VoA: Tanzania imepokea mkopo kutoka kwa Korea Kusini na kutoa sehemu ya bahari na madini

VoA: Tanzania imepokea mkopo kutoka kwa Korea Kusini na kutoa sehemu ya bahari na madini

Hivi nchi inapotaka kukopa ni Rais anaamua tu akakope au kuna vigezo vingine? Hatari hii
Maana hata na baba mwenye busara akitaka kukopa huwa anashirikisha familia.
Ndio mtapoona umuhimu wa katiba ya kimarekani...Kabla ya raisi kwenda kukopa lazma wabunge waidhinishe kwa ridhaa ya raia wao.
 
Picha hii inaonyesha ujumbe wa Tanzania (wageni) ulijaza chumba cha mkutano mpaka wakakosa viti, wakati ujumbe wa Korea (wenyeji) walikuwa wanne. Wajumbe wote hao wanalipwa per-diem na kodi zetu?

img-20240603-wa0020-jpg.3007813
Wajumbe wa tz wako makini sana
Hapo mtegemee mrejesho mzuri
Kabisa kuhusu ziara yao huko
Lazima samsung,hyundai waje kuwekeza huku

Ova
 
Hapo sasa nakuelewa mkuu... huyu mama anahitaji kukemewa vilivyo yeye na hao wasaidizi/washauri wake ambao kimsingi hawana nia njema na taifa hili pamoja na vizazi vyake.

Binafsi nimekuwa nikiamini tangu siku ya kwanza huyu mama anahitaji kuongozwa hili uongozi wake uwe na tija kwa taifa, lakini watu hao wa kumuongoza wawe ni watu makini na wenye nia ya dhati kabisa na taifa hili, kwa bahati mbaya sana yeye anaongozwa na madalali yanayoangalia future ya familia zao tu basi na sio future ya taifa letu.
Unamrudisha katika chama mtu kama ABDULRAHMAN KINANA,mkuu unatarajia nini?!
Huyo Kinana nani asiyejua historia yake ya ubadhilifu wa mali za umma/ufisadi!?
Pia hana msimamo madhubuti.
Pia hana maono.
Hapa katika maono ndipo alipoharibu kabisaaa!
Kiufupi hili taifa ili lipone kuna mawili yafanyike kwa pamoja ama moja wapo;
1)CCM ibadili sera zake za chama/za uongozi,maana sera za sasa kandamifu na nyonyefu na zimepitwa na wakati.
2)CCM iondoke madarakani.
 
Mosi, Watanzania fanyeni kazi kwa bidii kila mmoja kwa nafasi yake, ili kwanza kupata maendeleo binafsi kiuchumi...

Pili, Watanzania wa kada zote epukeni kuendekeza rushwa na ubadhirifu wa fedha za umma, waliopewa nafasi ya kuwa wafanyakazi kwenye taasisi za umma wamegeuka kuwa wala fedha na wabadhirifu waliopindukia...

Tatu, Watanzania wengi wangali wajinga wasioweza kutumia hata 3% ya ubongo ambao wamepewa bure kabisa na Mungu. Watanzania walio wengi kwa makusudi kabisa wamekuwa ni watu wa kukiuka taratibu za kimaendeleo zilizoanishwa wazi na hata ambazo hazipo wazi (zinazohitaji common sense) na ndio maana utaona Watanzania wanaharibu miundombinu kama ya barabara, wanajenga nyumba kiholela tu, mambo ya kipuuzi yana wafuasi wengi kuliko mambo ya maana n.k
😁😁😁😁😁😁😁 upuuzi unaambatana na pongezi za rushwa ndio maana unashabikiwa na wajinga wengi. Vitu vya maana huwa havina wafuasi
 
😁😁😁😁😁😁😁 upuuzi unaambatana na pongezi za rushwa ndio maana unashabikiwa na wajinga wengi. Vitu vya maana huwa havina wafuasi
Hii umenikumbusha kitu,kina mama wakipitia changamoto za uongozi wa CCM karibia na uchaguzi wanahongwa pesa za vicoba na vitenge na mablauzi kesho utashangaa wameshika mabango"chagueni CCM".
LAMAMAYEEE!
Vipesa vya vicoba vikiisha CCM isharejea madarakani msoto wa miaka mitano tena.
Nahisi pia wananchi wa TZ tuko na shida mahali.
 
