Vivienne sio Mtanzania: tuwe na tabia ya kuheshimu mipaka ya Utaifa na Jitihada za wengine

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Kumekuwa na wimbi jipya katika mitandao ya kijamii wiki hii, likimhusisha binti mahiri wa soka, Vivienne Theresa Upendo Lia, ambaye baadhi ya Watanzania wameanza kudai ni “Mtanzania” kwa sababu tu jina lake lina sauti ya Kiafrika ama kibantu. Lakini ukweli ni tofauti kabisa. Vivienne ni Mwingereza halisi, mzaliwa na mkazi wa Uingereza, anayeichezea timu ya taifa ya wanawake ya Uingereza U19, baada ya kung’ara pia katika kikosi cha Uingereza U17 kati ya mwaka 2022 na 2023.
images (68).jpeg

Hata hivyo, taarifa hizi potofu zinaendelea kuibua mjadala mpana kuhusu utamaduni wa watanzania “kudai” mafanikio ya watu wengine wenye asili ya mbali tu na nchi yetu. Hii tabia, kwa hakika, inaonyesha namna tunavyohangaika kutafuta fahari ya kitaifa bila kuwekeza vya kutosha katika kukuza vipaji vyetu wenyewe.
images (69).jpeg

Binti Vivienne amelelewa, kusomeshwa, kufundishwa na kulelewa na mfumo wa soka wa Uingereza sio Tanzania, amepata kulelewa na Shirikisho la FA sio TFF. Kila hatua aliyopiga ni matokeo ya juhudi na uwekezaji wa taifa la Uingereza na sio Tanzania.
images (67).jpeg

Ni kweli, jina lake linaweza kuwa na asili fulani ya Kiafrika, labda kupitia mababu zake, lakini hilo halitoshi kumfanya kuwa Mtanzania. Utaifa ni zaidi ya jina; ni malezi, ni uzalendo, ni mahali mtu alikulia na anapolipigania taifa lake. Vivienne mwenyewe ni mwanamke ambaye anachipukia kutoka ndani ya soka la wanawake la Uingereza, anayejivunia kuwakilisha bendera yake ya Uingereza – na anayo haki ya kufanya hivyo.
images (66).jpeg

Badala ya kutumia muda kudai na kulazimisha utambulisho wa Vivienne, tunapaswa kuulizana maswali yafuatayo: tunawekeza vipi katika Vivienne wetu hapa nyumbani? Wakina Vivienne waliopo JKT Queens pamoja na timu za wadada za Simba na Yanga.
images (65).jpeg

Kuna wadada wengi wenye vipaji vya soka, muziki na sanaa, lakini wanakosa fursa, vifaa, au motisha. Kama tungewekeza nguvu hizo tunazotumia kushangilia mafanikio ya wengine, labda tungekuwa tunasikia majina ya “Vivienne wa Kitanzania” yakitikisa dunia.
images (68).jpeg

Vivienne ni mfano wa mafanikio kupitia mfumo thabiti wa malezi ya vipaji. Tumuachie abaki na Uingereza wake acheze mpira wake na apate mafanikio yake, na sisi tujifunze namna ya kujenga mazingira yatakayowawezesha watoto wetu kufikia kiwango kama chake – kwa jina, kwa bendera, na kwa fahari ya kweli ya Tanzania.
 
Watu wameshasahu kuwa hatuna Dual Citizenship 😃 Hii British-Tanzanian sijui kaitolea wapi?
Screenshot_20251014_225130_X.jpg
 
Hayo maneno ya watanzania wakisema hvy yako wapi?
Au watu wawili watatu wakisema hvy ndo watanzania wote wamesema hvy?
Nimeattach picha pia ukienda Instagram kuna raia zinasambaza hii habari
 
