KERO Viwango vya mishahara sekta binafsi haviendani na viwango vilivopangwa na Serikali hasa kada ya watunza kumbu kumbu

KERO Viwango vya mishahara sekta binafsi haviendani na viwango vilivopangwa na Serikali hasa kada ya watunza kumbu kumbu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Changamoto ya salary scale kwenye mashirika yanayofanya kazi sekta binafsi baadhi Yao wanalipa mshahara mdogo ambao hauendani na salary scale iliyowekwa na Serikali na ni ajira za mkataba.

Hata pale wanapohuisha mkataba mpya badala ya mshahara kuongezeka, unaweza ukabaki pale pale angali majukumu ya kazi kwa mtumishi anaongezewa zaidi kwa ukubwa sana na gharama za maisha zimepanda sana.

Mfano tu, mafuta yapo juu lakini mshahara kwanini ubaki pale pale au ukashuka zaidi haswa cadre ya watunza kumbu kumbu yaani data clerks? Unakuta mtumishi ameajiriwa ana degree analipwa mshahara wa scale ya diploma na wa diploma analipwa mshahara scale ya ngazi ya cheti. Je, ni halali kweli kuwatendea hivi hawa watumishi?

Tunaomba mfuatilie hili, hasa hasa mradi wa kuzuia na kupambana na virusi vya UKIMWI kupitia shirika la HJFMRI nyanda za juu kusini.
 
Eeh mkuu hii ni ngoma kweli, wengi wetu tunakaa kwenye mashirika binafsi na mshahara unakuja kama ni sadaka. Salary scale ya serikali ni ndoto tu hapo, mkataba unasema moja na ukianza kusema unatishiwa kuachishwa kazi. Nimeona wenzangu wakilalamika kila siku. ngoma
 
Back
Top Bottom