Vladimir Putin amewataka wanajeshi wa Ukraine wajisalimishe wenyewe

USA tayari anayo Alaska sebleni kabisa kwa Russia na hajafanya lolote juu ya hilo,

Russia anajazwa tu, kuna mstari anasubiliwa auvuke

Sent from my HUAWEI LUA-U22 using JamiiForums mobile app
Alaska waliiuuza Warusi kwa Marekani kwa hiari.
Alaska ipo bara la America, unasemaje sasa wapo sebuleni kwa Urusi.
Jifunze jiografia vizuri
 
Tatzo humu ndani watu wanamlaumu putin bila kujua sababu..
Afu nmegundua watz wengi hawajui vitu vingi wao kazi yao ni kusoma vichwa vya habar ya ulaya na us na kumlaum putin bila kujua hata chanzo ni nn...
Safi sana Putin.. wao si wahuni tuone sasa
Kunywa kinywaji ghali, muamala utakufwata.
 
Maelezo mazuri kabisa haya.
 
Uko na akili ndogo hadi naona nikikujibu napoteza muda bure...propaganda za Marekani zimejaza fuvu lako
Bahati nzuri/mbaya hunifahamu. Laiti ungalinifahamu ungefuta hiyo “akili ndogo” haraka sana na kuniomba nikupe elimu ya uhakika kuhusu masuala ya modeli hii.

Vijana ndio mnaishi ulimwengu wa propaganda sana kuliko kutafuta elimu ya uhakika. Hapa tayari mmeshaligeuza suala hili kuwa “mechi kati ya Mrusi na Mmarekani”! Na makundi ya wachangiaji yanajitanabahisa kati ya mashabiki wa udikteta na wale wa demokrasia.

Jitahidini kujenga “rational thinking” badala ya kutawaliwa na hulka za kishabiki hadi katika masuala ya maana.
 
Taja mkataba aliouvunja Putin ila nakwambia Ukraine hawakueshimu Wala kuimplement Minsk Agreement
 
Hii iko wazi. USA haiwezi kuingia vitani. Putin mwenyewe angekuwa na taarifa za uhakika kuwa US wataingia asingeanzisha hiyo vita.

US watamuachia “ajinyonge mwenyewe” huku wao wakimpiga vikwazo na kugawa na kuuza silaha tu.

Jua tu Urusi si tishio kiuchumi kwa USA. Silaha za nuklia ndani ya umasikini si lolote ni kama North Korea tu. China ndio tishio la leo.
 
Laana ya kumdhurumu Dr.Shika iko mbioni kuwageukia Warusi. Waende Nyanguge,Magu wakaungame kwenye kaburi la Mzee wa "mia tisa itapendeza".
 
Kama si Tishio wasingeifatilia kwa namna ya kipekee kumbuka Marekani wanaijua nguvu ya Urusi kuliko tunavyodhani.

Putin ameamua liwalo na liwe na Mmarekani Hana Cha kufanya either aingie au akae pembeni.

Kumbuka Ukraine haipo pamoja kama Taifa, upande wa Mashariki wanamsapoti Putin na Magharibi wanataka NATO.
 
Marekani ilipokuwa inaenda kuishambulia Iraq ilikuwa na manufaa gani kwa taifa lake?
 

Hata sisi hatufagilii Zanzibar wajiunge na OIC.
 
Offcourse,
Na hii ni karata kwa usa nadhani ye atangalia fursa za kiuchumi kwake kwenye huu mgogoro wa hawa ndugu wawili,
Ku step inn kurushiana makombora na russia ni upumbavu tu kwa sasa na hakuna atakachopata zaid ya hasara kwake,
Ila kwa influence yake akitia fitna zake russia akawekewa sunction za kiuchumi na ye akakamata fursa ata mpiga gape kubwa la kiuchumi russia,na huo ndo ushindi mzuri kwa sasa..
Na am sure 99%..huu ndo ushauri wa kitalaam alopewa biden..
 
Umeandika point zinazoweza kujadiliwa. Lakini kwanza rekebisha lugha (literally & figuratively) kisha jihadhari sana kuchukulia watu kirahisi rahisi.

Sijui umewezaje kunitambua kama form four leaver tena wa division zero. Enzi zangu division hazikuwepo na wengi walioishia form four walikuwa na hadhi ya graduates wa leo.

Nenda taratibu weka kiburi pembeni. Ongea kama msomi hakika utapata positive feedback ya maoni yako. Utaelimika zaidi.
 
Marekani ilipokuwa inaenda kuishambulia Iraq ilikuwa na manufaa gani kwa taifa lake?
Ulikuwa ni uamuzi mwingine wa kipumbavu sana uliofanywa na Rais GW Bush katika misingi ya uongo na unafiki.

Haukuwa na manufaa yoyote kwa Marekani na ulileta maafa makubwa kwa waIraq na askari wa Marekani na washirika wao. Tena uliwezesha kuanzishwa kwa ISIS.

Inakisiwa makampuni binafsi ya Marekani (defense contractors) yalisanya mabilioni ya US dollars kwenye vita ile.
 
Marekani ni tatizo kubwa na Ukraine wana lazimishwa kujiunga NATO kwa manufaa ya 🇺🇸
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…