Mnaojenga Kigamboni, miaka ishiri ijayo mtalia.
Kigamboni ni tambarare, ardhi ikisha jaa nyumba, maji yakashindwa kuzama ardhini, sasa dhahama ya mafuriko ndio itawakumba.
Fuateni agizo la waziri wa ardhi. Safety ya Kigamboni iko kwenye kumilikisha wakazi viwanja vya low density.
Pia kwa sasa wizara iangalie uwezekano wa kupiga marufuku nyumba za Dar kuwekewa paving blocks.
Paving blocks zinablock maji ya mvua yasizame ardhini hivyo kusababisha mafuriko ya mara kwa mara Dar.
Kama mtu anaweka paving, basi asiweke eneo linalozidi 30sq meter kwa ajili ya maegesho ya gari. Eneo linalobaki lipandwe nyasi.