MOTOCHINI
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 28,064
- 31,401
- Thread starter
- #21
Uwezo wa serikali yetu kununua mahindi toka kwa wakulima ni mdogo ukilinganisha na kiasi kinacholimwa.
Wakulima wetu hawana uwezo wakuhifadhi mahindi yote wanayovuna kutokana na uwezo wao mdogo na njia zakuhifadhi mahindi yasiharibike.
Wakiuza kwa bei nzuri angalau (kwamajirani) japo nao waboreshe maisha yao serikali inaleta nongwa.
Sasa hawa wakulima wafanyeje? Ukizingatia soko la ndani limedorora na wanauza kwahasara!
Huku wakulima hao hao wana mikopo kwenye mabenki, vikoba, Sacco's bila kusahau pembejeo wanataka chao.
Hapo mi ndio nashindwa kuelewa hii nchi yetu ni yaaina gani. Kila kitu siasa
Kuna vitu vyakuleta masiala sio Hili sawa!!
Hivi unaijua njaa?