Hahahaaa..unanikumbusha mbali sana mzee..Enzi hizo nimetoka kumaliza form six nikasema ngoja nitafute kibarua kuliko kukaa home kibwege..nikaenda zangu sabasaba maonesho msimu ulikuwa unakaribia kwa hiyo walikuwa wanakarabati majengo..kuna jengo moja lilikuwa linatakiwa kuchimbuliwa floor ya zege.Hapo ndio nilipata kazi ..upana wake au kimo cha hiyo zege ni kama nusu mita (Means kutoka juu kwenda chini).Alooh nilipiga sururu kama ishirini hivi nikaona viganja vinachanika..nikawaachia kazi yao nikasepa..kesho kuamka viganja vimeota malenge lenge hahahaa.