VODACOM naomba mnisaidie kwanini Mb zangu zinakwisha Haraka pasipo matumizi utafikiri kuna jini linakula?

VODACOM naomba mnisaidie kwanini Mb zangu zinakwisha Haraka pasipo matumizi utafikiri kuna jini linakula?

Nimeeleza wazi kuwa sijiungagi kifurushi cha jero bali nilifanya hivyo katika kutaka kujiridhisha na kutafuta majibu ya sababu ya ulaji na uishaiji wa kasi wa mb ambao haukuwepo swali sasa wewe unaweza vipi kununua bando la bei kubwa wakati unaona kuna hali isiyo ya kawaida imetokea?
Sio kweli hizo ndio bando zako. Kwanza wewe ulitakiwa kuwa kwenye free package ya internet . Kumbe hata hawakupi free package , yaani vijana watanzania ni wahovyo sana. Abdul anaishi Dubai kwa kodi zetu kumbe wewe pambio za hapa JF unajilipia bundle , kijana kama wewe ni HASARA kwenye taifa na mwisho wa siku mnaacha vizaz masikini kwenye nchi yenye mfumo mbovu, huduma za elim mbovu, huduma za miundo mbinu mbovu, bima ya afya mbovu na watoto zao wanaenda kupata elimu nje, wako wanaenda hapo Kayumba. Watoto wako watakulaani wakija kuona post zako , yaani uongo unaupaka perfume.

Lucas mwashambwa kumbe haupo hata kwenye payrol ya vocha dah . CCM ina elites , nyie subirini kofia na fulan za oct 25

Vijana wa shisha
 
Yaaani kelele zote na pambio zako unakuja kulia lia Mb 234 wakati huo ume jiunga kifurushi cha tsh 500/= (Mb 246)
Mzee iko chama unacho kipambania kila siku umu hakithamin juhudi zako hata bundle la tsh 15,000/= mwezi wameshindwa kukuungia??
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mimi ni mtumiaji na mteja wa miaka mingi wa mtandao wa voda ,lakini Haijawahi kutokea na sijawahi kushuhudia hali hii katika simu yangu ya ulaji wa mb utafikiri kuna jini limepiga kambi kula mb zangu. Hali hii imejitokeza tangia jana jioni ambapo nilikuwa na mb mia mbili na 34 lakini ghafla nikashangaa naletewa sms kuwa zimekwisha.

Nilipigwa na mshangao mkubwa sana.baadaye nikasema ngoja nijaribu niweke mb za mia tano.nikaweka nikapewa mb 246 cha kushangaza nikaingia jamii forum na kukaa kama dakika tatu au nne hivi bila kufungua video ya aina yoyote ile.lakini nikaletewa sms kuwa zimebaki mb 61.

Lakini cha kushangaza baada kama tena ya dakika 2 hivi nikaletewa sms kuwa kifurushi chako cha JKU kimekwisha.Nilishangaa sana na kusikitika sana hali hiyo.

Nimepiga sana huduma kwa wateja bila kupata msaada wa aina yoyote ile,kwa kuwa sikupata nafasi ya kuongea na wahudumu wa voda zaidi ya kupewa maelekezo ya kujihudumia mwenyewe.

Sasa muda huu tena nimejiunga bando la mia tano na kupewa mb 246 hivi lakini cha kushangaza nimeingia tu JF na kukaa kama dakika mbili bila kufungua video au kuandika chochote wala kusoma habari hata moja zaidi ya kuangalia nyuzi tu.nikasema ngoja nikaangalie salio,nikakuta tena salio eti ni mb 110 .

Wakati hali hiyo haijawahi kutokea. Sasa najuwa humu jukwaani wapo voda nataka kujuwa shida ni nini?
We mwashambwa lazima unyooke kwanza wametega kwako tu usiwe online. Any way hili swala la mbs ni changamoto mtandao wa voda wamezidi tutawakimbia sio mda aisee
 
Soma uelewe vyema.mimi sininuagi bando la jero bali nilinunua katika kufanya uchunguzi baada ya kuona mabadiliko ya ghafla ya uishaiji wa bando.
Sasa hakuna bundle linapotea bila matumizi
1. Speed ya internet inachangia sana kumaliza bundle haraka..the higher the speed the more consumption of bundle...ukiweza shusha mnara wa internet usome 3g au 4g kama unasoma 5g

2. Weka off auto update ya apps zako...endapo zinajiupdate lazima zinakula mb za kutosha...hapa pia unaweza weka off auto download ya pics na video kwenye whatsapp na apps nyingine

3. Cheki kama Hotspot ipo on...means unaweza ukawa unatumia bundle lako na kifaa kingine kwa kujua au kutokujua

4 kama kuna apps hutumii weka notification off..pia notifications kama za YouTube na apps nyingine weka off kama hauzitumii kwa wakati huo maana zinapokuletea notifications zinatumia bundle lako

Mengine wadau watakuongezea
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mimi ni mtumiaji na mteja wa miaka mingi wa mtandao wa voda ,lakini Haijawahi kutokea na sijawahi kushuhudia hali hii katika simu yangu ya ulaji wa mb utafikiri kuna jini limepiga kambi kula mb zangu. Hali hii imejitokeza tangia jana jioni ambapo nilikuwa na mb mia mbili na 34 lakini ghafla nikashangaa naletewa sms kuwa zimekwisha.

Nilipigwa na mshangao mkubwa sana.baadaye nikasema ngoja nijaribu niweke mb za mia tano.nikaweka nikapewa mb 246 cha kushangaza nikaingia jamii forum na kukaa kama dakika tatu au nne hivi bila kufungua video ya aina yoyote ile.lakini nikaletewa sms kuwa zimebaki mb 61.

Lakini cha kushangaza baada kama tena ya dakika 2 hivi nikaletewa sms kuwa kifurushi chako cha JKU kimekwisha.Nilishangaa sana na kusikitika sana hali hiyo.

Nimepiga sana huduma kwa wateja bila kupata msaada wa aina yoyote ile,kwa kuwa sikupata nafasi ya kuongea na wahudumu wa voda zaidi ya kupewa maelekezo ya kujihudumia mwenyewe.

Sasa muda huu tena nimejiunga bando la mia tano na kupewa mb 246 hivi lakini cha kushangaza nimeingia tu JF na kukaa kama dakika mbili bila kufungua video au kuandika chochote wala kusoma habari hata moja zaidi ya kuangalia nyuzi tu.nikasema ngoja nikaangalie salio,nikakuta tena salio eti ni mb 110 .

Wakati hali hiyo haijawahi kutokea. Sasa najuwa humu jukwaani wapo voda nataka kujuwa shida ni nini?
Wote tutaongea lugha Moja tu,chawa mkubwa wewe na bado
 
Back
Top Bottom