Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Now wana mgambo mmoja hivi wa maduka matatu
Siku hizi napita tu pale ila miaka ya nyuma siku mmoja polisi wa mwinyijuma walimkama mlinzi wa nyumbani kwetu kino kwa kosa la uzururaji so wakati napita akaniona akaniita na kuniambia nikamwite maza polisi walivyosikia hivyo wakaogopa sana maana walikuwa hawamjui na hawajawahi kumuona ila walikuwa wanaambiana tu wenye nyumba ila ni wafanyakazi wa usalama wa taifa basi maza alipofika wala akuuliza akawaambia mtoeni kama wakamtoa kwa uoga wa kutojua. Kumbe bi mkubwa alikuwa anafanya kazi sigara. Basi nikawa nikipita hata mimi wananiogopa, one day tuko home nje maskani na wanangu mpaka saa 9 usiku wakapita polisi wa obey wakataka kutukamata wakaambia hao waacheni msiwaguse hata kidogo. Basi ikawa burudani usiku ni vibaka wala kukwamatwa na polisi
 
Sifa nyingine ya mwananyamala,vijana wengi sana wamekimbilia South,wapo waliomaliza 10-20 yrs huko SOUTH.
Weng sana wapo Bondeni,hawana idadi
Wengine wamezagaa ujerumani, china na uingereza hasa wale waliokuwa wanachaza sarakasi. Ila wale waliokuwa makonda na madereva wangi wako south zaidi ya miaka na miaka kama hawana kwao wala ndugu
 
Kuna wapga chabo maarufu mwalimu wa msufini na bon jove wa shoka hawa walikuwa na vyeo kabisa vya upigaj chabo,nakmbuka mzee kamanyola aliajir wamasai walinde watu wasipige chabo matokeo yake haohao wamasai ndo wakawa wanapiga chabo ikabidi watimuliwe wakazungushia ukuta usawa wa madirisha ikawa ndo kama wamerahisisha kaz kwa wazee wa chabo maana walikuwa wanaingia ndan ya ukuta wanachek muv la bureeeeew
Mama weee..! Mbavu zangu.[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Mwananyamala wageni ni wanyasa na wazaire (wakongo) wapo wengi sana nakumbuka kuna mnyasa wahuni walimpa kopo la maji safi na jero akanunue umeme wa LUKU kule Garden kituo kimoja mnapanga mstari km 2hours mnyasa akasota kishenzi ktk ile jam kufika dirishani zamu yake ya kutoa card ya tanesco yeye akalipitisha kopo lake lile akajidia "ngasema wale ujazie wa mia tano " ...***** wakongo wa mwannyamala nao wameshakuwa masera wameambukizwa tabia zile zile kuna mmoja alipanga room ya giza kwa bibi frola bibi wa kimakonde ila mtaani kutwa kutembea na gitaa mrefu huyo papaa kuna madada wakajitia kumjua sana papaa papaa wakampa kazi salon kwao kitengo cha kucha sijui nini papaa yule anakuja kwa salum karanje mtaalam wa pesa bandia papaa yule ananunua pesa bandia anawachanganyia wale madada ktk pesa za mahesabu ya siku...siku nyingne anachomoa fuse ktk draya anajitia hii mbovu madada wanaangaika pale kuiwasha ddraya papaa mwisho anafata fundi mtaani kwake anachukua muhuni mtaani anampanga fresh muhuni akifika pale anajitia fundi ata 2hous analifanyia matengenezo lile draya mwisho wa mchezo fuse inarudishwa draya linapiga kazi fundi analipwa pale km 20 au 30 papaa anamsindikiza fundi wanapiga half half
 
Vibaka wezi hawa maarufu hawatakaa watokee tena.. Nina historia nao.. Mjushi anawafahamu vema kila mmoja kwa sekta yake
Morroco
Kumbwiga
Tito
Jumanne
Pembe
Walinitengeneza nami nikawatengeneza ngoma draw... Tukaenda sawa.. Sasa hivi wanakula bata akhera
Uliwafanyaje, nimeanza kukuogopa mshana[emoji23]
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji85] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji3] sana tuu[emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji3] [emoji3]
Inaonekana mshana aliishi au anaishi huko.
 
Nimeondoka hapo kitambo sanaa hivi ule uwanja wa spurs bado upo ,aise pale ilipigwa mechi moja Kali miaka ya 2001 Kati ya faru dume ya manzese na timu nyingine nimeisahau aise ile mechi baada ya firimbi ya mwisho tu uwanja ukageuka kuwa wa vita.
Nevada tandale sokoni
 
Nimeondoka hapo kitambo sanaa hivi ule uwanja wa spurs bado upo ,aise pale ilipigwa mechi moja Kali miaka ya 2001 Kati ya faru dume ya manzese na timu nyingine nimeisahau aise ile mechi baada ya firimbi ya mwisho tu uwanja ukageuka kuwa wa vita.
Amsterdam hapa uzuri makaburini ilikua timu ya fujo nayo
 
Sifa nyingine ya mwananyamala,vijana wengi sana wamekimbilia South,wapo waliomaliza 10-20 yrs huko SOUTH.
Weng sana wapo Bondeni,hawana idadi
Mwananyamala imekua hivyo kwa sababu madon wale wa mjini kitambo sana ndio walikua wakiishi huko. Kuna don mkubwa sana wa kufoji documents zote za bandarini akiitwa For Cash alishafariki kitambo sana ndio alikua akiishi huko Mwananyamala B; baadae akina marehemu John Ngogo wote walikua pale kabla pesa haijakubali. Na mazungu ya unga yote makubwa enzi hizo waliishi Mwananyamala na Kinondoni. Na ma don kibao tu ughaibuni maskani yalikua Mwananyamala.Huku ughaibuni ni kama Mwananyamala ingine imemove tu huku tupo kibao. Undava wa hicho kitongoji umeanza kitambo sana. Coaster nyingi za mjini zilimilikiwa na madon wa huko na kinondoni akina marehemu Juma Jimmy Lover.
 
