Vodacom Premier League 'VPL' Simba SC dhidi ya Mbeya City, Kazi ipo Uwanja wa Uhuru

Vodacom Premier League 'VPL' Simba SC dhidi ya Mbeya City, Kazi ipo Uwanja wa Uhuru

65' Simba SC wamefanya mabadiliko kwa kumtoa Mohemd Hussein nakuingia Gerson Fraga
 
Ajibu anafanyiwa faulo huku mchezaji wa Mbeya City Baraka huku Kapeta akiingia

Inapigwa na Ajibu..Anapigaaaaaa anacheza golikipa wa Mbeya City
 
75' Mbeya City wameamka baada ya kufanya mabadiliko kwa wachezaji wawili, wanacheza kwa kujaribu kupenya lango la Simba

Simba SC 2-0 Mbeya City
 
Shambulizi la Mbeya City linagonga mwamba..Ilikuwa hatari sana..!
 
Anatoka Ajibu na anaingia Deo Kanda..Simba SC
 
Ni free kick kuelekea Simba..Ni eneo hatari sana

Haya sasa anakwenda Mapunda anapigaaaa, anababatiza mabeki wa Simba na kupoteza nafasi ile.
 
87' Goooooooooooooooooooaaal goooal gooal Deo Kanda anaipatia Simba SC bao la nne baada kumlamba chenga golikipa huku mabeki wakiwa wamechelewa kurudi baada kupanda

Simba SC 4-0 Mbeya City
 
Taarifa ziwafikie pale jangwani kwamba tutakutana January
 
90+3' Kuelekea kumalizika kwa mpambano huu wa VPL

Naaaaaaaaaaaaaaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Simba SC imeibuka na ushindi mnono wa mabao manne bila majibu yakiwekwa kimiani na Kagere, Chama, Shiboub na Kanda

Simba SC 4-0 Mbeya City
 
Back
Top Bottom