Vodacom kubadili vifurushi kuanzia jumatatu 16/08/2021

Vodacom kubadili vifurushi kuanzia jumatatu 16/08/2021

Name:
Number: Vodacom
Content:
Habari, Tunakufahamisha kutakuwa na mabadilikokatika vifurushi vyetu tarehe 16/08/21. Endelea kufurahia huduma bora kutoka Vodacom. Vigezo kuzingatiwa
Time: 14/08/2021 11:08:04
 
Hlo ilikuwa wakat wa tamko la waziri vifurushi vikabadilishwa tukapga kelele wakasema vrudi kama zaman
Vilirudishwa bei ya zamani lakini walikuwa na mchakato wa kufanya mabadiliko ya bei na sasa mchakato ndio umekamilika ndio tusubiri tuone bei zitakavyokuwa
 
Naona bado wanatutafutia au watutia hasira tupige kura za maruhani uchaguzi ujao.
 
Mimi Halotel wamenitumia hio msg nikapiga ili kuuliza ni mabadiliko gani,

Customer care wao alivyopokea kaniambia subiri kidogo nikishuka nipo kwenye boda boda.
Du! hii Kali sasa,[emoji38][emoji38],yaani mi nilipiga wiki iliyopita TTCL huduma kwa wateja yaani alivyopokea yule mama sijui Dada anaongea utadhani kajifunika blanket,anaongea kwa uchovu, nikahisi labda yupo jikoni maana nasikia kama mtu anaosha vyombo,ishu yenyewe ilikuwa ndogo tu nilikwangua vocha vibaya ikawa haionekani,nikaambiwa subiri saa 24,utajulishwa mpaka leo hakuna lolote ni wiki sasa,vocha yenyewe niliamua kutupa tu
 
Nimepokea sms ya Vodacom asubuhi ikinijulisha kuwa kuanzia 16/08/2021kutakuwa na mabadiliko ya vifurushi. Mpaka sasa sijajua ni Vodacom pekee au na mitandao mingine nao watapandisha.

Sms hiyo haijaweka wazi kama vifurushi vitapanda au vitapungua lakini kwa fikra zangu naona vifurushi vitapanda hasa upande wa data/internet!

Unategemea nini kwenye mabadiliko ya vifurushi vya Vodacom?

View attachment 1891714
Siku hizi nitakuwa natazama zangu Ertugrul tu na mama watoto. Simu nitaigusa kukumbusha wadeni wangu tu basi.
 
Ha
Hello, Please be informed that we will review our bundles on 16/08/2021. Continue to enjoy quality services from Vodacom. Terms and Conditions apply.

Nipo Halotel hii imebaki tu pambo kwenye kimeo changu
Halotel nao tayar mkuu washatuma sms 😂😂😂😂
 
Hawa jamaa tayari wameshapandisha sio kwamba wanasubiri hio tarehe 16/08/2021.nadhani hio meseji ni geresha tu hata mimi walinitumia lakini nimeangalia muda si mrefu vifurushi vimeshapanda.

Kwenya menu ya 'yakwako tu' nilikuwa naweza kupata GB 1 kwa wiki na dk 150 mitandao yote kwa 1,500 ila leo nimekuta haipo hio.

Sasa hivi imepanda ni shs 2,000 halafu dk za mitandao mingine ni 15 tu,hizo 150 ni voda-voda.

Halafu kuna mtu anasema watanzania hawajakataa tozo eti
IMG_20210814_195321.jpg
 
Watapandisha maana meseji zimekua nyingi sana ingekua kuna punguzo ujumbe wa furaha ungeonekana...
 
Nimepokea sms ya Vodacom asubuhi ikinijulisha kuwa kuanzia 16/08/2021kutakuwa na mabadiliko ya vifurushi. Mpaka sasa sijajua ni Vodacom pekee au na mitandao mingine nao watapandisha.

Sms hiyo haijaweka wazi kama vifurushi vitapanda au vitapungua lakini kwa fikra zangu naona vifurushi vitapanda hasa upande wa data/internet!

Unategemea nini kwenye mabadiliko ya vifurushi vya Vodacom?

View attachment 1891714
HATA HALOTEL WAMETOA KITANGAZO HICHO!
 
Hii ndio pesa ya kununulia Land Cruiser L300, maana tozo itajenga barabara bado ya mafuta na spea.
 
Hivi hakuna kipengele cha sheria za kimtandao kwa sisi watumiaji kuweza kuyashitaki haya makampuni? hasa pale yanapoamua kuja na mabadiliko pasipo makubaliano na mtumiaji ? Au tuseme ni maagizo toka juu?

Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom