Vituo vya habari vyapigwa rungu na TCRA kwa kurusha maudhui katika muda ambao watoto hawapaswi kuangalia ama kusikiliza

Vituo vya habari vyapigwa rungu na TCRA kwa kurusha maudhui katika muda ambao watoto hawapaswi kuangalia ama kusikiliza

Inama nipachike rungu, papasa kichwa nisafishe mtaro!

Kongole Wasafi.
 
Mbona hotuba Q
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevitoza faini ya Sh milioni 30 vyombo vya habari sita, kwa kukiuka kanuni na maadili ya utangazaji ikiwamo redio ya Clouds FM kuzungumzia supu ya pweza kuimarisha tendo la ndoa katika muda ambao wasikilizaji wanaweza kuwa watoto.

Mbali ya Clouds FM, vyombo vingine vilivyoadhibiwa ni East Africa Radio, na televisheni za Star, Sibuka, na Global Tv na Duma Tv.

Akisoma uamuzi huo jana jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Joseph Mapunda alisema vyombo hivyo vilikiuka kanuni za mawasiliano kwa nyakati tofauti.

Mapunda alisema redio ya Clouds FM kupitia kipindi chake cha Jahazi, walihamasisha vitendo vya ngono, kwa kutumia supu ya pweza katika kuimarisha tendo la ndoa kwa muda ambao wasikilizaji wanaweza kuwa watoto.

Alisema baada ya kusikiliza utetezi wao, wanatozwa faini ya Sh milioni saba na kupewa onyo kali baada ya kuwatia hatiani kwa kosa hilo.

Katika shauri lingine, kituo cha Duma TV kimetozwa faini ya Sh milioni saba na kufungiwa kuchapisha maudhui kwa muda wa mwezi mmoja ili wajipange na kuzifahamu kanuni na kuzingatia weledi na maadili ya utangazaji.

Mapunda alisema Duma ilikutwa na hatia ya kukiuka kanuni kwa kuchapisha na kutangaza maudhui yenye lugha isiyo na staha na iliyo na udhalilishaji wa kijinsia kwa wanaume na wanawake.

Alisema redio ya East Africa imetozwa faini ya Sh milioni tatu na kupewa onyo kali kwa kukiuka kanuni hiyo, kwa kurusha maudhui ya kukashifu utendaji wa serikali kupitia uteuzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kutumia lugha ya kashfa dhidi ya utendaji wake.

Vilevile Global Tv imetozwa Sh milioni saba na kupewa onyo kali, baada ya kupatikana na hatia ya kuchapisha picha ya mnato na kutangaza maudhui yasiyokuwa na lugha ya staha na yenye kushabikia vitendo vya mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja.

Mapunda alisema maudhui hayo, yangeweza kuwaumiza na kuwakwaza waumini wa dhebebu la Anglikana na Watanzania kwa ujumla. Pia, alisema Sibuka Tv inatozwa faini ya Sh milioni tatu baada ya kupatikana na hatia ya kushabikia mauaji ya kutisha katika muda, ambao watoto wanaweza kuwa sehemu kubwa ya watazamaji.
Mbona hotuba za JPM zina mambo mengi yasio faa kusemwa hadharani
 
hela ya uchaguzi/kampeni inavyotafutwa

Sent using Jamii Forums mobile app

Hapa kinacho tengenezwa ni Hofu na ikisha enea zaidi ya hapa kuelekea Uchaguzi Mkuu wimbo ni mmoja tu ,Taasisi ni Mhimili wa Serikali na hao Watu (Viongozi wa Taasisi) wana tokana na alie juu.

Nje ya hapo ni kweli pana Matangazo megine ambayo huwekwa sio ya Staha na haya zingatii Muda, yani linawekwa Tangazo upo na Madogo kwenye Usafiri mpaka unaangalia chini kwa Aibu.Ni vyema kujenga Taifa la Watoto wetu wenye Maadili labda Siku Moja atatoka Mtawala ambae atakuja kuwa kamata
Watawala wa Sasa wanao vunja Sheria.
 
redio ya Clouds FM kuzungumzia supu ya pweza kuimarisha tendo la ndoa
HUYO MUANDAAJI WA KIPINDI AFIKISHWE MAHAKAMANI TAFADHALI SANA TUMEOMBA.

PIA SERIKALI TUNAIOMBA IONGEZE VIWANGO VYA FAINI ILI IWE FUNDISHO KWA REDIO NYINGINE. TUNAZITAKA REDIO STATIONS ZOTE ZIFUATE MAADILI YA KITANZANIA NA SIO KIMAGHARIBI.
 
25 May 2018

Maudhui Mitandaoni Sheria ya Mwaka 2018

TCRA watoa leseni kwa Blogs na Online TV, waeleza sababu kuu 3

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekabidhi leseni za kufanya huduma ya kutoa habari kwa njia ya mtandao kwa Blogs, Online TV na Online Redio ambazo zimekamilisha usajili.



Bongo5 na Michuzi pamoja na Lemutuz ni moja kati ya Blogs na Online TV ambazo zimekabidhiwa leseni ya kufanya huduma hizo huku baadhi ya blogs kama Muungwana, Millardayo, Mwanaharakati na nyingine nyingi zikipewa leseni ya kurusha matangazo kupitia blogs pekee.


Source : Bongo5

Bado TCRA wajiongeze, watupie jicho YouTube maana baadhi ya akaunti za waTanzania wanaolipa leseni za online TV kwa TCRA zilizopo chini ya uangalizi wa serikali ya sikivu ya Awamu 5 kulinda maadili huko mitandaoni wanakuwa na maudhui tata sana yanayoweza kutazamwa na watoto wadogo muda wote iwe asubuhi, mchana yaani 24/7
CCM Oyee! Maendeleo ktk Maadili Hayana Chama !

.
 
HUYO MUANDAAJI WA KIPINDI AFIKISHWE MAHAKAMANI TAFADHALI SANA TUMEOMBA.

PIA SERIKALI TUNAIOMBA IONGEZE VIWANGO VYA FAINI ILI IWE FUNDISHO KWA REDIO NYINGINE. TUNAZITAKA REDIO STATIONS ZOTE ZIFUATE MAADILI YA KITANZANIA NA SIO KIMAGHARIBI.

Acheni double standards!

Supu ya pweza eti ni uvunjifu wa maadili, wakati huo matangazo ya tiba mbadala za nguvu za kiume kila pale.

Kuna kipindi nakumbuka mamlaka zilipublish dawa fulani kuwa inafaa!!
 
Uamuzi wa shauri la Ukiukaji wa Kanuni za Utangazaji dhidi ya Vituo vya Clouds Fm, East Africa Radio, Duma Tv, Global Tv, Sibuka Tv na Star Tv
IMG_9782.jpg

IMG_9783.jpg

IMG_9784.jpg

IMG_9785.jpg

IMG_9786.jpg
 
3: Kituo cha #EastAfricaRedio kimekutwa na hatia ya kurusha maudhui yenye kukashifu utendaji wa Serikali katika uteuzi wa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) na kupewa onyo kali pamoja na kutozwa faini ya Shilingi milioni 3.
Mteule huyo, kama ilivyo kwa mteuaji, ni marufuku kumuongelea vibaya, sifia tu!
 
Back
Top Bottom