VoA watolea ufafanuzi taarifa ya Masharti ya Mkopo wa Korea Kusini kwa Tanzania

VoA watolea ufafanuzi taarifa ya Masharti ya Mkopo wa Korea Kusini kwa Tanzania

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Siku moja baada ya kutoa taarifa inayoeleza masharti ya mkopo ambao Tanzania imeupokea kutoka Korea Kusini hivi karibuni (Soma hapa). Shiriki la Habari la Sauti ya Marekani (VoA) limeibuka na kutafuta ufafanuzi wa kina wa taarifa ya mkopo huo kutoka Serikalini. Habari hiyo inaeleza:


Serikali ya Tanzania imetolea ufafanuzi juu ya Mkopo waliopokea kutoka Korea Kusini ulioambatana na makubaliano ya ushirikiano katika Sekta ya Uvuvi pamoja na madini huku wachumi nchini wakiitaka Serikali kujenga utaratibu wa kutoa taarifa za kitaalamu Kabla ya kuingia kwenye Mikopo. Kueleza manufaa yatakayopatikana kutokana na Mikopo hiyo.

Mwandishi wa VoA anaripoti kuwa, kwa mujibu wa Msemaji wa Serikali Mobhare Matinyi amethibitisha Tanzania kuingia Mkataba na Korea Kusini, utakayoiwezesha Tanzania kupokea kiasi cha Dola za Kimarekani Bilioni 2.5 kwa Kipindi Cha Miaka mitano kuanzia 2024 mpaka 2028. Matinyi amesema kuwa Mkopo huo utaanza kulipwa baada ya miaka 25 na utalipwa kwa kipindi Cha Miaka 40.

Mkopo huo unatarajiwa kuwa wenye riba nafuu ya asilimia 0.01. Katika habari hiyo Msemaji wa Serikali ya Tanzania Mobhare Matinyi amesikika akisema

Mkopo huu utaanza kulipwa baada ya miaka 25 yaani ukifika mwaka wa 26 baada ya kuwa umemaliza kutolewa 2028. Tutapewa Kipindi Cha Miaka 40 kuulipa. Riba ya Mkopo huu ni 0.01%.


Tanzania kushirikiana na Korea kusini kujenga bandari ya uvuvi Bagamoyo

Aidha katika taarifa hiyo, anasikika Msemaji wa Serikali akisema hati za makubaliano zinajumuisha ushirikiano katika uchumi wa bluu, ikiwemo masuala ya Uvuvi na utafiti katika masuala ya madini ya kimkakati yakiwemo lithium na grafti. Makubaliano hayo pia yanatarajiwa kujumuisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo, mradibutakaogharimu Dola za Kimarekani milioni 156.5 ikiwa ni Moja ya sehemu ya mradi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ikishirikiana na Jamhuri ya Korea.

Hata hivyo Dkt. Bravious Kahyoza ambaye ni mchambuzi wa masuala ya uchumi amesema ni muhimu serikali kuweka utaratibu wa kufanya uchambuzi yakinifu kabla ya kuingia kwenye mikopo kuonyesha namna ambavyo taifa litakwenda kunufaika na mikopo hiyo.

“Serikali ni muhimu kuwa na utaratibu wa kufanya uchambuzi yakinifu na kuonyesha ni kitu gani kinakwenda kutokea, ni kwamba serikali ifanye uchanganuzi makini wa kuonyesha ni kitu gani tunakwenda kukifanya na kitakwenda kutoa matokeo gani kwa umma.” Amesema Kahyoza.

Matinyi amemalizia kwa kusisitiza mkopo huo ni mkopo nafuu na hauna mashariti yoyote yanayohusisha kutoa sehemu ya bahari na madini.

PIA SOMA
- Prof. Kitila Mkumbo akanusha masharti ya Mkopo wa Korea Kusini. Asema utalipwa kwa miaka 40

- VoA: Tanzania imepokea mkopo kutoka kwa Korea Kusini na kutoa sehemu ya bahari na madini

- Ziara ya Rais Samia Korea Kusini atasaini Mkopo wa Tsh. Trilioni 6.51

- Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi azungumza na waandishi wa habari kufafanua kuhusu Mkopo wa Korea Kusini
 
VOA hawajakanusha, wala hawajafafanua taarifa yao ya awali. wamereport tu taarifa kwa upande wa serikali ya Tanzania iliyotolewa leo.

Kunatofauti kati ya kutolea ufafanuzi na ku-report taarifa.
 
