Naenda kwenye mada moja kwa moja!
Hawa jamaa ni matapeli na kama umejiunga na hii kitu uwe makini unaweza toa hela na badae usilipwe kama yaliyomkuta mzee wangu.
Moja hamna mkataba wa maandishi kati yako na wao. Hii itakufanya wewe kushindwa kupeleka malalamiko yako mbele ya sheria pale wanapokataa kukulipa mazungumzo yote mnafanya kwa mdomo na makubaliano ni kwa mdomo. Serikali tunaomba muungilie kati huu mfuko umekaa kitapeli kuanzia hapo.
Mzee wangu kalazwa week mbili hosptali kubwa shida ya presha na sukari. Baada ya kutoka movie ikaanza hapo. Kwenda kwenye ofisi zao kila mtu anamtupia mwenzake zile karatasi. Jamaa wakaniambia wao wanalipa siku 5 za kulazwa na sio siku zote. Nikawaambia wakati mzee anajiunga mlisema bima yenu ni siku 30 kwa mwaka mnatoa elfu 40 leo hii siku tano. Wakasema akuelewa ila wao wanatoa siku 5.
Nikasema sawa baada ya hapo wakasema mzee inahitajika risiti ya EFD machine nikawaambia mzee amuoni anatumia bima ya Jubilee mnataka tena risiti ya nini? Form hizo hapo za bima kuonesha kalazwa risiti serikali inampa Jubilee sio mimi. Hapo wakatupiana mzigo wakasema kesi yako fanya contacts mwenyewe na watu wa vodabima kwa whatsap nikapewa namba 0767984688. Tukawatumia zile documents ikapita siku nzima kimya namaanisha 24hrs. Nikatuma msg whatsap kuwa mbona hamjibu kitu.
Nikaona isiwe shida nikapiga namba 100 na kuongea nao nikaongea na mtoa huduma nikamwambia sijibiwi whatsap akasema utajibiwa.
Baada ya mda msg ikaingia kwa mzee tuma vielelezo vya kusema ulilazwa amekoti msg ile niliyosema mbona hamjibu kitu. Nikawajibu vielelezo hivo hapo juu. Nikaforward tena. Wakadai hamna report ya daktari nikawaambia someni vizuri hiyo form ya kuruhusiwa kutoka ina short history ya mgonjwa na maradhi yake.
Wakadai wao wanataka report ya Dr. Tukawaambia hatuna. Wakasema watafanyia kazi. Jana wakampigia mzee simu nakumwambia Dr. Wao kaangalia hayo maradhi ni maradhi sugu, wao bima yao hailipi magonjwa sugu. Inalipia magonjwa haya kama malaria, typhod na mengine ila magonjwa sugu hawalipi. Mzee akasema mbona hamkusema hivi toka mwanzo wakasema hakusikia vizuri ila wao hawalipi magonjwa sugu, mzee akawaambia naombeni mnitoe kwenye huduma yenu dk si nyingi msg akapewa ameondolewa kwenye huduma.
Nakuandikia wewe unaelipia bima hii kwa kukatwa m pesa uwe makini sana na hawa watu. Hakikisha una makubaliano nao kwa maandishi. Nilipatwa na hasira nikamwambia mwanasheria mshikaji wangu nataka kuwapeleka mahakamani akasema hamna ushaidi hapo ni kupoteza mda tu hamna kitu kinachomlinda mzee kwa document ya aina yeyote.