Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Nasikia kuna wizi wa majeneza umeibuka msisiri B... Mzee mmoja anasema anashangaa miaka yote haijawah kutokea[emoji3]
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
mshana jr ebu nifafanulie mtaa wa Pamba Street pale Mwananyamala A, una kasoro gani? Nasikia ale kuna Mze mmoja hivi alikuwa mchawi kishenzi na alikuwa anafanya kazi bandarini. Huko bandarini watu wakimuudhi tu hupotea majini na pale mtaani kwao watu walikuwa hawakanyagi. Una ufahamu wowote juu ya huu mtaa? Mimi nilkuwa natokaga na demu fulani toka pale na ndipo nilipokuwa nasikiaga hizi story za kutisha ila huyo mze mwenyewe sijawahi kumuona.
Mmh hili ngoja nitaenda huko weekend hii
 
Namkumbuka mama zakaria bonge, nishabeba Binti yake naye anamzigo wa haja nampeleka beach tunamalizana Huku huko, sijui yupo pale, mkubwa siyo yule mdogo
 
kumbukumbu yangu ya nyamala ni ule uwanja wa B...yani lolote linaweza kutokea kabla,katikati na baada ya mechi
wahuni wanavuta bangi mbele ya askari
enzi hizo gemu za ndondo watu wanakuwa na majeshi mastaa,akina lunyamila,mohamed hussein mmachinga,said msasu(huyu alitokea timu ya kitaa chetu hadi akaenda simba)
tulikuwa tunatembea kwa mguu tokea mwembechai,tunadondokea tandale kwa tumbo flani,tunavuka kimto cha kizushi(daraja mti mmoja mwembamba,usipokuwa good balancer unadondokea majini ukitoka kambale wamekudandia nguoni)
kwa ufupi mwananyamala ni nyoko..my favorite spot ni masai these days....nyapu nje nje
Tushaenda kucheza mikoroshini chini pale na American embassy, sijui ilitokea nini nikaacha jino, mimi nacheka tuu
 
Huyo shoga mpaka huku minazini njia ya kwenda sokoni karibu na kwa kina sharifa hivii nyumba ya kwanza kushoto alikua anakaaa hapo kulikua kuna mashoga wengi tukipita toka shule tunawashangaa wanavyokaa kibarazani vipiii unamkumbuka jack amabae sasa hivi ni shoga maarufu
Walikuwa na sehemu yak hapo wanafanya birthday parties, ukipiga deo unashangaa wanaume wana shanga kiunoni
 
Ukiwa umekulia dar watu Wa Mwananyamala lazima ukutane nao ktk mpira ndondo au ligi za mchangani , beach club au shuleni lazima waraouathiri tuu au utapata story zao au kuzushuhudia
Mbona mechi za tandale huzikumbuki na ngumi zake
 
Mbona mechi za tandale huzikumbuki na ngumi zake
mkuu nimeongelea kwa ujumla sana mimi kwetu luhanga , Kigogo na Mburahati. Sijakaa mwananyamala nilikuwa mpitaji tuu na ni bado mpitaji. story nyingi za watu wa huko utazipata au utashuhdia ktk mechi zao na hapo ni mpaka timu yetu ikutane na za huko ktk ligi amabazo mara nyingi makurumla na kinesi.
moja ya ninachokikumbuka ni kama mnachezaza na timu za huko ni lazima mjiandae na wababe wenu wawepo. nakumbuka kuna jamaa anaitwa EMMA kama sikosei alikuwa anasaidia sana timu za kitaa.
ila mwananyamala inasifika hata kipidi kile tunaenda coco beach kipindi cha skku tulikuwatunacheza mbali na namba za mbagala tandale na mwananyamala yaani ilikuwa mnajulikana kuwa hamtokei mitaa hiyo kwanza mnakuwa na hofu na piga ua mtakuwa outnumberd wao lazima wawe wengi tuu.
 
Mwananyama kwa utemi sasa kila kona kuna Gym, kuanzia vijana, komakoma, A, kisiwani kwa kidile...mirembe gym(hapa kuna gudu, dole) kwa mwalami gym( salum kiwiku) one nil gym( obede ngumu jiwe) bwawani huku kwa stevn nyerere (manchester gym shafii mashetani, albeto)...utemi utemi tu ktk mechi za mchangani LIGI ZA MBUZI game inapigwa pekupeku hio na wanaocheza ni baba flani watu wazima kabisa ndio alipotokea KANIKI huwa game aimaliziki lazima kiwake tu
unanikumbusha mbali ujue..
 
Back
Top Bottom