Vivienne sio Mtanzania: tuwe na tabia ya kuheshimu mipaka ya Utaifa na Jitihada za wengine

Vivienne sio Mtanzania: tuwe na tabia ya kuheshimu mipaka ya Utaifa na Jitihada za wengine

Wamesema Nationality: British-Tanzanian hawakusema Citizenship: British-Tanzanian

Kiujumla Nationality hutumika kuonyesha sehemu ya makazi. Mtu anaweza kuwa siyo mtanzania lakini ana makazi Tanzania
Nationality = Who you are (by origin or birth).

Citizenship = What you can do legally (by law and rights in a given country
 
Wamesema Nationality: British-Tanzanian hawakusema Citizenship: British-Tanzanian

Kiujumla Nationality hutumika kuonyesha sehemu ya makazi. Mtu anaweza kuwa siyo mtanzania lakini ana makazi Tanzania
Not exactly! Fanya homework kidogo.
 
Kumekuwa na wimbi jipya katika mitandao ya kijamii wiki hii, likimhusisha binti mahiri wa soka, Vivienne Theresa Upendo Lia, ambaye baadhi ya Watanzania wameanza kudai ni “Mtanzania” kwa sababu tu jina lake lina sauti ya Kiafrika ama kibantu. Lakini ukweli ni tofauti kabisa. Vivienne ni Mwingereza halisi, mzaliwa na mkazi wa Uingereza, anayeichezea timu ya taifa ya wanawake ya Uingereza U19, baada ya kung’ara pia katika kikosi cha Uingereza U17 kati ya mwaka 2022 na 2023.
View attachment 3488747
Hata hivyo, taarifa hizi potofu zinaendelea kuibua mjadala mpana kuhusu utamaduni wa watanzania “kudai” mafanikio ya watu wengine wenye asili ya mbali tu na nchi yetu. Hii tabia, kwa hakika, inaonyesha namna tunavyohangaika kutafuta fahari ya kitaifa bila kuwekeza vya kutosha katika kukuza vipaji vyetu wenyewe.
View attachment 3488748
Binti Vivienne amelelewa, kusomeshwa, kufundishwa na kulelewa na mfumo wa soka wa Uingereza sio Tanzania, amepata kulelewa na Shirikisho la FA sio TFF. Kila hatua aliyopiga ni matokeo ya juhudi na uwekezaji wa taifa la Uingereza na sio Tanzania.
View attachment 3488749
Ni kweli, jina lake linaweza kuwa na asili fulani ya Kiafrika, labda kupitia mababu zake, lakini hilo halitoshi kumfanya kuwa Mtanzania. Utaifa ni zaidi ya jina; ni malezi, ni uzalendo, ni mahali mtu alikulia na anapolipigania taifa lake. Vivienne mwenyewe ni mwanamke ambaye anachipukia kutoka ndani ya soka la wanawake la Uingereza, anayejivunia kuwakilisha bendera yake ya Uingereza – na anayo haki ya kufanya hivyo.
View attachment 3488750
Badala ya kutumia muda kudai na kulazimisha utambulisho wa Vivienne, tunapaswa kuulizana maswali yafuatayo: tunawekeza vipi katika Vivienne wetu hapa nyumbani? Wakina Vivienne waliopo JKT Queens pamoja na timu za wadada za Simba na Yanga.
View attachment 3488751
Kuna wadada wengi wenye vipaji vya soka, muziki na sanaa, lakini wanakosa fursa, vifaa, au motisha. Kama tungewekeza nguvu hizo tunazotumia kushangilia mafanikio ya wengine, labda tungekuwa tunasikia majina ya “Vivienne wa Kitanzania” yakitikisa dunia.
View attachment 3488747
Vivienne ni mfano wa mafanikio kupitia mfumo thabiti wa malezi ya vipaji. Tumuachie abaki na Uingereza wake acheze mpira wake na apate mafanikio yake, na sisi tujifunze namna ya kujenga mazingira yatakayowawezesha watoto wetu kufikia kiwango kama chake – kwa jina, kwa bendera, na kwa fahari ya kweli ya Tanzania.
Mbona me simjui wala hiyo habari sijaisikia, Acheni kukuza mambo ya kijinga kuweni serious na hali ya sasa
 
Wabongo sijui ni ushamba ama kujipendekeza, kipindi yeye na familia yake wanajitafuta mpo kimya, sasa kawa star kajipata watu wanalazimisha ni Mtanzania.
 
Angekuwa amefanya jambo BAYA am sure wa bongo wasingeshupaia kuwa ni mbongo
 
Acha ushamba,hao watoto tunao wamezaliwa huko na baba zao ni sisi.
Na wako sana huko kwenye sport ,hamna anaelalamika kwanini katajwa asili yake Tz.
Utakua muhaya wewe,
Hata azaliwe wapi kwanza hata yeye anajitambulisha Brit🇬🇧-Tz org🇹🇿.
We unatupigia makelele hapa
 
Mtu anatuandikia makala ndefu kuhusu mtu ambaye hata hatumfahamu au hii ni ID ya Mwashambwa
Ukielewa ulichokiandika ndipo utaelewa kwanini Mwashambwa ana wake wengi humu ndani
 
Acha ushamba,hao watoto tunao wamezaliwa huko na baba zao ni sisi.
Na wako sana huko kwenye sport ,hamna anaelalamika kwanini katajwa asili yake Tz.
Utakua muhaya wewe,
Hata azaliwe wapi kwanza hata yeye anajitambulisha Brit🇬🇧-Tz org🇹🇿.
We unatupigia makelele hapa
Sawa Baba Vivienne
 
Wazee, huku Afrika unaonekana ni shithole kweli kama alivyosema Trump kipindi kile, kwanini kila mtu anapakataa? Mayweather,Lukaku na mdogo wake Romeo (hawataki hata baba yao azikwe Congo) na sasa huyu Viviane. 🤔

Tuondokeni mapema huku Africa kabla hatujachelewa. Ila na iwe bloody fucken kwa kila anayekataa asili yake
 
Umeongea point mkuu! Dogo hajui chochote kuhusu bongo
Ata kama hajui chochote lakini haiondoi Utanzania wake.Hii sawa na Makabila yetu,kuna watoto waitwa ni wasukuma na wamezaliwa dar,hawajawai kufika usukumana na hawajui chochote cha uko lakini baado ni wasukuma tu
 
Watanzania wengi ni wajinga sana, na kibaya zaidi hata kufanya research ndogo tu kabla ya kuropoka hawawezi.

Kuna mijinga mingi mitaani mpaka leo inaamini Rashford ni mpemba!
 
Wazee, huku Afrika unaonekana ni shithole kweli kama alivyosema Trump kipindi kile, kwanini kila mtu anapakataa? Mayweather,Lukaku na mdogo wake Romeo (hawataki hata baba yao azikwe Congo) na sasa huyu Viviane. 🤔

Tuondokeni mapema huku Africa kabla hatujachelewa. Ila na iwe bloody fucken kwa kila anayekataa asili yake

Mkataa kwao ni Mtumwa, Hao majamaa woteni wapuuzi tu
 
Ata kama hajui chochote lakini haiondoi Utanzania wake.Hii sawa na Makabila yetu,kuna watoto waitwa ni wasukuma na wamezaliwa dar,hawajawai kufika usukumana na hawajui chochote cha uko lakini baado ni wasukuma tu
Sawa basi Vivienne ni Mtanzania halisi. Na yote haya ambayo anafanya ji jitihada za Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan
 
Back
Top Bottom