Vituo vitano vyafungiwa, vyafutiwa leseni kwa kuuza mafuta juu ya bei elekezi

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imevifutia leseni za uuzaji wa mafuta vituo vitano, kwa makosa ya kuficha, kutouza na kuuza mafuta juu ya bei elekezi huku ikotoa onyo kali kwa wauzaji wa nishati hiyo wanaojaribu kufanya hujuma na kukiuka maagizo ya Serikali.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa Ewura, Titus Kaguo, alisema uamuzi huo umechukuliwa baada ya tathmini ya kina iliyowawezesha kubaini kuwa kuna sababu za makusudi kwa wauzaji hao kuhujumu uuzaji wa mafuta.

Alisema katika uchunguzi wa awali uliofanywa na Ewura, kuna dalili za wauzaji wa mafuta kufanya hujuma kwa kuwanyima wananchi mafuta kwa makusudi na kutoa onyo kwa waauzaji wote kutofanya hujuma ambazo zitawaingiza katika uhujumu uchumi.
 
Sto

Swahili Cri

Story ina upungufu. Sometimes haina haja ya kupost story inayoacha maswali mengi kwa wasomaji kuliko majibu
 
Nimeshangaa
Hivyo vituo mbona havijatajwa?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wakitaja vitu 10 unatakiwa uamni kitu kimoja tu, naona wanatia mkwara tu, tokea majuzi kuna shida ya mafuta, naona folen vituon na wese hakuna

kuna maeneo lita ni 3000 kwasasa, i think kuna sehem wamekoroga huko wenye vituo wakaamua punguza kidogo kusambaza wese
 
Kama wapi mfano lita ni 3000?!
 
Hivi bei ya mafuta soko la dunia imekaaje au hawa jamaa wameona kwasasa wanapata hasara kuendesha biashara sababu ya kuchuka kwa bei ya mafuta katika soko la Dunia....?!
 
Kuna siku niliingia victoria nikaambiwa petroli imeisha, wakati siku zote mafuta huwa hayakauki hapo. Nikaona isiwe tabu nikaenda Total. Nashauri safari nyingine ewura waje na bei ya buku ili wafiche vizuri mafuta..
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wakitaja vitu 10 unatakiwa uamni kitu kimoja tu, naona wanatia mkwara tu, tokea majuzi kuna shida ya mafuta, naona folen vituon na wese hakuna

kuna maeneo lita ni 3000 kwasasa, i think kuna sehem wamekoroga huko wenye vituo wakaamua punguza kidogo kusambaza wese

Duh .huku ni 1545
Rahaaaa
 
Back
Top Bottom