Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Mkuu, hii ya kusema hatujafika hizo level haina afya, mbona tulikuwa na kiwanda cha kuunda body za Scania Kibaha?Kwanza Tofautisha Kiwanda cha kuunda na ku Assemble, Africa most of time ni viwanda tu vya Ku assemble, kuunda from scratch hizo level hatujafika bado.
Tanzania pia kuna hivyo viwanda vya ku assemble mimi sio mtu sana wa Magari wenye ujuzi wataongezea ila haya mabasi, pikipiki, Malori etc huwa hayaji kama unavyoyaona, Assembly hufanyika hapa hapa Nchini.
Pitia hapa
Waunda bodi za Mabasi ya TZ na Kenya
Muundo wa body za mabasi yanayotengenezwa TZ na Kenya ni tofauti. Bodi za TZ (SCANIA DAR COACHES) Mbele Dar Express na bodi zilizoundwa TZ na DAR coach Mabasi yenye chesis ya SCANIA na Bodi zilizoundwa TZ Ndani Kwenye Dashboard Bodi za Kenya Kwa hapa Wakenya...www.jamiiforums.com
Au mbona tulikuwa na kiwanda cha kutengeneza matairi cha General Tyre Arusha.
Nakataa mtu ukisema hatujafika level hii, tulitakiwa tuwazidi Kenya na Uganda kwenye hili la kuunda mabasi na by products zake.
Twatakiwa kumpata mbia kwa mfano kutoka China ambao wao sasa wamehamia kwenye EV ambae ataunda mabasi na kutuachia teknolojia yake tukimlipa ada.
Au Ulaya kutoka nch zile ndogondogo kama Hungury ambao nao wana viwanda vya kuunda mabasi watupatie wataalam wa kutufundisha kuunda mabasi kisasa, huo ndo ushirikiano wa kistratejia.
Hivyo tutaweza kuunda mabasi kwa muda wetu na kwa kutumia vijana wetu waso na ajira.