SaaMbovu
JF-Expert Member
- Oct 8, 2013
- 6,027
- 5,344
Hiyo inaitwa Delaying tactics.Hongereni Simba kuanzia viongozi, wachezaji na benchi la ufundi. Timu imecheza kwa mbinu nzuri ya mipira mirefu kutokana na mazingira ya uwanja na imefanikiwa.
Ugomvi wangu mimi bado ni benchi la ufundi kwa nini hawa hamasishi wachezaji wafunge magoli mengi. Mara nyingi Simba ikishafunga magoli mawili au matatu basi wachezaji wanaridhika wanapunguza kasi na kuanza kucheza "back pass" nyingi na vipasi vifupi fupi. Sisi watazamaji huku kwenye vibanda umiza tumelipa 500 zetu ili tuone magoli hata kama ni 10 - 0 raha yetu ni kushangilia kila goli likiingia sio hizo pasi zenu. Kwa mfano leo tayari Ruvu walikuwa na upungufu wa mchezaji mmoja lakini unaona bado Simba hawapeleki mashambulizi kwenye goli la Ruvu. Baadae tena katolewa mchezaji wa Ruvu bado mambo ni yale yale. Timu kama hizi ukizipata piga goli nyingi waache kuongea ongea. Hebu fikiria kale kagoli kamoja walikokafunga kwa Mkapa walikuwa wanakazungumzia mpaka leo jioni kabla ya mechi na jina walibadilisha kabisa wakaanza kujiita Barcelona ya Bongo.
Ombi langu kwa benchi la ufundi ni kuwa itapendeza zaidi Simba ikichukuwa ubingwa kwa kuweka pia rekodi ya kufunga magoli mengi na raha zaidi ni iwapo pia itatoa mfungaji bora. Kwa hiyo benchi la ufundi lihakikishe kuwa hata kama timu inaongoza kwa goli mbili basi kama uwezekano upo washambuliaji kufunga zaidi basi wasaidiwe ili wafunge zaidi kuliko kucheza pasi na kurudisha mpira nyuma na kuwaacha washambuliaji wamesimama kama watazamaji.
Wanafanya hivyo ili kutotengeneza mazingira ya wachezaji kuumia kwakuwa tayari wanaongoza kwa tofauti nzuri ya magoli. Na mchezo huu akiwepo Nyoni ndio Simba hucheza sana.
Na hii ndio maana unaona Simba wachezaji wengi hawapati majeraha.
Japo nakereka sana kama wewe hapo.