa mkubwa gani akawa ameondoka eneo lile, basi unaambiwa alitafutwa balaa na mwisho wa siku matokeo yumo.

3. Kuna siku tunasubiri usahili,kuna vijana wakawa wanasema wameagizwa kuja hapo kama utani vile,aisee haikuwa utani matokeo yalitujulisha.

4. Tumefanya usahili,matokeo watu ambao hawakuwepo kwenye usahili ndio waajiliwa.

5.Umetoka umejiandaa na kile ulichosomea mfano mechanical engineering na vile vitu vinavyoendana na umejiandaa haswaa,unaingia wanaanza kukuzodoa,mara huyu aulize mambo ya demokrasi yaani ni ujinga tuu maadamu wakukere tu maana hawana mpango na wewe ni vile umekuja acha wapoteze tu muda,inakera acha tu.

Dah mambo ni mengi sana,ushauri wangu vijana msio na connection mkaze sana na kumuomba Mungu,lakini naamini kila kitu kinawezekana.

Kama una kisa ni ruhusa kuweka.
Basi umekosea. Haukuwa ni usahili bali ya uswahili
 
Poleni mno generation hii, mtaumia sana na dawa ni kupanua wigo wa kuhangaika, kipindi cha nchi Ina heshima na adabu kulifanyika interview ya vijana kwenda kujifunza urubani wa ndege za jeshi na ufundi (601 na 603 KJ),waliletwa wataalamu kutoka China waendeshe hii interview, ilikua fair na kuhuzinisha kama hukupita hata awamu ya kwanza, urefu na wengi waliishia pale ,na looo pia walichunguza kwa maumba kama ulishatembelewa!!kwenye tigo jamani tumepitia mengi hapa duniani
Kizazi cha vijana cha sasa ni magoigoi wala siwaonei huruma. Mijadala yao yote ni ''jinsi ya kula tunda kimasihara'' au Yanga na Simba. Kwa nini hawaongozi kudai mabadiliko ya mfumo na serikali kuwajibika. Ndiyo maana hata serikali inawadharau na kuwaita kwenye interview eg watu elfu tano wakati nafasi zinazotakiwa ni mbili tu.
 
ila kuna michezo ya kipuuzi na kishamba mno huwa wanaifanya mibuyu ya baadhi ya wasailiwa.

wewe unajua kabisa huyu ntambeba na atapita,kwanini kila mtu aone na ajue hilo!!!unakuta jitu linashuka kwenye gari la moja ya maboss wa usaili,sijui ndio kuvimba au ufala tu!!!
Wanajua kabisa mi-tanzania ni kama mi-nyumbu haiwezi kufanya chochote ndiyo maana hawajifichi. Trust me. Nchi ambayo vijana wanajitambua hakuna anayethubutu kufanya hivi. Patachimbika!
 
Kizazi cha vijana cha sasa ni magoigoi wala siwaonei huruma. Mijadala yao yote ni ''jinsi ya kula tunda kimasihara'' au Yanga na Simba. Kwa nini hawaongozi kudai mabadiliko ya mfumo na serikali kuwajibika. Ndiyo maana hata serikali inawadharau na kuwaita kwenye interview eg watu elfu tano wakati nafasi zinazotakiwa ni mbili tu.
Umenena kweli mkuu na wakichezewa kule wanakimbilia huku kulalama
 
Ni wiki Tatu zilizopita niliitwa kwenye Interview KCB BANK MAKAO MAKUU DAR nafasi ya CORPORATE AFFAIRS MANAGER,kufika pale tupo Wasailiwa 12 na mmoja yeye anafanyia Usaili akiwa Mwanza(huyu ni staff wa KCB BANK MWANZA)!!![emoji1787]na katika 11 tulio Dar Wasailiwa wawili nao wadada ni wa palepale ndani KCB BANK Maka Makuu[emoji1787]Usaili tuliambiwa saa 8 mchana lakini ukaanza saa 10 jioni(ilikuwa ni Written Interview).Yaani tangu tumefika pale wale wadada(wa HR na Head wa Communications)wakawa wanajizungushazungusha weeee nikajua tu hapa USANII unachezwa!!!kuja kuleta hiko ki-swali Chao chenyewe eti (I)WHAT IS EVENT PLANNING??(II)PROCEDURES ZA EVENT PLANNING(III) EXPLAIN SHORTY ON THOSE PROCEDUCES OF EVENT PLANNING??
yaani ni ki-swali ambacho nilikijibu ndani ya dakika 10 japo wao walisema dakika 30!!!juzi napokea Email kutoka kwa huyo Dada HR anaitwa MONDE LUSHAKO eti nilipata below PASS MARK hivyo sijachaguliwa kwa Oral nilicheka mpaka nikapaliwa na Wine yangu!! [emoji1787][emoji1787] yaani ni wasanii walikuwa na mtu wao wahuni wale[emoji1787][emoji1787]na mimi nina uhakika kile ki-swali chao nilikipata chote 100 kwa 100!!nilimjibu kwenye Email yake kwamba WAMUOGOPE MUNGU na waache tabia ya kusumbua watu waje kwenye Interview wakati nafasi tayari wana mtu wao!!!hebu imagine wengine mpo Dar mnafanya Interview na mwingine(staff wa ndani KCB Bank humohumo) anafanyia Usaili akiwa Mwanza peke yake [emoji1787][emoji1787]na kwa tuliofanyia Dar tulifanya pia na wadada wawili wa palepale KCB BANK tena wakiwa na Uniform za KCB [emoji1787][emoji1787]Nchi ngumu sana hii
Mkuu naomba kupingana na wewe. 1. Kwa nini unadhani wafanyakazi wa KCB hawakuwa na haki ya kujaribu ku-apply? Kwani vigezo ni kuwa walitaka watu nje ya KCB tu? Hapa nadhani walikuwa sawa. 2. Pengine hiyo written Interview kuna waliofanya vizuri kushinda wewe. Unajua unaweza kudhani ulifanya vizuri sana kumbe kuna waliofanya vizuri zaidi. Uliona masahihisho ya mitihani ya wote ili uone wengine walivyojibu?
 
Back
Top Bottom