Mr Why
JF-Expert Member
- Nov 27, 2019
- 2,992
- 5,665
"Hakuna kitu kitakachompata Ibrahim Traoré ilimradi mimi bado niko hai. Marekani au Ufaransa hawana haki ya kumkamata Rais wa taifa huru la Afrika." __ Rais wa Urusi, Vladimir Putin.
"Nataka kufanya mambo kuwa wazi kabisa. Rais Ibrahim Traoré alinifata baada ya yeye mwenyewe kutathmini na kuchagua njia ya hatima kwa nchi yake. Mimi nilijiunga naye tu kama mshirika wa kibiashara na rafiki ili kumsaidia kutimiza ndoto zake.
Urusi haimnyonyi wala kuiba chochote kutoka Burkina Faso, yote ni Biashara ya Haki. Biashara kati ya Urusi na Burkina Faso ni rahisi: tunasubiri nchini kwetu, na Burkina Faso wanachimba madini yao, kuyachakata na kuyaagiza kwetu kwa masharti yao wenyewe. Kama tungekuwa tunawanyonya, tungekuwa na shughuli za uchimbaji za Warusi kule Burkina Faso, lakini hatuna kwa sababu Urusi inaamini katika Biashara ya Haki.
Nina kila kitu kinachohitajika kusambaza ushawishi wangu kote duniani kama Superpower, lakini Urusi haijawahi kutumia mabavu dhidi ya yeyote.
Marekani na Ufaransa wanampinga Bwana Ibrahim Traoré kwa sababu hawawezi tena kuiba rasilimali za Burkina Faso chini ya uongozi wake. Badala ya kuruhusu Burkina Faso kujichimbia madini yao na kuuza bidhaa zilizokamilika, wao wanataka kuchimba wenyewe na kuiba kutoka kwa watu wa Burkina Faso. Sasa, kwa sababu hawawezi tena kuiba, wanamchafua kwa kumuita mwizi ili wapate sababu ya kumuondoa, lakini hilo halitatokea.
Hivi ndivyo wanavyofanya kila mara nchi wanazozidhibiti zinapojinasua na kuanza kukua. Mimi namwona Ibrahim Traoré kama ndugu yangu na nitafanya kila liwezekanalo kumlinda. Marekani au taifa lolote jingine halina mamlaka juu yake. Yeye ni rais wa nchi huru ya Afrika na anastahili heshima."~Rais Vladimir Putin