Vodacom Premier League Lipuli FC 1-1 Simba SC, Uwanja wa Samora Mkoani Iringa

Mliopo Dar Simba wakipoteza game hii viboko viwahusu. Hakuna namna. Huyu Mlipili anadhani yuko peke yake humo uwanjani.
 
45' Naam kutoka uwanja wa Samora mkoani Iringa mtanange wa VPL, kati ya Lipuli FC na Simba kwa sasa ni mapumziko ambapo wenyeji wako mbele ya goli moja dhidi ya Simba SC

Lipuli FC 1-0 Simba SC
 
Mtakoma!!
Hahhahah aisee lazma tukome , kusema ukweli huyu kocha toka amekuja Simba imebadika sana, zile 4G sahv shida sana kuzipata. Kwa mtizamo wangu Simba angepewa huyo kocha msaidizi , au Matola
 
Apigwe tu kwa kweli.

Ili ajue Ubingwa haupatikanagi kirahisi.

Labda wabadili mchezo ila wakiendelea kucheza hivi, watapoteza hili game then jpili ijayo itakuwa game tamu sana
 
Labda wabadili mchezo ila wakiendelea kucheza hivi, watapoteza hili game then jpili ijayo itakuwa game tamu sana
Umeonaeeee. Yaani leo hamna cha Kwasi, Okwi wala Adebayo wote wamefichwa lol.

Na Jimapili lazima tuwashangaze.
 
Hahhahah aisee lazma tukome , kusema ukweli huyu kocha toka amekuja Simba imebadika sana, zile 4G sahv shida sana kuzipata. Kwa mtizamo wangu Simba angepewa huyo kocha msaidizi , au Matola
huyo si ndo kocha mwenye CV kubwa Afrika...
 
huyo si ndo kocha mwenye CV kubwa Afrika...
CV gan kubwa, Ndemla alvokuwa onfire msimu huu sahv anasugua benchi, Mzamir kiungo bora kabisa, ukiachana na Mo wote wanasugua et Kapombe ndo kawareplace.
Dah aisee kiungo ya Simba inapwaya balaaaa.
Naona kuna dalili kubwa hawa vijana kwenda Jangwani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…