FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Hata bila ya kuchunguza kwa kina, ukitazama kijuujuu tu utaelewa kuwa vituo vya kulelea Yatima ni biashara ya kujipatia kipato wanaoendesha vituo hivyo.
Vituo vyote vya Yatima vina asilimia 1 au 0 ya yatima kweli. Vingi vimejaa watoto waliopatikana kwa njia haramu (watoto wa zinaa na uasherati).
Pia utakuta humo watoto wa familia masikini zilizorubuniwa kuwa watoto wao watalelewa vizuri na kupelekwa shule. Wapo na wale wa wazazi waliogombana au kutorokana wakamwachia ulezi mzazi mmoja, anaposhindwa kulea peke yake, njia ya mkato ni kumpeleka mtoto au watoto kwenye kituo cha "yatima".
Kwa kuwa vituo vya "yatima" biashara yao ni kujipatia kipato kupitia huruma za watu wanaopeleka misaada na sadaka zao huko, vituo hivyo havikatai mtoto wa aina yoyote vile, mradi wao watoto wawepo ili biashara yao ifane.
Wanaoendesha vituo hivyo, hawajali lolote kuhusu hao watoto, wapo tayari kuwauza wakati wowote kwa wale waliokosa bahati ya kuzaa au hata kwa watu wenye kuharibu watoto (paedophiles).
Jamii, hususan serikali inatakiwa ichunguze kwa kina vituo vya "tatima" vyote, haijalishi ni vya kidini au binafsi. Vyote havifai kabisa kuwepo.
Nashauri wabunge wapeleke muswada bungeni, kama inabidi hivi vituo viwepo basi vitungiwe sheria zitazokua na manufaa na zitazowalinda hao watoto.
Tujadili.