Vodacom kuanza kuuza hisa Machi 9

Vodacom kuanza kuuza hisa Machi 9

Mkuu mimi binafsi naona ni opportunity nzuri sana kuwekeza kwenye Telecoms. nilitumiwa prospectus yao nikaisoma ipo vizuri wanatengeneza profit baada ya kodi ni bil. 29. ingawa imeshuka kutoka bil 32 mwaka 2015 na bil 128 mwaka 2014. hii inatokana na competition kuwa kubwa lkn wanaongoza kwenye market share. na pia ukiongelea Vodacom unaongelea global kila mtu anaitolea macho. Dividend ni 50% profit itakayopatikana kwa mwaka. Najua wengi wetu ni speculators na tunategemea price appreciation ili kufaidika. Vodacom haitofilisika leo wala kesho na kama opportunity kama hii ikipatikana ya ku participate katika IPO sio ya kuacha wakuu.
Well Said.
 
Jamani kuuliza sio ujinga....natanguliza hili neno kwa sababu nataka kuelimishwa juu ya hili neno HISA linamaanisha nini na mchanganuo wake ukoje?..nashukuru
 
Jamani kuuliza sio ujinga....natanguliza hili neno kwa sababu nataka kuelimishwa juu ya hili neno HISA linamaanisha nini na mchanganuo wake ukoje?..nashukuru

1. Hisa ni nini?

Hisa ni sehemu ya umiliki wa kampuni. Hivyo hisa moja inawakilisha asilimia ndogo ya umiliki katika kampuni. Kama kampuni ina hisa milioni moja na mwekezaji anamiliki hisa 10,000, mwekezaji huyu anamiliki 1% ya kampuni. Mwekezaji anayenunua hisa basi ananunua haki ya kumiliki kampuni. Stahili za mwenye hisa ni pamoja na kushiriki katika kutoa maamuzi ya kampuni katika mkutano mkuu wa wanahisa na kupata gawio litokanalo na faida. Ana haki pia ya kuuza hisa zake kwa faida pale ambapo kuna ongezeko la thamani ya hisa.

2. Gawio ni nini?

Gawio ni malipo yanayofanywa na kampuni kwa wanahisa kutokana na faida ya kampuni. Malipo haya yanapendekezwa na wakurugenzi na kuidhinishwa na mkutano mkuu wa wanahisa. Gawio linaweza kulipwa kutokana na faida ya mwaka husika au malimbikizo ya faida za nyuma. Gawio linaweza kulipwa kwa fedha taslim au kwa kuwaongezea hisa wanahisa.

Pia click 'search box' kwenye hii forum halafu uki- type neno 'hisa' utapata maelezo kuhusu hisa kwenye threads nyingi zilizoandikwa hapo awali.
 
Unaruhusiwa cha msingi utajaza form tofauti kulingana na kiasi ulicholipia

Asante Babu wa Loliondo kwa kutujuza – your contribution is really appreciated!

Swali langu ni kuhusu article hii:
Tanzania: ... Bank, Broker Partner to Help Informal Sector Buy Vodacom Shares
Tanzania: ... Bank, Broker Partner to Help Informal Sector Buy Vodacom Shares

COVENANT Bank and Zan Securities have partnered in supporting the Tanzanians in informal sector to buy recently floated shares of Vodacom Tanzania.
At the weekend, the Covenant Bank and Zan Securities announced their partnership that is aimed at enabling entrepreneurs in the informal sector to own the company through buying of shares.
The Managing Director of the Bank, Ms Sabetha Mwambenja, said under the partnership, the Covenant Bank would act as a bridge connecting entrepreneurs with the Zan Securities through which they would buy the shares. Ms Mwambenja said the target would be micro entrepreneurs organized in their groups such as cooperatives or Village Community Banks (VICOBA).

Swali langu ni hili:
- Je hawa Vodacom wameshindwa kuziuza hizi 25% share kwa investors wa kawaida mpaka wanaanza kusaka investors kutoka VICOBA?
Naomba jibu iwapo unafahamu what might have happened.
 
Sijui kuna nini
nimeenda Crdb wanasema Vodacom hisa hawajui lolote

nasikia ni bank moja tu NBC ndo watauza

sijaelewa kuna nini?

Halafu kumbe market share ya voda ni 31 tu asilimia?
na Tigo 29? tofauti ni asilimia 2 tu?

Voda si waliwahi kushika soko zaidi ya asilimia 50?

Naona kama hizi hisa zina longo longo hivi...
Hapana Mzee pitia Ktk mawakala Wao km orbit security Wapo floor Ya kwanza diamond jubilee.wao watakupa Namba za banki ukalipie.kuna Bank za Crdb.nmb.nbc.halafu unapeleka slip Kwa hao mawakala then utakuwa umemaliza Kazi unasubiri vikao Na. Mikutano yao Na. Dividend km itakuwepo utapata
Kampuni ya Vodacom Tanzania kupitia Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) itaanza kuuza hisa zake milioni 560 kwa thamani ya Shilingi 850 kila hisa. Mauzo yataanza tarehe 09.03.2017 na kufungwa tarehe 19.04.2017.

======

YAWAPIGA MSASA MAWAKALA WATAKAOKUSANYA FEDHA ZA HISA

Mawakala wa kuuza hisa za Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom TanzaniaPLC, wamepatiwa mafunzo elekezi ya siku moja yaliyokuwa na lengo lakuwaelimisha jinsi ya kukusanya fedha wakati wa zoezi la kuuza hisa zakampuni hiyo litakapoanza hivi karibuni tukio ambalo limekuwa likisubiriwakwa hamu kubwa na watanzania walio wengi.

