Vodacom Premier League VPL | Ruvu Shooting Vs Simba SC | Uwanja wa CCM Kirumba

Vodacom Premier League VPL | Ruvu Shooting Vs Simba SC | Uwanja wa CCM Kirumba

mkuu naomba unipe ratiba mechi ngapi zimebaki , kuna uwezekano hawa utopolo wakaandika historia ya kutupigia makofi ?
20210517_065229143669.jpg
 
Hawa paka shume walitubahatisha kale kagoli kamoja leo wamekula jeuri yao, Massau Bwire akatafute pakujificha, hilo kombe TFF waanze kulitanguliza Msimbazi taratibu, sasa namtaka uto tu.
Kocha Sven naye aliishiwa mbinu alikuwa na kambinu kamoja tu, sasa akibanwa tu hakuwa na pa kutokea tofauti na huyu.
 
Hivi jamaa huwa ana bifu na kapombe? Maana hii si mara ya kwanza, yani huwa hatuko fair kabisa kwa kapombe.
siyo yeye tu kuna wachezaji waliondoka simba kwa dharau leo wana wivu mkali kuna huyo,humoud wa namungo na banda asiye na team ambaye aliisagia simba kunguni vya kutosha huko south africa ila baada ya ile display ya mechi ya pili wa south wenyewe walijua simba ni team ya aina gani
Nyoso alivunja mkataba simba iliyokuwa na njaa akakimbilia coast union iliyokuwa na udhamini wa bin slum nafikiri aliahidiwa mshahara sijui wa milioni moja kwa hiyo leo wana hasira sana na wachezaji waliowaacha kwenye dhiki simba leo wanakula maisha
 
Hongereni Simba kuanzia viongozi, wachezaji na benchi la ufundi. Timu imecheza kwa mbinu nzuri ya mipira mirefu kutokana na mazingira ya uwanja na imefanikiwa.

Ugomvi wangu mimi bado ni benchi la ufundi kwa nini hawa hamasishi wachezaji wafunge magoli mengi. Mara nyingi Simba ikishafunga magoli mawili au matatu basi wachezaji wanaridhika wanapunguza kasi na kuanza kucheza "back pass" nyingi na vipasi vifupi fupi. Sisi watazamaji huku kwenye vibanda umiza tumelipa 500 zetu ili tuone magoli hata kama ni 10 - 0 raha yetu ni kushangilia kila goli likiingia sio hizo pasi zenu. Kwa mfano leo tayari Ruvu walikuwa na upungufu wa mchezaji mmoja lakini unaona bado Simba hawapeleki mashambulizi kwenye goli la Ruvu. Baadae tena katolewa mchezaji wa Ruvu bado mambo ni yale yale. Timu kama hizi ukizipata piga goli nyingi waache kuongea ongea. Hebu fikiria kale kagoli kamoja walikokafunga kwa Mkapa walikuwa wanakazungumzia mpaka leo jioni kabla ya mechi na jina walibadilisha kabisa wakaanza kujiita Barcelona ya Bongo.

Ombi langu kwa benchi la ufundi ni kuwa itapendeza zaidi Simba ikichukuwa ubingwa kwa kuweka pia rekodi ya kufunga magoli mengi na raha zaidi ni iwapo pia itatoa mfungaji bora. Kwa hiyo benchi la ufundi lihakikishe kuwa hata kama timu inaongoza kwa goli mbili basi kama uwezekano upo washambuliaji kufunga zaidi basi wasaidiwe ili wafunge zaidi kuliko kucheza pasi na kurudisha mpira nyuma na kuwaacha washambuliaji wamesimama kama watazamaji.
 
Back
Top Bottom