Faiza kwa %75 hivi mada yako ina makosa.
Lau ungekua umepitia maisha ya uyatima usingeongea hivi
Au ungepitia hio ulioitaja kuzaliwa nje ya hiyo hio uliotaja ndoa usinge andika hii mada.
Kwenye kituo wanaweza kuwepo watoto 100 lakini akawepo mmoja kati ya hao mia ambae atamshukuru Mungu kwa dhati kwaajili ya uwepo wa hiko kituo.
Katika jamii hakuna kitu kinacho fanyika moja kwa moja kikiwa perfect na hakuna kitu kinachofanyika moja kwa moja bila ya faida.
Umetoa hitimisho la kwamba bunge litumie sheria ya kuthibiti, au serikali ivifute!
Binafsi niliwahi kua kwenye moja wapo ya vituo hivyo kama mfanyakazi kwa miaka kama 5 hakuna hata siku moja niliona hata mtendaji wa kata amewahi kuja pale usipokuwa kipindi kile cha Corona kuhimiza kunawa mikono.
Sio kwa mba serikali hawajui uwepo wa hivi vituo, wanajua sana lakini havipo kwenye hesabu zao!
Ikitokea vikafungwa vyote kama ulivyo shauri hao walio yatima kweli hata kama mmoja umewahi kufikiria hatma yake?
Mimi binafsi nimezaliwa nikajikuta yatima chini ya mwaka mmoja wazazi wangu wote walikufa, maisha nilioishi kipindi hiko yalikua magumu sana sana, nilitamani wakati fulani hata aheri nisingezaliwa! Sikua na furaha wala amani wala tumaini, upweke niliokua nao mpaka ninapoandika hapa umeniathiri na matokeo yake nayaona leo.
Sasa kama ningebahatika kupata kuwepo kwenye kituo cha yatima unadhani nisinge mshukuru Mungu badala ya kulaumu na kukata tamaa, ingawa hata sasa namshukuru sana Mungu.
Ukweli ndugu
FaizaFoxy pamoja na makosa ya hao wasimamizi wa hivi vituo lakini uwepo wao ni wa muhimu zaidi huo uliiita ni biashara ya utumwa.