Wakati Nuhu Peter Changawa alipojiunga na Twyford Tanzania mwaka 2017, alikuwa ni mtaalamu wa ghala mwenye ujuzi mdogo wa usimamizi wa maghala ya kisasa. Hii leo, anasimamia operesheni za ghala katika kiwanda cha kusindika glasi, akipanda cheo kutoka mtaalamu hadi msimamizi na meneja wa ghala. Kazi yake ilimpeleka kwenye kiwanda cha kauri cha Twyford Zambia, ambako alipata ujuzi zaidi.
Katika safari hiyo, wafanyakazi wenzake kutoka China walimfundisha mifumo ya kisasa ya usimamizi wa ghala, usimamizi wa kidijitali wa orodha ya bidhaa, ufuatiliaji wa malighafi, na njia za kuboresha ufanisi wa uendeshaji. Anasema kilichomvutia zaidi kwa wafanyakazi kutoka China ni nidhamu yao ya kazi, umakini katika kila kitu, kushikilia ubora, na kuwa tayari kushirikisha ujuzi wao kwa waajiriwa wenyeji.
Kufanya kazi katika kiwanda cha Twyford Tanzania si tu kumemsaidia Changawa kuboresha ujuzi wake wa kitaalamu, bali pia kumeleta utulivu mkubwa wa kifedha kwa familia yake huku kukiimarisha hisia ya nidhamu, uwajibikaji na kufanya kazi kama timu.
Kama Changawa, karibu mafundi 1,000 katika kiwanda hicho wamepata mafunzo ya utengenezaji wa bidhaa za glasi, operesheni za kiufundi na umeme, na ukaguzi wa vifaa. Kwa mujibu wa meneja wa kiwanda cha ufundi wa umeme Wan Guanru, waajiriwa Watanzania kwa sasa wanaweza kufanya kazi bila kusimamiwa kuanzia uzalishaji hadi usimamizi.
Hadithi ya Changawa ni moja kati ya nyingi zinazojitokeza kutoka kampuni ya Kimataifa ya Twyford barani Afrika, ambako uzalishaji wa ndani unaenda mbali zaidi ya ujenzi wa viwanda mpaka uhamishaji wa ujuzi wa kiviwanda, kuchochea thamani ya mnyororo wa thamani wa ndani, na kupanua uwezo wa utengenezaji. Twyford ilianza uzalishaji wa kauri nchini Tanzania mwaka 2017 na baadaye kuanza utengenezaji wa bidhaa za glasi. Hii leo, inaendesha viwanda viwili vya bidhaa za glasi na kiwanda kimoja cha kauri nchini humo, na kutoa ajira kwa zaidi ya watu 2,000, na zaidi ya asilimia 90 ni Watanzania, kwa mujibu wa naibu mkurugenzi Zhu Kaihong.
Zaidi ya asilimia 90 ya mali ghafi na nishati inayotumika katika viwanda vya bidhaa za glasi pia zinapatikana nchini humo, ikiwemo mchanga wa silika, gesi asilia, feldspar, dolomite, na chokaa. Zhu anasema, umuhimu wa manunuzi ya ndani si tu kwa ajili ya kupunguza gharama za uzalishaji, bali unahusu kuwezesha miradi ya uzalishaji kuwa mizizi halisi ya ndani.
Mchakato kama huo unaonekana nchini Senegal, ambako Twyford ilianzisha kiwanda cha kauri mwaka 2017 na kuanza uzalishaji mwaka 2019. Kiwanda hicho sasa kina uwezo wa mwaka wa mita za mraba milioni 33.5 na kuajiri watu 1,892, wakiwemo waajiriwa wa kudumu na wafanyakazi wanaoajiriwa kwa mikataba ya muda mrefu. Kampuni hiyo inafanya kazi na karibu wasambazaji 300 na kuuza bidhaa zake katika nchi kama Gambia, Mauritania, na Cabo Verde. Meneja wa biashara Cheikh Boucounta Diop anasema, kiwanda hicho kimeisaidia Senegal kupunguza utegemezi wa nje huku kukitoa fursa kwa sekta za madini, uchukuzi, na usambazaji.
Kwa waajiriwa kama Sandjiry Ba, ambaye alijiunga na kampuni hiyo mwaka 2022 na kuwa kiongozi wa uchapishaji wa inkjet katika karakana ya mstari wa bidhaa za kioo baada ya kupata mafunzo kutoka kwa mafundi wa Kichina, kiwanda hicho kimekuwa sehemu ya kutengeneza ajira na kupata ujuzi wa kuwarithisha wengine.
Kwa wafanyakazi wazawa kama Changawa na Ba, mabadiliko ni ya kibinafsi, fursa za kupata ujuzi mpya, kuwajibika zaidi, na kujenga maisha ya utulivu zaidi. Kwa uchumi mpana, uhusiano kama huo unatoa njia ya kuendeleza nguvukazi yenye ujuzi, kuongeza kwa kina uwezo wa ndani wa uzalishaji, na kuboresha thamani ya mnyororo wa kiviwanda.