Viwanda hivi vilikufa, vingine ni mali ya wawekezaji wasanii Marais muliopita tuwaambie nini?

Vijana panueni vichwa vyenu! Zama za kusoma kwa ajili ya kuajiriwa viwandani zilishapita! Hizo ni outdated thinking!
 
hapa ndipo kuna shida kubwa sana.kama tunataka viwanda serikali ikae chini ifikirie hili kwa umakini sana.unakuta menye kiwanda Tanesco inamlipisha gharama kubwa ya ummeme eti anatumia sana umeme.!!ataachaje kuuza kwa bei kubwa bidhaa??
 
Na bora hata vilivyokufa
Viwanda vyenyewe vilikua regional imbalance angalia hapo hakuna kiwanda lindi, mtwara, wala songea inshort ukanda tu ndo ulitawala hapo
Kusini ilitengwa snaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siamini kama Nyerere alirithi viwanda, embu taja hiyo list ya viwanda alivyorithi kwa wazungu. Ina maana hakujenga hata viwanda kadhaa vikubwa miaka yote 24?
Soma history vizuri utajua hakuna kiwanda kilichojengwa na Nyerere vyote vili taifishwa!!!.. Cabinet ya Nyerere ndio ilikuja kuua vyote
 
Soma history vizuri utajua hakuna kiwanda kilichojengwa na Nyerere vyote vili taifishwa!!!.. Cabinet ya Nyerere ndio ilikuja kuua vyote
Hayo ndio madhara ya balehe za siku hizi. Hebu weka hapa source ya hiyo historia yako tuisome na sisi tujifunze mapya!
 
Hayo ndio madhara ya balehe za siku hizi. Hebu weka hapa source ya hiyo historia yako tuisome na sisi tujifunze mapya!
Balehe ya siku hizi nzuri sana ndio maana tunaakili na tunajua history vizuri,1970 Tanzania ilikua masikini wa kutupwa tulikua tumeua viwanda vyote!!!...mtu anayesema Nyerere alijenga viwanda nadhani hajui history vizuri (Nchi hii ni ya wakulima) wakati wa kupiga kura ya uhuru ilikua jumatatu siku ambayo watumishi wote wa serikali na viwandani walikua kazini!!
 
Ndio umemaliza hiyo historia yako? POLE SANA KIJANA!
 
Hayo ndio madhara ya balehe za siku hizi. Hebu weka hapa source ya hiyo historia yako tuisome na sisi tujifunze mapya!
Na kuelimisha tena wakati wa uhuru wafanyakazi,wafanyabiashara hawakuwa tayari kwasababu walijua utaifishaji utatuacha masikini wa kutupwa..na wakoloni walikua wanawaambia mkipiga kura ya uhuru Nchi hii itakua jiwe!!..ndio maana tunasema Nchi ya wakulima na wanyonge
 
Mpaka sasa awamu ya tano imefufua vingapi na Sera yake ya viwanda?
 
Mutex kiko Musoma na si Mwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hebu taja viwanda vilivyokuwepo wakati nchi inapata Uhuru.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viwanda VILITAIFiSHWA NA AZIMIOLA ARuSHa kuanzia mwaka 1967 na kuendeleza. Vikawekwa Chini ya UMMA wa Watanzania. Wakaanza kuvibomoa, kuiba Mashine na Spare PArts zake. Mwisho Viwanda vikawa Godawuns. Mfano kile cha Sunguratex Gongo la mboto. Waliiba Hadi milango na na madirisha zikabaki kuta tuuu. Siasa Ujamaa na Kujitegemea Iliyolenga kuondoa Capitalism(Ubepari), Ukabaila, ubwenyenye, Ubwana, Ubeberu na mengineyo. East Africa Community ya 1977 ikafa, 1978-1979 Vita kuu na Uganda. Matokeo Viwanda na Mashamba makubwa ya Wazungu vikazidi kufa. Tukaingia kwenye mdororo wa Uchumi. Bidhaa muhimu zikapotea, ukazuka Ulanguzi na RTC na Maduka ya Ugawaji kwa foleni. 1979 Ukame na njaa Kali Hadi 1984.Sokoine akapambana Hadi akafa. Wazungu wakatutenga. Shilingi ikashuka. Mwinyi akatawala akaleta Ruksa ya kuleta bidhaa yoyote Tz. Hatimaye Mkapa akatawala akawaridhia Wazungu wakafufua Uchumi. Serikali ikajivua dhamana ya kutoa ruzuku Kwa Social Services tukaleta User fee angalau sh 300. Uchumi ukafufuka. Kikwete akayaendeleza ya Mkapa Uhisiano wa kimataifa Ukakua pamoja na Uwekezaji. Awamu ya 5 tunajenga Viwanda Vipya.
 
Siamini kama Nyerere alirithi viwanda, embu taja hiyo list ya viwanda alivyorithi kwa wazungu. Ina maana hakujenga hata viwanda kadhaa vikubwa miaka yote 24?
Ni kweli Viwanda alivyojenga Nyerere ni Vichache sana. Vingi vilijengwa na Wahindi na Wazungu. Alichofanywa Nyerere Chini ya Siasa ya Ukamaa na Kujitegemea ni kuviTAIFISHA(NATIONALISATiON). Yaani kuweka Chini ya Wazawa UMMA wa Watanzania. Tukashindwa kuendeleza Vikafa. Mfano wa Tanganyika Packers ya Kawe(Cow Way). Kiwanda kilisindika nyama ya kopo ikawa inauzwa Arabuni, Ulaya na USA. Mzungu wa kiwanda hiki alinunua Ngombe Usukumani, Tabora na Arusha. Alikuwa na Eneo maalum la kuwalisha kabla ya kuchinjwa. Nyumba za wafanyakazi na mengineyo. Kiwanda kilishamiri Biashara Safi. Hata Mimi nilikula nyama ya Kopo ya Kawe. WalivyoTaifisha tu Hadi Leo hakijawahi kufanya Kazi. Matokeo yake Eneo la Tanganyika Packers limekuwa Eneo la Mikuano ya Injili, Nyumba NHC zinajengwa pale, wauza Maua wanamiliki, stand ya Mabasi na shughuli nyingine. Kiwanda chetu cha Nyama tulikiua Sisi wenyewe Kisiasa. Tena wakati wakaanza kuzichakata. Wanasema ziliozea ndani pakanuka miezi 3. Mashine zake Sijui zilipelekwa wapi.
 
Ptuuuuu! aibu kubwa! nahisi umetoroka mirembe wewe sio bure!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…