Viwanda vya kuunda mabasi vilazimishwe kuzalishia mabasi Tanzania

Viwanda vya kuunda mabasi vilazimishwe kuzalishia mabasi Tanzania

Zamani Mabasi yalikuwa yakitengezwa humu humu Nchini, baadae katika miaka 90 ndio tukaanza kuona Mabasi ya Kenya, tena Mkoa wa Tanga ndio waanzilishi.

Tanroads walipoanzisha Mizani za Barabarani yale Mabasi yetu na ya Kenya yakawa ni mazito, ndio Mchina na Brasil wakaingia sokoni na Double axle na body za Fiberglass.

Sasa hivi Mchina Brasil ndio anaongoza
Mkuu, nafikiri mleta mada alenga kuhusu Town buses.

Yaani UDART inakuwa na yashirikiana na wenye biashara ya "town buses" ambao nao hununua mabasi au kufanya "leasing" kutoka kwenye viwanda vya mabasi.

Yaani kunakuwa na transport system ambayo yaunganisha wadau wote bila vurugu wala kutupiana ngumi.

Transport system inounganisha bus makers, bus terminals, route planners, surveyors, town planners na wale wengine.
 
1. Kama mnavyojua sekta ya USAFIRISHAJI imekua kwa kiasi kikubwa. Lakini la kusikitisha mabasi yaliyo Mengi huagizwa China na Kenya.

2. Je haiwezekani kuwalazimisha wenye viwanda hivyo kujenga "Assembly plant" nchini kuongeza ajira, Kodi na ukuzaji/urithishaji teknolojia/maarifa kwa wazawa?

NB: waagizaji nao walazimishwe kununua basi nchini Tu.

**SIDO, NIT, UDSM (CoET), DIT amkeni
Kwanza Tofautisha Kiwanda cha kuunda na ku Assemble, Africa most of time ni viwanda tu vya Ku assemble, kuunda from scratch hizo level hatujafika bado.

Tanzania pia kuna hivyo viwanda vya ku assemble mimi sio mtu sana wa Magari wenye ujuzi wataongezea ila haya mabasi, pikipiki, Malori etc huwa hayaji kama unavyoyaona, Assembly hufanyika hapa hapa Nchini.

Pitia hapa
 
1. Kama mnavyojua sekta ya USAFIRISHAJI imekua kwa kiasi kikubwa. Lakini la kusikitisha mabasi yaliyo Mengi huagizwa China na Kenya.

2. Je haiwezekani kuwalazimisha wenye viwanda hivyo kujenga "Assembly plant" nchini kuongeza ajira, Kodi na ukuzaji/urithishaji teknolojia/maarifa kwa wazawa?

NB: waagizaji nao walazimishwe kununua basi nchini Tu.

**SIDO, NIT, UDSM (CoET), DIT amkeni
Inawezekana uganda wanafanya

Google "KIRA motors uganda"
Au " metu bus industry"

View: https://www.tiktok.com/@metu.bus/video/7448190751894293766?_r=1&u_code=dbf59cl9ck6me1&preview_pb=0&sharer_language=en&_d=e7ic522lg2k5g7&share_item_id=7448190751894293766&source=h5_m&timestamp=1734542931&user_id=6808050075873428486&sec_user_id=MS4wLjABAAAATg0QnrViyNCBqdPQ6KP2oB1dhi7pORdsn4MLbXqnJcZSdRSsjxKzlaJmTWnpBMJ5&social_share_type=0&utm_source=whatsapp&utm_campaign=client_share&utm_medium=android&share_iid=7391795065691719429&share_link_id=79bd078a-fd37-4749-865b-b0d27a49f4d9&share_app_id=1233&ugbiz_name=MAIN&ug_btm=b2001&enable_checksum=1
 
Nadhani, sina utalaamu wowote kwenye magari
Hapa unaongea na Dereva wa Truck kwa miaka 30 sikutaka kuendesha Basi baada ya kuona Madereva wa Mabasi wakifa sana kwa UKIMWI.

Nilikuwa na jamaa zangu wengi madereva wa mabasi walioondoka na Juliana.

Lifespan ya Dereva wa Basi miaka 90 ilikuwa ni ndogo sana.
 
Lakini pia mtambue technology inabadilika Kwa Kasi sana. Mtawezana na speed hiyo. Wenzako wako toleo la kumi wewe ndio kwanza unaangaika na teo la kwanza
 
Siku nikiwa Rais wa hii nchi kila bidhaa inayoagizwa kwa wingi nje ya nchi itategenezewa Tanzania. Kama wawekezaji watakataa kuuza kuleta teknolojia nitajenga kiwanda kimoja kila baada ya miezi mitatu.

Ninaamini 100% Africa hatuendelei sio kwasababu ya ujinga tuliolishwa miaka mingi shida ni hatuzalishi tunavyotumia. The largest importer ni USA, China , Germany.......na ndizo nchi tajiri duniani
Baba wa Taifa Mwl JK,Nyerere(RIP)alijenga viwanda vingi sana nchi hii viliishia wapi? Tuanzie hapo kwanza.
 
Mzungu kakaba Kona zote hata Afrika kusini Wana assemble hawatengenezi kuanzia mwanzo kitu ambacho nilikua sifahamu, Afrika kiwanda cha kuunda gari kuanzia mwanzo hakuna ni viwanda vya kuunganisha magari Tu
 
Unazungumzia kuunda mabasi hapa...ulishajiuliza kwanini taasisi inayohusika na kutunza mazingira inashindwa kuweka sheria dhidi ya makampuni yanayozalisha chupa za plastic kama chupa za maji, maziwa na zile za bia kama HENKEN au WINDHOEK ili chupa ziwe ziwe kama za soda au bia ili kutunza mazingira?
Yaani wewe ukinunua chupa kuna kiasi cha pesa unaiacha dukani ili ukirudisha chupa chochote kwenye duka yoyote unarudishiwa pesa yako...
Viongozi wetu hawako serious na maisha ya wananchi wao.
Morocco hapo tu wanaunda Magari siyo kwamba pachasing power yao ni kubwa balk ni nia ya viongozi wao kuona umuhimu wa wananchi wao kusogezewa huduma hiyo karibu.
Yaani unatoa pesa kiasi cha 50bilioni kurudia uchaguzi wa wabunge ambao wewe ndiye umewashawishe waachane na chama chao cha awali alafu uwarudishe tena kufanya majukumu yaleyale....si utahira huo.
 
Siku nikiwa Rais wa hii nchi kila bidhaa inayoagizwa kwa wingi nje ya nchi itategenezewa Tanzania. Kama wawekezaji watakataa kuuza kuleta teknolojia nitajenga kiwanda kimoja kila baada ya miezi mitatu.

Ninaamini 100% Africa hatuendelei sio kwasababu ya ujinga tuliolishwa miaka mingi shida ni hatuzalishi tunavyotumia. The largest importer ni USA, China , Germany.......na ndizo nchi tajiri duniani
Unaongea kama kweli vile..ukiwpa huna hela wewe ni zero tu hata uwe na mamlaka kiasi gani.? Hizo nchi unazoziongelea ni matajiri haswa..!
 
Hapa unaongea na Dereva wa Truck kwa miaka 30 sikutaka kuendesha Basi baada ya kuona Madereva wa Mabasi wakifa sana kwa UKIMWI.

Nilikuwa na jamaa zangu wengi madereva wa mabasi walioondoka na Juliana.

Lifespan ya Dereva wa Basi miaka 90 ilikuwa ni ndogo sana.
Hongera mkuu, 90 ulikuwa unaendesha lori? da tukupe maua ako asee
 
Back
Top Bottom