Dah.! Umenikumbusha mbali sana mkuu yaani tukisema kila mtu arudie kazi yake ya zamani...!
Mfano mimi nilikuwaga na washkaji flani tukawa tunaiba mafuta ya transformers ila sintosahau siku tulipoparamia transformer flani ghafla ulisikika mripuko wa ajabu kufumba na kufumbua mwenzetu mmoja alikufa pale pale mwingine alifia hospital kuanzia siku hiyo niliacha kabisa kazi hiyo.
Namshukuru Mungu sa ivi niko zangu Dom nna banda langu natengeneza na kuuza majeneza na maisha yangu yako fresh nimejenga,nimeoa na nnamiliki
"Kagari" japo ni kama kale ka Mr bean.[emoji1] [emoji1] [emoji1] maisha yana historia ndefu sana.
Mungu anakupenda sana wewe jamaa
 
Ninachowakubali wahuni wa mwananyamala wakikujua hawakukabi utaombwa ya fegi tuu..***** sasa uwe wa kuja shughuri utaipata...

Alafu watu wanajuana Kwa aina ya wizi utasikia furani huwa havunji Ila kama dirisha limekatwa nyavu huyu atakuwa flani tuu basi wananzengo wanamfata arudishe alichoiba kwa amani kabisa.
Mwananyamala mpaka wazee wa miaka 60 na wenyewe wakiongea lazima washushie na TUSI. Maeneo haya TUSI ni kama kiungo cha sentensi, utasikia KUMAMAEWALAI yaani TUSI linahusishwa na mungu
 
Kuna siku bado nipo mdogo nipo form two nimekatisha makaburini mwananyamala mda km saa mbili usk nakwenda CAMP (kujisomea na wanafunzi wenzangu ili uingie form three kuna wastani) nakatisha pale makaburin wametoka jamaa moja mbele yangu gafra tu mara huku nyuma wametokea jamaa wawili nikawa nipo katikat flani hivi ila bado kuna distance yanii awajanifikia wala sijawafika ila nishagundua hawa ni wandewa...sasa kwa mbali kunasikaka sauti ya mnanda(mchiriku) maeneo ya kwa kina mbamba huko chaukucha..nikaona dah leo nimekwisha sina simu, sina pesa ila wahuni awawezi kunielewa km mimi denti tu. fasta nikajitia kuimba wimbo wa mnada " washa shideo eeh shideo washa shideo eeh shideo huku naelekea mbele alipo yule mmoja wahuni wakabaki pending kama vile wanajiuliza huyu ng'ombe au mwenzetu??huyu muhuni mwenzetu au?? Wakiwa wamestuck nilikatisha katikati yao kama air force one[emoji125] [emoji125] [emoji125] vitendo vyote vilifanyika sekunde kadha kuwasoma na kuwaact na kutoka speed
Umenichekesha sana, uswahilini miyayusho sana. Kuna jamaa angu alikuwa anakaa nyuma ya izi fremu zinazoangaliana na hospital ya mwananyamala alikuwa anapenda nyimbo za michiriku na minanda, sasa miaka ile ya 2000 pale makongo secondary alikuwa anapenda kuimba imba izo nyimbo kalibia na mti Mkubwa wa mbuyu maeneo ya hall ya mitihani, sasa siku iyo, anaimba imba na kimvua mvua kilikuwa kinapigapiga, akatokea afande mmoja anaitwa Miraji(Marehemu kwa sasa) akamuuliza wewe kijana njoo apa, na awo wote wanaosikiliza akamuuliza wewe pale mwananyamala tukipita na gari asubuhi na kukuta kituoni ni kwenu, jamaa kusema ndio afande akasema wote wanaojijua wanatoka kipande icho kaeni pembeni, kilichofata adhabu ya kwenda kufyeka, afande miraji akawa anasema nyinyi mlitakiwa muende bagamoyo mkajifunze sanaa
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] kweli mkuu si pale nyumbani kwa kina amini yule muimba mziki.ray c ndo ilikuwa maskani watu wamemlalua sana pale kino mahakaman
Duh!nimekaa sana ghetto hiyo mitaa,kuna kichochoro flani matata sana kati ya ukuta wa mahakama na nyumba ya mzee Chidumule hapo wanachuo wa Tumaini wamekwapuliwa sana simu,laptops na hela kisha masela wanakimbilia kwenye madimbwi yale nyuma ya Kambangwa Sec.
 
Duh!nimekaa sana ghetto hiyo mitaa,kuna kichochoro flani matata sana kati ya ukuta wa mahakama na nyumba ya mzee Chidumule hapo wanachuo wa Tumaini wamekwapuliwa sana simu,laptops na hela kisha masela wanakimbilia kwenye madimbwi yale nyuma ya Kambangwa Sec.
Hapo kwenye huo uchochoro wa Chidumule ukinyosha, unapokata kona tu kuna saloon ya kike. Maajabu saloon yenyewe inahudumiwa na was.enge.
 
Back
Top Bottom