WATANZANIA TUSIPOTOSHWE KUHUSU HATI ZA MAKUBALIANO KATI YA TANZANIA NA KOREA KUSINI

Na Amosi Richard

Hivi karibuni baada ya Mhe.Rais.Dkt. Samia Suluhu Hassan Pamoja na Ujumbe wake kuwasili nchini Korea Kusini kwa ajili ya Ziara Rasmi na ya Kikazi na kusaini hati za makubaliano kati ya Tanzania na Korea zitakazoiwezesha Tanzania Kupata Mkopo wenye Masharti nafuu wa shilingi trilioni 6.8 kumetokea wapotoshaji kuanza kusema mambo ya uongo wakitaja kuwepo masharti yanayohusu kuuzwa kwa Madini na Bahari.

Ukweli ni kwamba hakuna masharti ya aina hiyo na mkataba ni Sehemu ya 2 (MOU)² na tamko la Pamoja la kunzisha Mkataba wa ushirikiano wa Uchumi (EPA) kwa Miaka Mitano (5) ijayo ambapo mkataba huu utaiwezesha nchi yetu Kupata Mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi trilioni 6.8 kuanzia 2024-2028 ambayo inakwenda kwenye Miundombinu ya Maendeleo kama ilivyoelezwa na Taarifa Rasmi ya Ikulu na Mkopo huu una riba nafuu ya 0.01% na utaanza kulipwa baada ya miaka 26 baada ya kukabidhiwa pia utalipwa ndani ya kipindi Cha miaka 40 na sio Mitano kama wanavyopotosha.

Aidha tutambue kuwa katika ziara ya Mheshimiwa Rais.Dkt. Samia Suluhu Hassan Nchini Korea Tanzania haijasaini Mkataba wowote na Jamhuri ya Korea unaohusu Tanzania kupeana Bahari wala Madini kwa nchi ya Korea bali alishuhudia utiwaji saini wa Hati ya Maelewano (Memorandum of Understanding-MOU) mbili za Ushirikiano katika sekta za Uchumi wa Bluu na Madini ya Kimkakati.

Tusikubali kupotoshwa na wanaharakati na Wapinzani wasioitakia mema nchi yetu kuhusu madini ya kimkakati, Tukumbuke kuwa Serikali kwa kipindi kirefu imekuwa ikitafuta wawekezaji watakaowekeza katika utafiti, uchimbaji na uongezaji thamani wa madini ya kimkakati nchini.

Pia Wapotoshaji wanasema kuwa Tanzania imeuza Bahari, La hasha ukweli ni kwamba Serikali imesaini Mkataba wa ushirikiano katika Uchumi wa Buluu ambao unalenga kuboresha teknolojia ya uvuvi, kujenga bandari za uvuvi na viwanda vya kuchakata Samaki na si vinginevyo.

Mkopo huu una faida nyingi kwa Taifa letu kwani unakwenda kuchochea ukuaji wa Maendeleo, Ukamilishaji na Uanzishwaji wa Miradi, Kuboresha huduma za Kijamii kama Afya, Elimu Maji ,Umeme nk, Uzalishaji wa Ajira, lakini pia kuimarisha Mahusiano ya Tanzania Kimataifa.

Watanzania tuwe macho na tumuunge Mkono Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Jitihada zake za kuleta Maendeleo katika Taifa letu na kamwe tusikubali akatishwe Tamaa na Watu wasioitakia mema nchi yetu. Wapinzani na Wanaharakati katika nchi yetu hawajawaji furahishwa na Kazi nzuri zinazofanywa katika nchi yetu kwani zinawakosesha ajenda sasa wamebaki kupotosha kwenye kila jema katika nchi yetu, TUKAE NAO MBALI

=============
============
 
Kama kwenye ziara yenyewe yupo na wasanii unategemea kuna la maana hapo.
1717505434222.jpg
 
kuboresha teknolojia ya uvuvi, kujenga bandari za uvuvi na viwanda vya kuchakata Samaki na si vinginevyo.
Madogo waliosomea Uvuvi wapewe kipaumbele sio wanawekana wekana wenyewe tu km kwenye HIZO Safari zao wanachomekana chomekana tu Q.umalamake ZAO wasengerema, madogo wamesomea Uvuvi wanasota tu mtaani HUKU trillion 6.5 mkazifanyie usenge usenge wa kuchomekana chomekana
 
Back
Top Bottom