Vodacom sasa watapatapa kutafuta wateja

Vodacom sasa watapatapa kutafuta wateja

Hivi ninavyoandika, line yangu ya Voda imekata network tangu mida ya saa12 jioni imebidi nibadili line natumia mtandao mwingine.
 
Lowasa ndiye aliyeshika mpini hapo jamaa ni wezi sana. Wamerithi kutoka kwa jambazi mama.
 
Hivi ninavyoandika, line yangu ya Voda imekata network tangu mida ya saa12 jioni imebidi nibadili line natumia mtandao mwingine.

Yaani mi kila wakati inakata.. inabidi nifanye tethering... too boring
 
Kwa kweli voda wamenikwaza sana baada ya kuruhusu mtu asiyehusika kuzisoma sms zangu. Imeniuma sana huyo mtu kaniambia everything tena ni sms za personal! Haya si majungu na wala sina ushindani na voda na si mwajiriwa. IMENIUMA SANA SANA SANA!
 
Utakuwa unalipiwa wewe, voda waizi haswa wanakula hela ya kifurushi utadhani mbwa amelamba damu unaweka hela unaambiwa imeisha hata hujatumia, network inasumbua sijawahi kuona voda ni janga kwa kweli
Labda ni promoter, Mkuu
 
Walinisababishia matatizo wala sitaki kuwasikia tena na lain nimechoma moto, mpango mzima zantel part of etisalat
 
Ukitaka kuhakikisha Voda ni WEZI chukua stop watch anza kuongea na simu, then then start stopwatch.ukimaliza kuongea stop it. Kama umeongea dakika 10, na ulikuwa na mda wa dakika 12, then angalia mda wako wa maongezi uliobakia, ndipo utapochoka na kuamini kuwa hawa jamaa ni noma.
 
Kiongozi mm natumia Voda tangu 2005, hayo unayo yasema hayana ukwel wowote,hakuna mbadala wa Voda, hao wengine ndio majanga tupu

Usipinge mkuu hata mm yamekuwa mara kwa mara tatizo la network kukata na sms kuchelewa kufika, hivyo nimelazimika kuwajuza jamaa zangu namba yangu mbadala ya airtel naikishajulikana mahama mazima
 
Hawa jamaa niliwapenda sana ika ilifikia mahali nikachoka, Nilijuwa na utaratibu wa kujiunga na kifurushi cha wiki ambacho unapata sms dkk na internet buundle 700 mb, nilishangaa baada ya siku mbili wakati nipo mtandaoni naambiwa MB zako zimekwisha, kitu kikubwa nilifanya nilidownload kitu chenye MB 46 tu na browse internet kwa kutumia simu yangu ya mkononi nikawapigia simu wanitumie taarifa zangu za matumizi ya MB wakasema watatuma ndani ya muda mfupi matokea yake wiki na miezi ilikatika, ndio hapo nikaamua kuwaachia vumbi, halafu hapa maeneo ya THEMI NANENANE Arusha mtandao upo slow mno yaani kufungua tuu ile page ya google ni 15 min...Daaaaah kwaherini VODA
 
Daah kweli kila mtu ana experience tofauti na hii mitandao yetu. Mi naona mitandao yote with exception of Zantel ambayo sijaitumia bado ni chai tu na kwa kweli inaboa. Jana tu Airtel bundle ya yatosha imebidi nijiunge Mara mbili ktk interval ya saa sita tu na wala sikuitumia simu kwa lolote ( 3G na cellular data access zikiwa off). Ingawa frequency ya ubovu kwa Voda kwa sasa nakubali ipo juu na nathibitisha mengi yaliyoandikwa humu mpk kupotea kwa salio la M Pesa kiajabu ajabu. Tunaweza kufanya categorization ndogo juu ya strength na weakness ya mitandao hiyo na tutakuta kuna baadhi ya aspect kihuduma wamezidiana, na Hali hiyo kuihama moja kwa moja kuwa ngumu. Mfano ( by experience and normal observation)

Coverage countrywide:
1. Airtel
2. Vodacom
3. Tigo

Network strength
1. Airtel
2. Vodacom
3. Tigo

Mobile Money:
1. Vodacom [M Pesa]
2. Tigo [tigo Pesa]
3. Airtel (Airtel money)

Vifurushi (Internet, calls and message)
1. Airtel
2. Tigo
3. Vodacom

Customer care
1. Airtel
2. Tigo
3. Vodacom

So muhimu ni wadau hawa kurekebisha walipoteleza ili customers tuendelee kupata ubora tunaouhitaji..
 
Tangu rostam auze hisa zake Voda imekuwa ga ri la Mkaa
 
Kuna jamaa mmoja ID yake ni papiso(samahani ikiwa kama nimeikosea ID) mwezi uliopita alisema yuko voda na akaanzisha thread kujibu kero za watu mbalimbali kupitia jf sasa thread hii inamuhusu kwa asilimia zote. Japo kipindi alichosema anajibu kuna baadhi ya malalamiko hakujibu kwa ufasaha kama wengi tulivyotarajia.

Tigo sio haba maana sasa wameachia hadi msg za bureee unaambiwa kabisa mwambie na wenzako yaani unatuma kwa uwezo wako sasa hawa kazi ni kwako msg tuu inakaa hewani mpaka inakulazimu umpigie simu uliyemtumia baada ya kuona hajibu lolote. TCRA ndani ya jf mna ID yenu pia kuna wakati mlisisitiza watu waandike malalamiko kupitia e mail yetu ila mmekuwa hamtujibu,sio wote wanaowaandikia mkadhani wanaishi Dar kiasi kwamba ni rahisi kuja ofisini kwenu.

CC : TCRA
:
Vodacom (Rekebisheni kasoro hizi kwa haraka)
 
Back
Top Bottom