Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Keko kuna balaa toka enzi na enzi mpaka kesho ,keko usiende kuishi kila aina ya usela uko huko ,mchana kweupe unakabwa na watu wanaendelea na shughuli zao ,kijana wa miaka 16 anakushikia panga mchana,keko pasua kichwa watoto na watu wa huko wameshindikana ....keko kuna story tamu hope Uzi wake utafunguliwa

Magomeni pako poa sio kihivyo ,magomeni kagera mpaka Argentina hupenda sana michezo ya ngumi na vijana wengi wameingia huko ndio kwakina Thomas mashali huko kila mtu anajifanyia bondia

Mwembechai,mikumi,mapipa palikuwa hot lkn sio kama keko,mwananyamala,kigogo nk ..binafsi ni mzoefu wa magomeni mapipa mitaa ya suna huku ukitaka druglords ,watengeneza hela feki utawapata ,matapeli ,watoto wa mjini utawapata mpaka watoto waliosumbua miaka ya 2014,2015 kwa jina la panya road utawapata wakazi wa kinondoni wanawafahamu sana hawa


Ila kigogo,keko,Tandale ndio yanashabihiana na mwananyamala ..magomeni utundu upo ila maisha ya huku yapo medium kati kwa kati ndio maana kuna utofauti na mitaa tajwa hapo juu hivyo usela sio sana kama huko ila pachangamfu

sure mm nimekulia magomeni kagera nimesoma karume p/s, mtaani lazima ujue kupigana
 
Ahahhah kilichokuchekesha nikikumbuka nilikula ice cream zile za ukwaju na ninavyopenda ukwaju sasa mbona kila siku nilikua nawahi ili nipewe dell niuze
Kilichonichekesha eti halikuwa haesabu
 
Wanga wa m/nyamala washafanya yao.
Inawezekana aliamka anaumwa kichwa sana akamwambia mama akee akamuitie ostadh amsomee duwa ostadh kufika Amina masikini ameshakata roho
 
[emoji41][emoji41][emoji41] kweli nilisoma vibaya jaman siunajua uzee nilionao
Sio kwamba unamsumbua kale kadadaaa make unabopendaga kukaa mbali na kukaitaa kaziii hipoooo
 
Ungepita kipindi hiko baba.
Sasa hivi wakabaji wote wameshakufa na wezi wengi wanaendesha boda boda
100% nakubali......miaka ya tisini mpaka 2002 kuanzia m/nyamala A kwenda mpaka kwa M/zakaria ilikuwa hatari sana....kuna zile nyumba za kota (M/nyamala A) jamaa walikuwa wanakaa kwenye vile vichochoro. Na ndipo roba za mbao zilipoanzia.
 
100% nakubali......miaka ya tisini mpaka 2002 kuanzia m/nyamala A kwenda mpaka kwa M/zakaria ilikuwa hatari sana....kuna zile nyumba za kota (M/nyamala A) jamaa walikuwa wanakaa kwenye vile vichochoro. Na ndipo roba za mbao zilipoanzia.
Vichochoro vyote siku hizi hamna watu wamevunja nyumba zao na kujengwa upya ilikua ukipita kichochoro hiki unatokea mtaa wa pili siku hizi ukianza kuingia mtaani moja kwa moja mpachi chini utokee mtaa wa pili
 
Back
Top Bottom