Vodacom Tanzania
Official Account
- Aug 12, 2013
- 324
- 126
- Thread starter
-
- #2,061
Vodacom,
Mwenzenu nimeenda kimasomo nje kidogo ya nchi, sijaitumia voda yangu toka tarehe 25/05/2014.
Nategemea kumaliza masomo mwisho wa mwezi wa kwanza 2015.
Je nitaikuta line yangu hai??
Tafadhali tutumie namba ya simu PM endapo hujapokea token zako.Jamani nisaidieni, M-PESA wezi, wananiibia kila mara. Tarehe 30 Nov.2014, wamenila, tarehe 3 Dec.12, wamenila tena. Nilipowapigia,kwamba sijapokea tokens wala fedha haijarudi. Wakaniambia fedha hurudishwa ndani ya siku saba. Leo siku ya 12 hakuna tokens hakuna hela.
M-pesa wezi....wezi hao...Kamata wezi hao! wezi....wezi....wezi hao! Mpesa wezi! Kamata hao!
Maeneo ya kwafundi baiskeli km 16 kutokajamanika ferry kigamboni network ya vodacom inasumbua sana. Tatizo ni la mda mrefu tusaidieni
Tafadhali tutumieni namba za simu PM na maeneo husika kwa msaada zaidi.Voda nyie sahv usanii umewazidi hamna kitu yaan network inazingua cm hazitoki ukituma txt km umeipeleka kwa miguu inachelewa kufika,ukiweka vocha hata kama una bundle unakuta mshaikata so kama mmeshindwa its better mkazima vimitambo vyenu mkafanya shughuli zingine jaman mnatukera
Ni muda sasa mtandao au kampuni ya vodacom imekuwa ikilalamikiwa na wateja wake kutokana na matatizo mbalimbali yaliyopo katika kampuni hiyo hasa pale ambapo salio la mtu lilipokuwa likikatwa na unapopiga simu huduma kwa wateja,muhudumu anakwambia kuwa salio lako limetumika kwa kuwa hukuzima data katika simu yako.
Hapo ndipo mwanzo wa wizi na hujuma za vodacom zilipoanza kwani iliwezekanaje simu iwe na kifurushi cha kutosha,MB za kutosha DAKIKA za kutosha na SMS za kutosha halafu mwisho wa siku uambiwe DATA ktk simu yako ndiyo iliyomaliza salio lako ?
Kwani matumizi ya data kuw on na matumizi ya vifurushi vya voda yanatofauti ?
Habari Baharia, una tatizo gani tafadhali na huduma zetu.Mm ni mtumiaji sana wa vodacom
Nmewapigia sana simu huduma kwa mteja
Nimetuma sana meseji kupitia ukurasa wenu wa facebook
Lakini kila siku mnasema porojo tuuuuu
Awa jamaa ni vilaza sana hakuna lolote wengi wao wanawaza kuiba tu wajinga sana. Muda mwingine mtu umenunu bandle ya cku nzima cha kushangaza masaa nane hadi tisa network upande wa internet inapotea masaa yote hayo hakuna internet wanakuja kurudisha usikuuu na masaa ya bandle lako kuisha muda wake yanabaki pale pale laiti kama vile tatizo halikua upande wao..mimi nasema hivi haya ni matatizo wanayoyatengeneza wenyewe ili kuiba pesa kwa kuwapunguzia muda wa matumizi wateja wao then wao wanachukua ile pesa ya muda ule ambao haukuweza kufanya matumizi ya simu yako ila kule wanaweka kama ulitumia
Habari, mafundi wetu hujitahidi kutatua changamoto ya mtandao mara tu inapotokea kuna tatizo na si kwamba mtandao huzimwa. Kila dakika kila saa wateja wananunua vifurushi hata muda wa usiku sasa unapofikiria kuzimwa si kweli kwa maana kama ndio hivyo basi mtandao utazimwa wakati wote.
Tunalenga kutoa huduma bora kwa wateja wenu na tunakabiliana na changamoto mara tu zinapojitokeza.
Kujua salio la bundle za kwenye internet mnatumia code gani au mnatumia namba zipi
chumvichumvi, inawezekana wakati mwingine pengine mahali alipo mtu huyo mtandao unasumbua. Mama yangu mdogo nikimpigia akiwa sebuleni kwetu haipatikani hadi aende chooni au chumba cha watoto.unampigia mtu unaambiwa hapatikani ili hali yupo hewani unatuma msg inafika kwa muhusika kwa kuchelewa yani ni shida tu