Zero Hours
JF-Expert Member
- Apr 1, 2011
- 12,942
- 18,669
Je waliwaonya au ni kupiga fine tu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo ni mwana CCM hawez guswa hata akikata mauno uchi hadharaniWasafi Chama lao tupo kimya tunawachora tu huku tunakunywa pepsi bariiiiidi na kuskiliza Playlist ya Amaboko[emoji86][emoji23][emoji1787]
Mbona hotuba za JPM zina mambo mengi yasio faa kusemwa hadharaniMAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevitoza faini ya Sh milioni 30 vyombo vya habari sita, kwa kukiuka kanuni na maadili ya utangazaji ikiwamo redio ya Clouds FM kuzungumzia supu ya pweza kuimarisha tendo la ndoa katika muda ambao wasikilizaji wanaweza kuwa watoto.
Mbali ya Clouds FM, vyombo vingine vilivyoadhibiwa ni East Africa Radio, na televisheni za Star, Sibuka, na Global Tv na Duma Tv.
Akisoma uamuzi huo jana jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Joseph Mapunda alisema vyombo hivyo vilikiuka kanuni za mawasiliano kwa nyakati tofauti.
Mapunda alisema redio ya Clouds FM kupitia kipindi chake cha Jahazi, walihamasisha vitendo vya ngono, kwa kutumia supu ya pweza katika kuimarisha tendo la ndoa kwa muda ambao wasikilizaji wanaweza kuwa watoto.
Alisema baada ya kusikiliza utetezi wao, wanatozwa faini ya Sh milioni saba na kupewa onyo kali baada ya kuwatia hatiani kwa kosa hilo.
Katika shauri lingine, kituo cha Duma TV kimetozwa faini ya Sh milioni saba na kufungiwa kuchapisha maudhui kwa muda wa mwezi mmoja ili wajipange na kuzifahamu kanuni na kuzingatia weledi na maadili ya utangazaji.
Mapunda alisema Duma ilikutwa na hatia ya kukiuka kanuni kwa kuchapisha na kutangaza maudhui yenye lugha isiyo na staha na iliyo na udhalilishaji wa kijinsia kwa wanaume na wanawake.
Alisema redio ya East Africa imetozwa faini ya Sh milioni tatu na kupewa onyo kali kwa kukiuka kanuni hiyo, kwa kurusha maudhui ya kukashifu utendaji wa serikali kupitia uteuzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kutumia lugha ya kashfa dhidi ya utendaji wake.
Vilevile Global Tv imetozwa Sh milioni saba na kupewa onyo kali, baada ya kupatikana na hatia ya kuchapisha picha ya mnato na kutangaza maudhui yasiyokuwa na lugha ya staha na yenye kushabikia vitendo vya mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja.
Mapunda alisema maudhui hayo, yangeweza kuwaumiza na kuwakwaza waumini wa dhebebu la Anglikana na Watanzania kwa ujumla. Pia, alisema Sibuka Tv inatozwa faini ya Sh milioni tatu baada ya kupatikana na hatia ya kushabikia mauaji ya kutisha katika muda, ambao watoto wanaweza kuwa sehemu kubwa ya watazamaji.
Dah, hakuna hata warning kwao..Inama nipachike rungu, papasa kichwa nisafishe mtaro!
Kongole Wasafi.
HUYO MUANDAAJI WA KIPINDI AFIKISHWE MAHAKAMANI TAFADHALI SANA TUMEOMBA.redio ya Clouds FM kuzungumzia supu ya pweza kuimarisha tendo la ndoa
Bado TCRA wajiongeze, watupie jicho YouTube maana baadhi ya akaunti za waTanzania wanaolipa leseni za online TV kwa TCRA zilizopo chini ya uangalizi wa serikali ya sikivu ya Awamu 5 kulinda maadili huko mitandaoni wanakuwa na maudhui tata sana yanayoweza kutazamwa na watoto wadogo muda wote iwe asubuhi, mchana yaani 24/7
CCM Oyee! Maendeleo ktk Maadili Hayana Chama !
.
HUYO MUANDAAJI WA KIPINDI AFIKISHWE MAHAKAMANI TAFADHALI SANA TUMEOMBA.
PIA SERIKALI TUNAIOMBA IONGEZE VIWANGO VYA FAINI ILI IWE FUNDISHO KWA REDIO NYINGINE. TUNAZITAKA REDIO STATIONS ZOTE ZIFUATE MAADILI YA KITANZANIA NA SIO KIMAGHARIBI.
Mteule huyo, kama ilivyo kwa mteuaji, ni marufuku kumuongelea vibaya, sifia tu!3: Kituo cha #EastAfricaRedio kimekutwa na hatia ya kurusha maudhui yenye kukashifu utendaji wa Serikali katika uteuzi wa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) na kupewa onyo kali pamoja na kutozwa faini ya Shilingi milioni 3.