Vodacom Premier League (VPL) Simba SC vs KMC FC, burudani ya uhakika Uwanja wa Taifa

Vodacom Premier League (VPL) Simba SC vs KMC FC, burudani ya uhakika Uwanja wa Taifa

Emmanuel Mvuyekuleeeee anapiga lakini golikipa Manula anadaka bila wasiwasi

KMC wanajaribu kwa mashambulizi ya kushtukiza lango la Simba
 
40' Nipe nikupe Mkude, Luis, Dilunga kwake Chamaa anapigaaa lakini mlinzi analala na kuokoa

Mabeki wa KMC wapo imara mpaka sasa kuhakikisha hakuna hatari
 
Luis Miquissone anapigaaa, anaunawa na refa anasema hakuna penatiiii

Wakati huo huo Kahata yupo chini baada ya kupata rabsha
 
Bonge moja la match... Kweli Simba ni chuo cha mafunzo,watazame KMC wanavyoupiga mwingi...ndio raha ya kucheza na anayeujua...
 
45+2' kuelekea kuwa mapumziko Uwanja wa Taifa

Kapombeeee kwake Dilunga anarudisha kwake Wawa...Simba wanamiliki

Naaaaaaam Mpira ni mapumziko ambapo timu zimemaliza dakika 45 bila kufungana

VPL, HT: Simba SC 0-0 KMC FC
 
Kipindi pili kimeanza safari ya kuhitimisha 90 za VPL

Hakuna mabadiliko kwa Simba wala KMC
 
Anakwenda Luis Miquissone lakini anazuiliwa, inapigwa ndefu kwake Sadala, kwake Kabundaaaa lakini Wawa anaokoa
 
55' Serge Alain anakwenda langoni mwa Simba, wanapoteza KMC wanaumiliki Simba kwake Mkude anasukuma mbele Chama, Chama, Chamaaaaa anapoteza

Simba SC 0-0 KMC FC
 
Luis Miquissone anafinya anampa Chama, Chamaaa kwake Kapombeeee anapigaa anababatiza

Mchezaji wa KMC yupo chini...
 
Back
Top Bottom