Vivutio vya utalii Tanzania na faida za utalii wa ndani

Joined
Aug 15, 2011
Posts
30
Reaction score
11
Tanzania imeweka rekodi ya aina yake baada ya vivutio yake vyote vitatu vilivyoingia katika shindano la kutafuta Maajabu Saba ya Asili Barani Afrika kushinda na kuingia katika orodha ya Maajabu Saba ya Asili Barani Afrika.

Aidha hifadhi ya Taifa ya Serengeti kimetajwa kuwa ni kivutio pekee kilichopigiwa kura nyingi zaidi miongoni mwa vivutio vyote vya Afrika vilivyoshindanishwa katika shindano hilo.

Akitangaza vivutio vilivyoshinda na kuingia katika orodha ya Maajabu mapya Saba ya Afrika katika sherehe zilizofanyika katika Hotel ya Mt. Meru jijini Arusha na kuhudhuriwa na watu mbali mbali mashuhuri kutoka ndani na nje ya nchini wakiwemo wabunge, mabalozi na mawaziri, Rais wa taasisi ya Kimataifa ya Seven Natural Wonders yenye makao yake nchini Marekani Dr. Phillip Imler amesema ushindi wa Tanzania ni wa kishindo na imeweka rekodi ya aina yake kwa vivutio vyake vyote kuingia katika orodha hiyo ya Maajabu Saba ya Asili ya Afrika.

Dr. Imler amevitaja vivutio vingine vilivyo shinda kuwa ni pamoja Red sea reef kutoka Misri, Mto Nile wa Uganda, Delta ya Okava ngo ya Bostwana na Jangwa la Sahara lililoko kaskazini mwa Afrika
Kwa upande wake mgeni rasmi katika sherehe hizo za Utangazaji wa maajabu hayo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.

Mizengo Pinda amesema vivutio vya Tanzania vilistahili kushinda kwani pamoja na upekee wa vivutio hivyo lakini ni ukweli usiopingika kuwa Tanzania inafanya vizuri sana katika kuhakikisha utalii unakuwa endelevu kwa kuhifadhi mazingira yanayozunguka maliasili zake zake na ndiyo maana ripoti ya Word Economic Forum inaonesha kuwa Tanzania ni nchi ya pili duniani baada ya Brazil kwa uhifadhi wa mazingira asilia, maeneo mengi ya asili ambayo ni urithi wa dunia na maeneo mengi yanayohifadhiwa ambapo takribani asilimia 28 ya ardhi ya Tanzania ni eneo linalohifadhiwa.

Mchakato wakutafuta vivutio Saba vya Bara la Afrika ulianza mwaka 2008 kwa kuhusisha vivutio kumi na mbili (12) ambapo watu mbalimbali kote duniani walipiga kura sambamba na kura za wataalaamu UNESCO na wa Taasisi ya Kimataifa ya Uhidhafi wa Mazingira ya IUCN.

=======
Vivutio vya Tanzania ni vingi sana, kama vile milima (kwa mfano mlima Kilimanjaro, milima ya Usambara, milima ya Udzungwa), pia mbuga za wanyama (kama Mikumi, Serengeti, Ngorongoro na Manyara), tena maporomoko ya maji ya mto Ruaha na mengineyo.

Faida za kutembelea vivutio vya ndani
Je, mara yako ya mwisho kusafiri sehemu ngeni ilikuwa lini? Uliposafiri, huenda ulihisi kwamba ulihitaji kupumzika na kusahau taabu za kila siku? Je, umewahi kwenda likizo katika maeneo yoyote ya vivutio? Fikiria karne moja hivi iliyopita, watu wengi duniani hawakuwa wakipata nafasi ya kusafiri au kwenda mapumziko kama ilivyo sasa.

Walikaa karibu na kwao maisha yao yote bila kutembelea maeneo ya mbali. Kusafiri nchi za mbali kwa namna yoyote ile ikiwemo kupumzisha akili au kujielimisha lilikuwa jambo gumu na ni watu wachache tu, hasa matajiri au wafanyabiashara waliopenda kusafiri ndio waliweza kufanya hivyo. Lakini siku hizi mambo yamerahisishwa zaidi, mamia kwa maelfu ya watu wanasafiri kokote wanakotaka katika nchi yao au hata nchi nyingine, hasa kwa safari za kitalii.

