Viungo vya binadamu vinavyokatwa kwa sababu mbalimbali hupelekwa wapi?

Viungo vya binadamu vinavyokatwa kwa sababu mbalimbali hupelekwa wapi?

Elsa Marie

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2017
Posts
2,284
Reaction score
5,596
Leo nilikuwa hospitali moja kwaajili ya matibabu. Nikamuona mzee mmoja kwenye wheelchair, ana mguu mmoja mwingine umekatwa kuanzia kwenye goti.

Hii ikapelekea nijiulize hivi viungo vinavyokatwa kwasababu ya magonjwa kama kisukari na mengine huwa vinapelekwa wapi.
Ni mgonjwa anapewa kiungo chake au hospitali wanaviteketeza?

Na kama mgonjwa anapewa kiungo chake, ni utaratibu gani anafanya? Kukiteketeza ama kukizika kwa heshima?

Mshana Jr
Msanii
makaveli10
 
Nadhani upo sahihi. Vitakuwa vinateketezwa maana havifai tena kwa matumizi mfano viun vingine kama figo na maini.

Mleta mada naona ingekuwa yeye angesema mguu wake uzikwe kwa heshima😀🤦🏾‍♂️
🤣🤣🤣
 
Vinaweza kuteketezwa na kifaa maalumu ( incinerator).

IMG-20241010-WA0014.jpg

Pia vinaweza chukuliwa kwa tafiti za kisayansi na kimaabara kwa kibali kutoka kwa familia au kwa mgonjwa.
 
Hapa tuite madaktari, kwa haraka haraka nahisi kwanza wanavitumia kujifunzia, ni kama vile maiti zinazokosa ndugu na nyinginezo, wanaosomea udaktari huwa wanafanyia mafunzo yao.
 
Nadhani upo sahihi. Vitakuwa vinateketezwa maana havifai tena kwa matumizi kama viungo vingine, mfano figo na maini.

Mleta mada naona ingekuwa yeye angesema mguu wake uzikwe kwa heshima😀🤦🏾‍♂️
Nijenge kakaburi kadogo kwaajili ya mguu wangu
 
Hapa tuite madaktari, kwa haraka haraka nahisi kwanza wanavitumia kujifunzia, ni kama vile maiti zinazokosa ndugu na nyinginezo, wanaosomea udaktari huwa wanafanyia mafunzo yao.
Hiyo ni sawa lakini vipi kama nitataka kuondoka na mguu wangu naruhusiwa?
 
Leo nilikuwa hospitali moja kwaajili ya matibabu. Nikamuona mzee mmoja kwenye wheelchair, ana mguu mmoja mwingine umekatwa kuanzia kwenye goti.

Hii ikapelekea nijiulize hivi viungo vinavyokatwa kwasababu ya magonjwa kama kisukari na mengine huwa vinapelekwa wapi.
Ni mgonjwa anapewa kiungo chake au hospitali wanaviteketeza?

Na kama mgonjwa anapewa kiungo chake, ni utaratibu gani anafanya? Kukiteketeza ama kukizika kwa heshima?

Mshana Jr
Msanii
makaveli10
Kwa ethics za utabibu. Kiungo kinachokuwa kinaondolewa kwa nia ya amputation kutoka kwa mgonjwa ni lazima mhusika atoe kauli nini kifanyiwe. Kwa mfano wapo wanaoondoka na viungo vyao kwa minajili ya taratibu za kuvizika ardhini, wapo wanaoomba facility wavidispose na hapo kama hakuna uangalizi ndipo wazee wa nguvu za giza wanapaotea sana hapo ili kuvinunua kwa malengo yao, lakini pia facility wanaweza kurequest utafiti zaidi kwenye kiungo kilichoondolewa ili kubaini historia na ukubwa wa maradhi husika
 
Kwa ethics za utabibu. Kiungo kinachokuwa kinaondolewa kwa nia ya amputation kutoka kwa mgonjwa ni lazima mhusika atoe kauli nini kifanyiwe. Kwa mfano wapo wanaoondoka na viungo vyao kwa minajili ya taratibu za kuvizika ardhini, wapo wanaoomba facility wavidispose na hapo kama hakuna uangalizi ndipo wazee wa nguvu za giza wanapaotea sana hapo ili kuvinunua kwa malengo yao, lakini pia facility wanaweza kurequest utafiti zaidi kwenye kiungo kilichoondolewa ili kubaini
Kama kuna option zote hizo basi imekaa vizuri. Thanks.
 
YANI UZIKE KWA HESHIMA KIGANJA CHAKO ULICHOKATWA HUU NI MCHEZO SASA
Inawezekana mila za watu wengine zipo hivyo. Inaweza isiwe kama ambavyo inakuwa kwenye msiba lakini kukihifadhi ardhini wewe mwenyewe kwa jinsi unavyopendelea, au hata kukichoma moto.
 
Back
Top Bottom