Tanzania na Ethiopia zimesaini mikataba kadhaa na Korea Kusini kwa ajili ya kupata mikopo ya mabilioni ya dola kwa ajili ya maendeleo.

Mikopo hiyo itaiwezesha Korea Kusini kupata fursa ya kuchimba madini muhimu katika nchi za Afrika.

Korea Kusini imeandaa kongamano na viongozi 30 wa nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania na Ethiopia.

Kongamano linafanyika wiki hii

Tanzaia imesema kwamba itakopa dola bilioni 2.5 kutoka kwa Korea Kusini katika muda wa miaka mitano ijayo. Mkopo huo utalipwa katika muda wa miaka 5.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan vile vile amesaini mkataba utakaoiruhusu Korea Kusini kutumia bahari yake na madini yanayotumika katika teknolojia ya nishati safi kama Nickel, Lithium na Graphite.

Ethiopia nayo imesaini mkopo wa dola bilioni 1 utakaolipwa katika kipindi cha miaka minne kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu, sayansi na teknolojia, afya na maendeleo ya mijini.

PIA SOMA
- Ziara ya Rais Samia Korea Kusini atasaini Mkopo wa Tsh. Trilioni 6.51

- Prof. Kitila Mkumbo akanusha masharti ya Mkopo wa Korea Kusini

Voice of America
Ina maana sisi tunachojua ni kukopa tu sio kuuza
 
Hii umenikumbusha kitu,kina mama wakipitia changamoto za uongozi wa CCM karibia na uchaguzi wanahongwa pesa za vicoba na vitenge na mablauzi kesho utashangaa wameshika mabango"chagueni CCM".
LAMAMAYEEE!
Vipesa vya vicoba vikiisha CCM isharejea madarakani msoto wa miaka mitano tena.
Nahisi pia wananchi wa TZ tuko na shida mahali.
Shida ni tamaa, ubinafsi tu na upumbavu. Maana mpumbavu ni mtu ambaye huwa hajifunzi tokana na makosa.

Mtu anajiwazia yeye na familia yake tu. Hiki ndio kitatupeleka kwenye kuangamia huko mbeleni. Matatizo yetu common hatuyabebi kama Taifa ila kila mtu anajiangalia yeye na familia yake tu.

Unadhani kwanini mtu akipata nafasi anawaza kujaza ndugu zake tu.
 
URONGO. Hakuna masharti kama hayo. Mkopo huu ni sehemu ya makubaliano katika awamu ya pili ya ushirikiano wa miaka mitano ijayo. Ni mkopo nafuu utakaolipwa katika miaka 40 kuanzia mwaka wa 26 kwa riba ya 0.01%.
Kuhusu madini ya kimkakati (strategic mineral resources-SMR), mkakati wa Tanzania ni kutafuta wawekezaji watakaowekeza katika utafiti, uchimbaji na kuongeza thamani ndani ya nchi.
Tumeweka wazi duniani kote kuwa tunataka wawekezaji watakaosafirisha betri za magari na sio madini ya kimkakati kwa lengo la kutengeneza betri hizo nje ya nchi. Kuhusu uchumi wa buluu, tumesaini mkataba kwa lengo la kushirikiana katika kuboresha teknolojia ya uvuvi, kujenga bandari za uvuvi na viwanda vya kuchakata Samaki. Eneo lingine ni ushirikiano katika teknolojia ikiwemo kujenga chuo cha TEHAMA nchini.
Yakitimia hayo yote niite PUSSY CAT nimekaa pale.
 
Hakuna tofauti na watoto walioachiwa ghorofa la urithi kariakoo halafu msimamizi wa mirathi aseme waliuze kila mtu afe na chake badala ya kuchukua kodi za kila mwaka.
Hao watoto wapo Mkuranga kwa sasa wamenyorodoka, mgao wa mauzo ya ghorofa za kurithi ulikata mwaka mmoja tu baada ya kugawiwa.

Hawana kitu kabisa, huwezi amini kama waliwahi rithishwa maghorofa kariakoo.
 
Najua sana hilo, but you can give a warning! wajue kuwa hawana ridhaa ya wananchi. Let the international community get informed of that rubbish
Mkuu unataka wananchi waitishe mkutano na kufanya maamuzi kuhusu ilo? Viongozi wanatenda kwa niaba ya watanzania
 
Back
Top Bottom