Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Hapo kwenye huo uchochoro wa Chidumule ukinyosha, unapokata kona tu kuna saloon ya kike. Maajabu saloon yenyewe inahudumiwa na was.enge.
Kitambo sana hiyo mitaa ila nakumbuka ukinyoosha nyumba ya kwanza kabisa unavyokata kulia alikuwa anaishi mama mmoja mkulya somebody mama Ghati kama sijakosea,alikuwa mkorofi sana akitibuka anatukana matusi mtaa mzima pale.
 
Mwananyamala nilidumu week mbili na ushee kama siku 16 flani hivi nikahama ndani ya hizo hizo week mbili. Vioja vilivyonipata vinatoshea kumpata mtu kwa angalau interval ya miaka miwili mimi vilinikuta ndani ya week mbili za kuishi mwananyamala . Nikiwa ndio kwanza naanza maisha nilipata chumba nyumba moja hivi karibu na sokoni. Kwanza nyumba yenyewe ilikuwa na manyau balaa yaani palikuwa na biashara ya supu na makongoro nyumba ya pili sasa yale mapaka yalikuwa yanaruka ukuta yanaingia upande wa nyumba niliyokuwa naishi yaani ndani ya uzio wetu ndio kilikuwa kijiwe cha yale manyau yalikuwa mengi kuliko kunguru.

Kitu kingine kilichofanya nikikumbuka nacheka maisha ya mwananyamala ni Luku jamani Luku inakaa masaa yaani umeme ukiwekwa kila mtu anazama chumbani mwenye kunyoosha ana nyoosha faster mwenye kupika kwa jiko lake anapika kabisa bada ya hapo mnakula giza kama siku mbili mbele maana umeme wenyewe ulikuwa wa kupigia foleni pale mwanamboka. Halafu masela mle ndani walikuwa na maisha ya msoto tu pesa ya kudandia mwenye nyumba hakuwa anaishi hapo ilikuwa shida balaa

La mwisho lililo nitoa mbio hadi nikasamehe kodi ya miezi mitatu nilipata lijamaa linafanya biashara ya vinyago linaishi mwananyamala kisiwani kule karibu kwa mama mmoja hivi aliitwa Zagalo. Limakonde lile kumbe malaya wanaliwinda wakagundua linataka kutuliza mambo kwangu wadada ile mishangingi mishankupe wa mwananyamala wakanifuata natoka zangu kazini ile naingia ndani ndani tu wakaruka ukuta kupitia ile nyumba ya wauza supu pona yangu alikuwa kaka mmoja bouncer (siku hizi yuko red brigade) aliwazuia akawaambia atawachapa makofi ila walikuja na viwembe wanikate kate ki*si*i wasingeshindwa wale .

Nakumbuka nilishapigwa roba ya maana pale A nikaporwa simu na viatu , pete na hereni, nilishawahi kupanda daladala kinondoni makaburini hadi nafika komakoma handbag iko nje ndani ndani nje imekombwa kila kitu. Nilishawahi kurudi room nikakuta nguo zimevutwa kupitia dirishani mchana kweupee hadi shuka lilivytwa likakwama kwenye tundu la kutolea kwa timbwili lile nilijikuta nasamehe kodi yangu nikaikimbia mwananyamala nikasogea mkwajuni kidogo kabla sijadumbukia chama la wana TMK. Ile mwananyamala ilikuwa tamu ila ndio hivyo nilitoka nduki [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Waonesha muvi, bubu,mbwana,rashd matata n.k ful kolokolo pale ....kamali asubuhi ,mchana muv usiku pilau,kishoka hahaha kuna siku nilitoroka hom kwenda kucheck pilau mida ya saa 5 nkaingia nkakaa mbele kabisa chini ile nageuka nyuma nakuta mjumbe wetu wa nyumba kumi nae ndani ya nyumba daaaaah
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mtaa wa wibu ni mateja na madawa na si mashoga.
Labda wibu ya sasa lakini kipindi hicho ndio sehemu pekee Dar na pengine Tanzania shoga kumiliki Pub.. Aunt Abuu
 
Pale karibu na hosptal ya mwanayamla kuna KAM dispnsary kuna siku wahuni walikwenda kuifunga ile KAM kuna kijana mmoja mzamini wa wahuni yanii wahuni wakiiba huko simu sijui handbag yeye ndio taita anawapa cash...yule Don wao kuna siku jino limemsumbua akaenda pale KAM doctor aliyemkuta zamu ameshapiga vyombo banana enzi hizo docor kampiga sindano ya ganzi fresh doctor ameacha jino bovu akatoa jino zima dah yule Don akatiwa pamba mdog mdog mpaka home ganzi inakwisha anagundua jino bovu lipo duh huo mtiti wake sio mdogo wakawambia wahuni wake leo sina pesa nimeumwa jino nimekwenda kutoa doctor kazingua wahuni wakatia timu pale KAM wanadai jino la Boss wao lile zima arejeshewe vumbi balaa wahuni waliondoka mpaka na mikasi na doctor juu juu wakaenda nae ujiji huko
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] ikawa ndani ntiti... Nje ntiti
 
Pale karibu na hosptal ya mwanayamla kuna KAM dispnsary kuna siku wahuni walikwenda kuifunga ile KAM kuna kijana mmoja mzamini wa wahuni yanii wahuni wakiiba huko simu sijui handbag yeye ndio taita anawapa cash...yule Don wao kuna siku jino limemsumbua akaenda pale KAM doctor aliyemkuta zamu ameshapiga vyombo banana enzi hizo docor kampiga sindano ya ganzi fresh doctor ameacha jino bovu akatoa jino zima dah yule Don akatiwa pamba mdog mdog mpaka home ganzi inakwisha anagundua jino bovu lipo duh huo mtiti wake sio mdogo wakawambia wahuni wake leo sina pesa nimeumwa jino nimekwenda kutoa doctor kazingua wahuni wakatia timu pale KAM wanadai jino la Boss wao lile zima arejeshewe vumbi balaa wahuni waliondoka mpaka na mikasi na doctor juu juu wakaenda nae ujiji huko
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] ikawa ndani ntiti... Nje ntiti
 
ma kisholi je,nyuma ya daladala camp pale mtaa wa kwanza,anapika kitumbua cha mwisho akiweka kwenye kikaango kuna mteja anasubiri.
vijana wake wote ni vibaka watakatifu
Bonge la fundi yule mama
 
Mshana, huu uzi ni bomba mbaya. Unasaidia kuwafungua baadhi ya watu kuhusu mitaa wanaishi. Kaka tukimaliza mwananyamala usicheleweshe, tuletee na mtaa mingine mkuu
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] tutahamia Manzese midizini Mburahati mpaka Kigogo bila kusahau Mabibo moja... Kuna beach kule
 
Siku moja niko Chaga bite pale Makumbusho nikapigiwa simu nirudi haraka home kuna movie ya bure
Kufika nikaongozwa Kamanyola... Aisee niichokiona... Basi TU... Kuna mhuni alimtongoza house girl wangu halafu wakaenda kamanyola. Sasa eti jamaa akaacha pazia wazi wana wajifaidie pilau halisi
 
vipi kuhusu nzega katika kuwa na majambazi sugu katika nchi;japo wengi walishachukuliwa na watu wasiojulikana.
 
Back
Top Bottom