Vituko vya maisha ya uswahilini

Uswahilini ndio sehemu pekee ambapo huwa hakitupwi kitu yaani ukitupa wenzako wanaokota wanauza,
Utakuta banda jamaa wametundika bidhaa za mtumba zilizotumika yaani ni kawaida kukuta wanauza vijiko,miko, majiko,pasi,masinki ya vyoo yaliyotumika na yamechakaa,mpaka na miswaki ya mtumba utapata.!
 
Kwahiyo umepeta sana mchele wa maonyesho eh au majirani ndio walikua na hizo tabia? [emoji2] [emoji2]
Hahahaa. Sio mimi bana rafiki.

Nilikuwa naona kwa majirani, mie Dingi angu uwezo wa kununua mchele alikuwa anao bana na hata kama akiwa hana basi desh zilikuwa zinahusika ila sio kuigiza. Hahahaaaaa.
 
Hahahaa. Sio mimi bana rafiki.

Nilikuwa naona kwa majirani, mie Dingi angu uwezo wa kununua mchele alikuwa anao bana na hata kama akiwa hana basi desh zilikuwa zinahusika ila sio kuigiza. Hahahaaaaa.

Ngarenaro hiyo enzi hizo. Lol
Hahah!! Sawa rafiki nikajua ni wewe bhn
 
Hahahaaaaa. Ila rafiki Mungu anakuona aiseeeee.

Sababu sio kwa kujua huko.
Heheh!! Tena huko sio kuniona tu bali ni kuniangalia kabisa [emoji23][emoji23]
 
Uswahilini ukifua jinsi kali hupaswi kuondoka hakikisha unakuwepo hapo mpaka itakapokauka,pia choo hutumika kama bafu na mlango ni kpande cha gunia au kanga/kitenge kilichoisha
Ukija na mgeni ukimkuta mama mwenye nyumba lazma akuulize "huyo ndyo mchumba wako? na yule mwingine yuko yapi uliyekuja nae siku ile?" Just imagine unaulizwa swali hilo na mchuchu a.k.a your new side chick yupo hapo hapo
Kwa kifupi,uswahilini huwa hakuna ustaarabu (nimeishi Maeneo ya Mburahti kwa Ma Doto, na Manzese kuko hovyo sana)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…