View attachment 477950
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao akifafanua jambo kwa mawakala (hawapo pichani )wakati alipokuwa akitoa mafunzo elekezi ya siku moja jijini Dar es Salaam leo juu ya ukusanyaji wa fedha wakati wa zoezi la kuuza hisa za kampuni hiyo litakaloanza hivi karibuni.

Semina hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Mlimani City ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Ian Ferrao alisema “Tunawashukuru kwa ushirikiano wenu tangia tulipoanza mchakato wa maombi ya kuuza hisa kwa umma hadi kufkia sasa ambapo tayari tumepata kibali cha kutekeleza zoezi hili kutoka serikali kupitia Mamlaka ya Dhamana Masoko na Mitaji (CMSA) na mkiwa wabia wetu katika mchakato huu tumewaita kwa ajili ya kubadilishana mawazo jinsi tutakavyofanikisha matarajio yetu tuliyokusudia na kuwa tayari kwa kazi iliyosubiliwa kwa muda mrefu”.

Ferrao alieleza kuwa Vodacom inatarajia kuuza asilimia 25% ya hisa zake kwa umma zenye thamani ya shilingi Bilioni 476/-na kila hisa itauzwa kwa shilingi 850/-

Vodacom Tanzania PLC,imekuwa ya kwanza kutekeleza sheria ya Electroniki na Mawasiliano ya Posta (EPOCA) na sheria ya fedha ya mwaka 2016 inayoyataka makampuni kumilikisha asilimia 25% ya hisa zake kwa umma kupitia Soko la Hisa la Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Ferrao, wananchi wataweza kununua hisa za zao katika matawi ya Benki ya NBC na mawakala wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) waliopo nchini kote.

Wakati zoezi la uuzaji hisa za Vodacom linatarajiwa kuanza rasmi hivi karibuni,wawekezaji na wananchi wamekuwa wakisubiri kwa shauku kubwa ambapo wamekuwa wakifuatilia kwa karibu jinsi zoezi hili linavyoendelea ili waweze kujipatia fursa ya kumiliki hisa katika kampuni kinara ya mawasiliano nchini.
View attachment 477951

View attachment 477952
 
Tena ukisoma vizuri hio tofaut ya faida ilisababishwa na hasara kwenye kampuni yake ya minara Helios Towers ambayo wameamua kuuza hisa zao na kuachana nayo,vinginevyo ni uwekezaji mzuri sana,tukizubaa tutakuja sikia baadae akina Manji ndio wana hisa za kutosha huko na kama kawaida yetu tutalalamika kana kwamba tulikatazwa kuwekeza wakati fursa tulipewa tukaipuuzia.
ngoja nikanunue kwanza hisa za laki nne halafu niangalie upepo kwanza.
 
Wadau wa Jf kuna fursa katika kampuni inayoitwa Bitco International ...
kampuni hii inahusika na investment ya coin iitwayo Bitcoin ambapo utainvest hela yako na utapata return ya 3% kila siku kwa muda wa siku 50.Bitcoin ni coin maarufu sana kwenye mataifa ya ulaya na America kwa muda mrefu sasa na pia imeanza kutumika katika matumizi ya kawaida kama fedha nyingine huko kwa wenzetu.
hii fursa ni real na na watu wanaendesha maisha yao kupitia bitco international.Kwa hapa kwetu Tanzania fursa hii bado ngeni ,ila wachache walioichangamkia wananufaika ikiwamo na mimi.

Uthubutu ni kitu muhimu sana katika mafanikio ya mwanadamu,nawashauri msikubali hii fursa iwapite .

kwa yeyote ambaye atahitaji maelezo ya kina na kujiunga anitafute kwa namba hii 0712 799747 au whatsapp kwa namba hiyo hiyo ,mimi nipo Dar.
 
1.Tuelezee kwa kina unufaikaje na huo uwekezaji

2.kwanini tukupigie simu wewe na usituelekeze kwa mawakala wanaotambulika Je kama ni tapeli ?(samahani lakini)

3.Je mikioani kuna matawi yake (kwasasa niko mwanza kikazi)

4.Kiasi cha kuanzia ni shillingi ngapi ?
 
kiwacho cha chini cha hisa ni ngap natakakujaribu hisa kama 10 - 50 nionje utamu wake
 
samahanini kwa kuchelewa kujibu ,niliweka namba ya simu ili iwe rahisi kuwasiliana as u know response ya kwenye jamii forums ni tofauti na text ya kawaida au whatsapp ..kwenye text na whatsapp ni rahisi kufanya mawasiliano ya haraka kuliko huku.
Hii ni international company kwa Tanzania haina matawi sehemu yoyote kwa sasa ila ina mawakala wa kuuza Bitcoin ambazo ndio utaziwekeza.Kuna baadhi ya nchi kama Naigeria na kenya wameshaanza kuanzisha na charity program ,so ni kampuni real na hakuna utapeli wowote.
faida za uwekezaji ndio kama hivyo nilivyosema kwamba unapata return ya 3% kwa siku kwa muda wa siku 50 kwa kile kiwango ulichowekeza.

Ningependelea zaidi kwa yeyote anayehitaji maelezo ya ziada anitafute kwa namba niliyoiweka either whatsapp, text au call

karibuni sana
 
Si ukaanzishe uzi tofauti
 
Back
Top Bottom