Mung Chris
JF-Expert Member
- Sep 12, 2017
- 3,391
- 3,849
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ametanza rasmi kuanzia July 01 2021, kuanza kwa zoezi la Kitaifa la uhakiki wa umiliki wote wa ardhi kwa kutumia kitambulisho cha NIDA kwa Nchi nzima.
“Tunataka Wamiliki wote hewa waliomilikishwa kimakosa, kiwizi, kiutapeli na kiujanja lazima tuwabaini lazima tujue kwa nini jina lako la kiwanja halifanani na majina ya hati yako ulipataje, tukiwabaini waliomilikishwa kimakosa viwanja vyao tutavipiga mnada ili Serikali ipate hela"