Ripoti moja ya Shirika la Utalii Ulimwenguni inasema hivi: ‘Utalii huingiza fedha nyingi za kigeni ambazo ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi nyingi.” Inasema: “Mwaka 1996, utalii wa kimataifa ulichuma fedha za kigeni zenye thamani ya Dola bilioni 423 za Marekani. Mapato hayo yalikuwa zaidi ya yale yaliyochumwa kwa kuuza mafuta, magari, vyombo vya mawasiliano, nguo, na kadhalika, katika nchi nyingine.”

Ripoti inaenda mbali na kusema:: “Utalii ndiyo biashara inayostawi zaidi ulimwenguni,” na ilitokeza ‘asilimia 10 ya jumla ya pato la nchi zote ulimwenguni.’ Nadhani kila mmoja atakubaliana nami kuwa kutembelea maeneo ya vivutio kuna faida kubwa, japokuwa suala la kutembelea maeneo mbalimbali ya vivutio halijazoeleka sana kwa Watanzania na Waafrika kama ilivyo kwa Wazungu.

Kusafiri siyo lazima kwenda nchi nyingine, bali hata safari za ndani ya nchi au ndani ya eneo lako unaloishi zina maana kubwa, hasa kama zitafanywa kwa lengo la kujifunza. Unapofunga safari ya kutembelea vivutio na maajabu ni njia nzuri ya kuona fursa zilizoko kwenye eneo fulani unazoweza kuzifanyia kazi na ukajipatia kipato au ukaongeza kipato chako. Utalii una faida kubwa na hufaidisha pande zote. Wewe kama mtalii, unapotembelea vivutio au maajabu nchini kwako au hata katika nchi ya kigeni, utaburudika sana na kuelimika.

Tanzania tunayo maeneo muhimu kwa utalii kama: hifadhi za taifa, mapori ya akiba, fukwe za bahari, maeneo ya kihistoria, milima, maziwa n.k. Unaposafiri unajifunza mambo mbalimbali ambayo isingekuwa rahisi kujifunza ukiwa nyumbani. Utajifunza jiografia, utamaduni au hata mtindo wa maisha wa watu wa eneo unalotembelea.

Si ushamba kutembelea maeneo ya vivutio katika nchi yako na kujifunza huko, kwani inasemwa kuwa kutembea umbali wa maili moja ni bora kuliko kukaa sehemu moja bila jambo muhimu hivyo, kutembla maeneo mbalimbali ni shule nzuri ya kuongeza maarifa. Ifahamike wazi zaidi kuwa, nchi zinazowahudumia watalii hujipatia fedha nyingi za kigeni, kwa kuwa nchi yoyote huhitaji fedha za kigeni ili kulipia huduma na bidhaa zinazotoka katika nchi nyingine. Kwa hiyo, unaposafiri unaweza kuboresha maisha ya watu wengine wa eneo ulilotembelea kwa njia moja au nyingine.

Fikiria vyombo vya usafiri unavyotumia safarini, hoteli utakazolala, viingilio utakavyolipa na kadhalika. Hivi vyote vinawapa kipato watu wengine na kuboresha maisha yao, hivyo, safari yako haikunufaishi wewe peke yako, bali hata watu wengine wanaohusika au kuhusishwa kwenye safari yako. Unaposafiri pia unapata marafiki mbalimbali watanaotokana na watu uliokutana nao safarini. Wapo baadhi ya watu waliowahi kupata wenza wa maisha kutokana na kusafiri; hivyo faida hii ya kusafiri haiwezi kuachwa nyuma.

