Vituo vya afya sita vyajengwa Wanging’ombe ndani ya miaka miwili ya Rais Samia

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Rais Samia Suluhu alipoingia madarakani aliipa sekta ya afya kipaumbele maana anajua afya ndio msingi wa Maendeleo hivyo amejenga na kuboresha vituo vya afya maana aliahidi kusogeza huduma ya afya karibu na wananchi.

Rais Samia Suluhu Hassan ameimarisha utaoaji wa huduma za afya katika Halmashauri ya Wanging’ombe ambapo amewezesha Ujenzi wa vituo vya afya sita katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wake vituo hivyo ni Saja, Usuka, Ilembula na Imalinyi vimeshakamilika na ujenzi wa vituo Vya afya Vya Wangama na Igima vinaendelea na Ujenzi kukamilika kwa vituo hivyo vimesaidia kusogeza huduma za afya kwa Wananchi na kupunguza gharama za kufuata huduma za afya mbali.

Huu ni muonekano wa vituo vya afya vilivyokamilika chini ya Rais Samia Suluhu

Hakika mama ameonyesha uimara
majengo pekee hayasaidii.lazima pia kuwepo na watendaji.majengo hayatibu bali watendaji ndo wanaotibu hivyo afungue na ajira za watendaji wa afya ili mambo yaende sambamba.
 
majengo pekee hayasaidii.lazima pia kuwepo na watendaji.majengo hayatibu bali watendaji ndo wanaotibu hivyo afungue na ajira za watendaji wa afya ili mambo yaende sambamba.
Ni kweli unachoongea mkuu lakini ninachojua tayari wameshapangiwa tayar katika vituo vyao ...labda useme idadi yao ni ndogo
 
Ni kweli unachoongea mkuu lakini ninachojua tayari wameshapangiwa tayar katika vituo vyao ...labda useme idadi yao ni ndogo
wengi wamepangiwa japa vituo tuseme ukweli bado avijakamilika halmashauri nyingi wanamuangusha mh rais kwa ili kwann ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…