VODACOM naomba mnisaidie kwanini Mb zangu zinakwisha Haraka pasipo matumizi utafikiri kuna jini linakula?

Sajili line ya halotel buku 2 GB 2.5 wiki itakusaidia
Mimi nawekaga mb nyingi sana kwenye voda.na niliweka mb za hela ndogo baada ya kuona hali hiyo siyo ya kawaida .hivyo nikataka nione nini shida .ndio nikathibitisha ya kuwa ulaji wa mb umebadilika ghafla na siyo wa kaimwaida na ni kama jini mla mb limerushiwa kwenye simu yangu.
 
Je simu yako inakuwezesha kudhibiti background apps zisitumie data?
 
Achana nao hao kina Dr Restart wanaosema unajiungaga za jero
 

Sio MB tu; bali hata muda wa Maongezi. Zile dakika mtu unazonunua - ukifananisha na muda ulioongea - unakuta haziendani kabisa. Mfano unanunua Dakika 460 kwa Tshs. 3,000. Dakika 460 ukigawa kwa 60; hayo ni masaa saba (7) na dakika 40 za kuongea tu. Utashangaa umeongea hata saa halijaisha, unakuta unaambiwa kifurushi kimeisha. Inaonekana kuna namna tunaibiwa muda wetu.
 
Unajua simu unayotumia app ngapi zina transmitt na ku receive data?
Unapoweka bundle tambua ni zaidi ya app moja zikula bundle si jf peke yake. Funga hizo app or zitoe kabisa

Halaf kwa miaka hii bundle la 500 ni kidogo sana, ccm hawawezeshi na kazi unayoifanya?
 
Ningekuwa najiunga bando la jero nisingekuwa nakuwepo humu jukwaani muda wote .lakini nadunda humu jukwaani kwa kuwa naweka bando la kutosha kuniwezesha kuwepo humu mwaka hadi mwaka na kujaa kama pishi la mchele.
Tatizo wapambe wa humu kama Chaliifrancisco wanakuchukulia poa wakati wewe ni mkulima na kilimo kinalipa
 
Nadhani kuna tatizo siyo wewe tu kunawati mtandao unakataa unaangalia hizo mb ambazo unajua zipo zinakuwa hazipo Kesho yake zipo na mtandao umerudi hahaha 😂
 
Nchi kila kitu uwizi uwizi tu lucas, lakini tunaishi naoo

Ova
 
Sasa mtu kama wewe unanunua bando hadi la 500 kweli, halafu ukitoka hapo unasema Mama anatimiza, Mama anatosha.

Wenzio kina Abdul wanaishi Dubai kwa hiyo kodi yako ya 500 huku wewe unakazana Mama ametimiza Mama Anatosha. Tuliwaambia CCM’nyie ni mabogus na ni vijana hovyo na washisha, kijana kama wewe una future nzuri kwenye maisha yako lakini unakazana Mama anatosha Mama anatimiza huku deep down unaungua na kuja kulia lia na bando za Mia tano JF, Ujinga ni dhambi isiyosameheka.

Tulisema Mama anaharibu nyumba ambayo na nyie mpo. Endeleeni Mama Anatimiza mama Anatosha na publish zenu za vibanda vilivyojengwa kama vituo vya Afya kwa Bil 500 na TRENI YENU ya escape from sabibo ye SGR iliyokula tril of TZS huku wewe unalialia na bando za 500.

Ujinga ni mzigo na ni dhambi isiyosameheka. Mama ameweza Mama ametimiza , Mama anatosha by Lucas Mwashambwa
 
Tafuta namna ya kujisaidia mwenyewe, niliwahi poteza GB kuwapigia wananiambia nimeacha data on na laini ilikuwa kwenye kitochi, ndio nimeunga niweke kwenye modem afu naambiwa nineacha data on wakati hata sijaitoa kwenye kitochi.
 
Sasa muda wote una andika mapambio humu kuhusu chama cha majizi una tegemea Mb zibaki vile vile?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…