Karibu kundi kubwa la watu, pengine nawe ni mmoja wao, wamewahi kusafiri kutoka eneo moja kwenda eneo lingine kwa malengo tofauti tofauti likiwamo la kuburudika, hata hivyo, moja ya safari nzuri katika safari hizo ni yenye kusudi la utalii. Utalii ni jambo linalopaswa kupendwa na kila mtu anayethamini uumbaji wa Mungu, kwa kuwa ni Mungu aliyewawekea wanadamu mazingira ya kuvutia na kustaajabisha ili tuweze kujifunza kupitia uumbaji wake.

Tanzania ni moja ya nchi zilizobarikiwa kuwa na maeneo ya kipekee katika nchi nyingi zenye utajiri wa maeneo ya vivutio, wanyamapori, milima, maziwa na hata historia katika makumbusho. Vivutio hivi ni utajiri mkubwa wa kujivunia na kila Mtanzania anapaswa kuiona thamani ya kuujali kwa kutembelea maeneo haya kujifunza na pia kuburudika.

Haipendezi kuona watu kutoka nchi za ughaibuni wakija kutalii maeneo haya ambayo sisi tumekuwa tukiyatazama tu pasipo kupata muda wa kwenda kujifunza huko. Yapo maneno ya asili na yenye kuvutia sana ambayo kama hujawahi kutembelea ni vyema ukajitahidi kutafuta nafasi ili kutembelea japo eneo moja au mawili, kwani utajifunza mengi s ikiwa ni pamoja na kupanua wigo wa kufikiri. Maeneo hayo ni pamoja na Msitu wa Nyumbanitu wenye kuku wa ajabu mkoani Njombe, Bwawa la Mto Nyange lenye viboko wanaocheka na mapango ya Kipatimo wilayani Kilwa, Hifadhi ya Gombe yenye sokwe wanaoishi kama binadamu mkoani Kigoma, eneo la Snake Park huko Monduli- Arusha, na Bonde la Ngorongoro ambalo ndiyo kitovu cha binadamu.

Maeneo mengine ni Maporomoko ya Maji ya Mto Ruaha, Mapango ya Amboni mkoani Tanga, eneo la Kondoa Irangi mkoani Dodoma, shimo la ajabu lijulikanalo kama Shimo la Mungu wilayani Newala, mchanga unaohama bila upepo huko Ngorongoro. Pia tunayo milima kama Kilimanjaro, Milima ya Usambara, Uluguru, Udzungwa, Oldonyo Lengai n.k. mbuga za wanyama kama Mikumi, Serengeti, Ngorongoro, Manyara, Selous, Katavi, na maeneo yenye historia kama Kilwa Kisiwani, Bagamoyo, Zanzibar na kadhalika.

Utajiri huu wa uwepo wa vivutio hivi na vingine vingi licha ya kuiingizia nchi mapato makubwa, pia ni maeneo yenye fursa kubwa na yanayofaa kutunzwa kwa ajili ya vizazi vya sasa na vinavyokuja. Haya yanapaswa kutunzwa na kutumiwa ipasavyo kwa kutembelewa ili neema iliyo ndani ya urithi huu, iwanufaishe watanzania hasa kwa kupanua uelewa wao wa mambo na kuburudika. Haya, yanapaswa kutunzwa kwa kutunza na kutoharibu mazingira na ma;liasili zake. Hivyo, kusafiri na kwenda kujionea vivutio mbalimbali ndani ya nchi ni burudani ya aina yake, hasa kama unasafiri kwenda kwenye eneo sahihi.

Unaposafiri hutaacha kujifunza, kupata burudani bora na ya kipekee na faida nyingine lukuki. Uwapo safarini unaweza kuona vitu vya kuvutia kama vile mazingira ya asili (mito, milima, mabonde, n.k.), wanyama pamoja na sanaa za eneo husika kama vile ngoma, maigizo, mavazi ya kitamaduni na kadhalika.

Ni ukweli usiopingika kuwa, Wazungu wanafahamu vyema umuhimu wa safari za kitalii, ndiyo maana wako tayari kulipa gharama kubwa ili watimize lengo hilo. Kimsingi, kutembelea vivutio humfanya mtu kuburudika na kufurahi, na tunapofurahi tutakuwa tumejiongezea siku za kuishi huku tukichochea utunzaji na ukuaji wa uchumi wa nchi.


Mlilima Kilimanjaro

Milima ya Usambara

Milima ya Udzungwa

Mbuga za wanyama

Pia unaweza soma vivutio zaidi hapa
Uzi wa Matembezi (Travel & Vacations) na Vivutio vya Utalii nchini Tanzania

Michango ya wadau
----
----
 

Attachments

  • Photo 1.jpg
    45.5 KB · Views: 710
  • photo 2.jpg
    53.8 KB · Views: 726
  • 1584085093864.png
    20.6 KB · Views: 10
  • 1584085110067.png
    20.6 KB · Views: 15
Tungeweza kupata hata vitano kutoka kwetu laiti kama tungetaka. yani hapo ndio tumeamua kidogo tumeingiza vitatu tungeamua sana? Tutafakari tuchukue hatua.
 
Vivutio vingine kwa Tanzania nje ya Mbuga ya Serengeti mbona hujavitaja mkuu?
 
Bila shaka Ngorongoro na mlima Kilimanjaro ndivyo vingine - ninahisi tu.
 
Suala ni moja tu,vinatusaidia vipi katika kukuza uchumi wa nchi yetu?????

Good point Mkuu! Hilo ndio suala la msingi. Inabidi serikali ielewe kwamba sasa inabidi kutumia hela ili kuingiza hela. Lazima watoe promotion na advertising kabambe kupita vyombo vya habari vya kimataifa kama CNN, Al Jazira, BBC na Sky News, na magazeti ya kimataifa kutia ndani magazeti ya kwenye ndege (airline magazines). Kuna airlines kama South African Airways ambayo gazeti lao la "Sawubona" linashinda tuzo za best airline magazine kila wakati, wanaweza wakaingia makubaliano nao kutoa makala za hivyo vivutio.

Pia Tanzania Tourism Board wanaweza kufanya makubaliano na airlines, mahoteli na mbuga za utalii kwa ajili ya "tourism packages", ambapo Wizara ya mambo ya ndani wanaweza kutoa free visa kwenye hizo packages.

Na pia tulisaini makubaliano ya anga na USA, kitu gani kinawazuia kufuatlilia direct flights kati ya Washington na Dar? Sio mbali, South African Airways wanafanya safari hizo. Waziri wa utalii atumie nafasi kuzungumza na balozi wa Marekani ili kuitumia nafasi hii vilivyo kwa kuangalia uwezekano wa direct flights za airline za Marekani kuja Dar. Na pia waangalie uwezekano wa kurejesha flights za Lufthansa, kwa kuwa Germans nao wanafanya sana utalii (je mliwafukuza Lufthansa kwa kuwa walipompekua Diria alipogundulika kutumia nafasi yake kufanya biashara haramu?). Acheni siasa katika biashara, wajerumani hawabembelezi mtu bwana, wanaishi kwa sheria wale!

Kama Mkurugenzi wa Shirika la Utalii haiwezi kazi mie nipo waniteue!

Vivutio tunavyo tunaishia kuvikalia tu na kupeleka hela kwenye mambo yasiyozalisha, ovyooo!
 
Daa!! umesema kweli mkuu maana mambo hii hata mie nmesomea na the way talk it seems lke you can lead well basi anza taratibu.
 
Hongera TZ.
Inasikitisha kuona hadi leo hatuwez kuneemeka na utalii au maliasili zetu. Vipusa vinauzwa kwa magendo na wakubwa, zamani walikuwa wanauza ngozi za wanyama siku hizi wanauza wanyama hai, baadhi ya maeneo yameuzwa kwa ubia.. sijui baada ya miaka itakuwaje..Ila mi nilichangia kura kaadhaa at least tupate promotion.. na kuweka uzalendo
 
Bado vipo vingi ambavyo havijatangazwa mfano Pori la akiba selous(Large concentration of wildlife duniani),ziwa Victoria(caldera ziwa kubwa linaloninginia duniani).Lake Tanganyika(deepest lake duniani,lenye viumbe vinavyofanana na vilivyopo baharini),sehemu alipochukuliwa mifupa ya kiumbe Dinosaur ambayo mifupa yake ndiyo pekee iliyokamilika na ambayo wajerumani waliiba huko Kilwa na hawataki kuirudisha TZ).mwenye kujua vingine atujuze?
 