Kumekuwa na wimbi jipya katika mitandao ya kijamii wiki hii, likimhusisha binti mahiri wa soka, Vivienne Theresa Upendo Lia, ambaye baadhi ya Watanzania wameanza kudai ni “Mtanzania” kwa sababu tu jina lake lina sauti ya Kiafrika ama kibantu. Lakini ukweli ni tofauti kabisa. Vivienne ni Mwingereza halisi, mzaliwa na mkazi wa Uingereza, anayeichezea timu ya taifa ya wanawake ya Uingereza U19, baada ya kung’ara pia katika kikosi cha Uingereza U17 kati ya mwaka 2022 na 2023.
View attachment 3488747
Hata hivyo, taarifa hizi potofu zinaendelea kuibua mjadala mpana kuhusu utamaduni wa watanzania “kudai” mafanikio ya watu wengine wenye asili ya mbali tu na nchi yetu. Hii tabia, kwa hakika, inaonyesha namna tunavyohangaika kutafuta fahari ya kitaifa bila kuwekeza vya kutosha katika kukuza vipaji vyetu wenyewe.
View attachment 3488748
Binti Vivienne amelelewa, kusomeshwa, kufundishwa na kulelewa na mfumo wa soka wa Uingereza sio Tanzania, amepata kulelewa na Shirikisho la FA sio TFF. Kila hatua aliyopiga ni matokeo ya juhudi na uwekezaji wa taifa la Uingereza na sio Tanzania.
View attachment 3488749
Ni kweli, jina lake linaweza kuwa na asili fulani ya Kiafrika, labda kupitia mababu zake, lakini hilo halitoshi kumfanya kuwa Mtanzania. Utaifa ni zaidi ya jina; ni malezi, ni uzalendo, ni mahali mtu alikulia na anapolipigania taifa lake. Vivienne mwenyewe ni mwanamke ambaye anachipukia kutoka ndani ya soka la wanawake la Uingereza, anayejivunia kuwakilisha bendera yake ya Uingereza – na anayo haki ya kufanya hivyo.
View attachment 3488750
Badala ya kutumia muda kudai na kulazimisha utambulisho wa Vivienne, tunapaswa kuulizana maswali yafuatayo: tunawekeza vipi katika Vivienne wetu hapa nyumbani? Wakina Vivienne waliopo JKT Queens pamoja na timu za wadada za Simba na Yanga.
View attachment 3488751
Kuna wadada wengi wenye vipaji vya soka, muziki na sanaa, lakini wanakosa fursa, vifaa, au motisha. Kama tungewekeza nguvu hizo tunazotumia kushangilia mafanikio ya wengine, labda tungekuwa tunasikia majina ya “Vivienne wa Kitanzania” yakitikisa dunia.
View attachment 3488747
Vivienne ni mfano wa mafanikio kupitia mfumo thabiti wa malezi ya vipaji. Tumuachie abaki na Uingereza wake acheze mpira wake na apate mafanikio yake, na sisi tujifunze namna ya kujenga mazingira yatakayowawezesha watoto wetu kufikia kiwango kama chake – kwa jina, kwa bendera, na kwa fahari ya kweli ya Tanzania.
Ni sawa lakni je ana mpenzi? maana unaonekana unamjua vilivyokuliko hata wazazi wake
 
Huyu mtoto ni kweli siyo Mtanzania kwa sababu amezaliwa Uingereza. Ila mzazi wake (na hasa mama yake mzazi maana nilimshuhudia kupitia luninga alipokuwa anahojiwa) ni Mtanzania anayeishi Uingereza. Kwa upande wa baba yake, sina uhakika kama na yeye ni Mbongo.

Na hata siku hiyo mama yake alipokuwa anahojiwa, dogo alikuwa hajui chochote kuhusu Kiswahili. Kimsingi hana tofauti na yule Malaika Mihambo wa Ujerumani, au Yusuph Poulsen. Wote hawa wana asili ya Tanzania.
 
Umeongea point mkuu! Dogo hajui chochote kuhusu bongo
 
Back
Top Bottom