VoA: Tanzania imepokea mkopo kutoka kwa Korea Kusini na kutoa sehemu ya bahari na madini

VoA: Tanzania imepokea mkopo kutoka kwa Korea Kusini na kutoa sehemu ya bahari na madini

Tanzania na Ethiopia zimesaini mikataba kadhaa na Korea Kusini kwa ajili ya kupata mikopo ya mabilioni ya dola kwa ajili ya maendeleo.

Mikopo hiyo itaiwezesha Korea Kusini kupata fursa ya kuchimba madini muhimu katika nchi za Afrika.

Korea Kusini imeandaa kongamano na viongozi 30 wa nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania na Ethiopia.

Kongamano linafanyika wiki hii

Tanzaia imesema kwamba itakopa dola bilioni 2.5 kutoka kwa Korea Kusini katika muda wa miaka mitano ijayo. Mkopo huo utalipwa katika muda wa miaka 5.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan vile vile amesaini mkataba utakaoiruhusu Korea Kusini kutumia bahari yake na madini yanayotumika katika teknolojia ya nishati safi kama Nickel, Lithium na Graphite.

Ethiopia nayo imesaini mkopo wa dola bilioni 1 utakaolipwa katika kipindi cha miaka minne kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu, sayansi na teknolojia, afya na maendeleo ya mijini.

PIA SOMA
- Ziara ya Rais Samia Korea Kusini atasaini Mkopo wa Tsh. Trilioni 6.51

- Prof. Kitila Mkumbo akanusha masharti ya Mkopo wa Korea Kusini

Voice of America
Mitano tena
 
BIASHARA NI WIN WIN SITUATION.KWA HIYO HAKUNA CHA AJABU HAPO
MKOPO NAFUU,CHIMBA ZAHABU KWA MKATABA MAALUM UTAPATA NAMI NITAPATA.
 
Back
Top Bottom