Viungo vyangu mwenyewe katika mwili wangu lakini vinagoma kunipa ushirikiano

Viungo vyangu mwenyewe katika mwili wangu lakini vinagoma kunipa ushirikiano

Kalaga Baho Nongwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2020
Posts
9,953
Reaction score
23,150
Wakuu si kwema kabisa
Kazi za site za ujenzi wa wachina zinafanana na mauaji. Kupandisha na kiroba cha saruji floor ya 4 huku subuhi umekula maandazi mawili na chai ya mia sio poa

Nimeingia site nikajiona shujaa wa maisha hali niliyokutana nayo ndugu zangu sio poa kabisa. Wiki hii yote mpaka appetite ya kula imekata kabisa. Imenihangaisha kwelikweli leo nimeamka akili inataka mkono minute lakini mkono kuinuka hautaki.

Jana jioni nimetoka site nilikuwa natembea najiona kama niko juu ya baskeli. Sio vidole wala miguu haitoi ushirikiano kabisa. Kazi za site wazee zisikie tu. Inafikia kipindi hata viungonvya mwili unavikagua kama vipo mana kila ukitaka vikusaidia kufanya mjongeo havitokei kushirikiana na wazo lako

Kalaga baho
20241202_070951.jpg
 
Kazi za site ngum sana na mshahar mdogo, imagine kwa siku mnachanganya udongo wa mifuko ya saruji 20 watu watatu
Nachofurahia ni kuwa unajituma Kaka .
Sema nini hapo viungo vinamaanisha usimuamini mtu yeyote Wala kitu chochote maana wasaliti ni wengi hapa duniani.
 
Wakuu si kwema kabisa
Kazi za site za ujenzi wa wachina zinafanana na mauaji. Kupandisha na kiroba cha saruji floor ya 4 huku subuhi umekula maandazi mawili na chai ya mia sio poa

Nimeingia site nikajiona shujaa wa maisha hali niliyokutana nayo ndugu zangu sio poa kabisa. Wiki hii yote mpaka appetite ya kula imekata kabisa. Imenihangaisha kwelikweli leo nimeamka akili inataka mkono minute lakini mkono kuinuka hautaki.

Jana jioni nimetoka site nilikuwa natembea najiona kama niko juu ya baskeli. Sio vidole wala miguu haitoi ushirikiano kabisa. Kazi za site wazee zisikie tu. Inafikia kipindi hata viungonvya mwili unavikagua kama vipo mana kila ukitaka vikusaidia kufanya mjongeo havitokei kushirikiana na wazo lako

Kalaga baho
View attachment 3170405
Pole mkuu. Mapambano makali sana..utayavuka salamaa
 
Hahahaaa..unanikumbusha mbali sana mzee..Enzi hizo nimetoka kumaliza form six nikasema ngoja nitafute kibarua kuliko kukaa home kibwege..nikaenda zangu sabasaba maonesho msimu ulikuwa unakaribia kwa hiyo walikuwa wanakarabati majengo..kuna jengo moja lilikuwa linatakiwa kuchimbuliwa floor ya zege.Hapo ndio nilipata kazi ..upana wake au kimo cha hiyo zege ni kama nusu mita (Means kutoka juu kwenda chini).Alooh nilipiga sururu kama ishirini hivi nikaona viganja vinachanika..nikawaachia kazi yao nikasepa..kesho kuamka viganja vimeota malenge lenge hahahaa.
 
Back
Top Bottom