Kile cha wanafunzi walioenda form one bila kujua kusoma walikikumbuka?

Hakina tija, si bora hiki: kiongozi wa nchi hajui kwanini nchi yake ni masikini!, mgonjwa wa mguu anafanyiwa upasuaji wa kichwa na kinyume chake!
 
Nanukuu...!!

''Pamoja na Tanzania kuwa ni nchi ya pili (2) kwa vivutio vya utalii duniani baada ya nchi ya Brazil lakini bado ipo nyuma kwa utoaji wa huduma za utalii ikiwa ni nchi ya mia moja na kumi (110) kati ya nchi mia moja thelathini na tatu (133) hali inayoweza changia kupunguza pato la taifa ilinalotoka na sekta ya utalii''

Hii habari ni kwa mujibu wa ITV Tanzania leo.

Nimejikuta napata uchungu sana juu ya hili, nikaona kama JF tuna haja ya kulijadili hili na kuona udhaifu uko wapi mpaka nchi hii inafikia kushindwa vibaya namna hii katika maswala yahusuyo maendeleo.

Hivi kivutio kimewekwa na Mungu, Tanzania kupitia wizara ya Utalii tumeshindwa kabisa kuboresha na kutangazia ili kupata watalii?? Bajeti ya wizara ya Maliasili na utalii kazi yake ni nini hasa??

Kwa wanaofahamu vyema naomba watujuze nini hasa kazi ya WIZARA YA MALIASILI NA UTALII?? Yule waziri wa utalii hayumo humu atupatie ufafanuzi wa kina juu ya hili!! Ni aibu aibu aibuuu
=============================================

 
Kama waziri usika ana jihusisha na biashara ya meno ya tembo tuna tegemea nn!....
 

Usijisikie uchungu. Elewa kwamba Watanzania tunapenda kujisifia kwenye vyombo vya habari, kama waingerrza na timu yao ya Taifa.

Angalia hapa:
http://en.m.wikipedia.org/wiki/World_Tourism_rankings

Utaona kuwa wenzetu wanaongelea kuingiza watalii zaidi ya milioni ishirini kwa mwaka, sisi tukijitahidi sana eti watalii milion moja. Miaka mingine tunaingiza watalii laki sita na ushee.

Tatizo letu ni kukariri kwamba watalii watakuja kupanda mlima kilimanjaro na kutembelea Serengeti na Ngorongoro pamoja na Zenji.
Vivutio vingine hatuvi-promote. Miji yetu michafu, ipo ugly, usalama wa wasiwasi, hoteli za wasiwasi halafu chache, barabara za kuvifikia vivutio vingine za shida...na matatizo mengine kibao. Sasa ukute sector yenyewe inasimamiwa na ma-much know- wabishi, wanasikiliza ushauri ukitolewa na wakubwa tu, sisi akina yakhe tukiwashauri tunadharauliwa kwa vile hatujui na hatujasomea utalii....

Lakini hii ndio nchi yetu, na ndivyo tulivyo.
 
Tanzania maeneo matatu tu yangeweza kuinua uchumi wetu kama yangekuwa na Viongozi weledi na wenye mapenzi mema na nchi yao.
.Maliasili na Utalii
.Madini na viwanda
.Mifugo na kilimo
 
Tanzania maeneo matatu tu yangeweza kuinua uchumi wetu kama yangekuwa na Viongozi weledi na wenye mapenzi mema na nchi yao.
.Maliasili na Utalii
.Madini na viwanda
.Mifugo na kilimo

Umenena vyema mkuu! Tumekosa viongozi wenye weledi na mapenzi mema kwa nchi yao
 
Mi nadhan serkali imeshndwa kutangaza vyema baadh ya vvutio vngne vya utalii wao wamekarir mikum,selou,n.k wanxahau vvtio vngne km michor ya mapngon kule handen,ziwa ngoz n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…