Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom,

Mwenzenu nimeenda kimasomo nje kidogo ya nchi, sijaitumia voda yangu toka tarehe 25/05/2014.

Nategemea kumaliza masomo mwisho wa mwezi wa kwanza 2015.

Je nitaikuta line yangu hai??

Habari Jebs2002, jitahidi kuwa unaitumia kwa angalau mara moja katika mwezi, unaweza kutuma japo meseji moja tu. Hii husaidia kutofutwa.
 
Jamani nisaidieni, M-PESA wezi, wananiibia kila mara. Tarehe 30 Nov.2014, wamenila, tarehe 3 Dec.12, wamenila tena. Nilipowapigia,kwamba sijapokea tokens wala fedha haijarudi. Wakaniambia fedha hurudishwa ndani ya siku saba. Leo siku ya 12 hakuna tokens hakuna hela.

M-pesa wezi....wezi hao...Kamata wezi hao! wezi....wezi....wezi hao! Mpesa wezi! Kamata hao!
Tafadhali tutumie namba ya simu PM endapo hujapokea token zako.
 
Maeneo ya kwafundi baiskeli km 16 kutokajamanika ferry kigamboni network ya vodacom inasumbua sana. Tatizo ni la mda mrefu tusaidieni

Voda nyie sahv usanii umewazidi hamna kitu yaan network inazingua cm hazitoki ukituma txt km umeipeleka kwa miguu inachelewa kufika,ukiweka vocha hata kama una bundle unakuta mshaikata so kama mmeshindwa its better mkazima vimitambo vyenu mkafanya shughuli zingine jaman mnatukera
Tafadhali tutumieni namba za simu PM na maeneo husika kwa msaada zaidi.
 
Ni muda sasa mtandao au kampuni ya vodacom imekuwa ikilalamikiwa na wateja wake kutokana na matatizo mbalimbali yaliyopo katika kampuni hiyo hasa pale ambapo salio la mtu lilipokuwa likikatwa na unapopiga simu huduma kwa wateja,muhudumu anakwambia kuwa salio lako limetumika kwa kuwa hukuzima data katika simu yako.
Hapo ndipo mwanzo wa wizi na hujuma za vodacom zilipoanza kwani iliwezekanaje simu iwe na kifurushi cha kutosha,MB za kutosha DAKIKA za kutosha na SMS za kutosha halafu mwisho wa siku uambiwe DATA ktk simu yako ndiyo iliyomaliza salio lako ?
Kwani matumizi ya data kuw on na matumizi ya vifurushi vya voda yanatofauti ?


Tungependa kupata namba yako ya simu Idd ili kufuatilia suala hili na kupeana majibu yasiyo na shaka. Pia kutatua suala la mtandao kusumbua.

Mhudumu hukuomba upige wakati mwingine kwasababu unakuwa umepiga simu muda huo huo ambapo tatizo limetokea ilhali taarifa zako huingia kwenye mifumo muda mfupi baada ya kufanya matumizi.

Tafadhali tusaidie namba ya simu kwa msaada zaidi.
 
Awa jamaa ni vilaza sana hakuna lolote wengi wao wanawaza kuiba tu wajinga sana. Muda mwingine mtu umenunu bandle ya cku nzima cha kushangaza masaa nane hadi tisa network upande wa internet inapotea masaa yote hayo hakuna internet wanakuja kurudisha usikuuu na masaa ya bandle lako kuisha muda wake yanabaki pale pale laiti kama vile tatizo halikua upande wao..mimi nasema hivi haya ni matatizo wanayoyatengeneza wenyewe ili kuiba pesa kwa kuwapunguzia muda wa matumizi wateja wao then wao wanachukua ile pesa ya muda ule ambao haukuweza kufanya matumizi ya simu yako ila kule wanaweka kama ulitumia

Habari, mafundi wetu hujitahidi kutatua changamoto ya mtandao mara tu inapotokea kuna tatizo na si kwamba mtandao huzimwa. Kila dakika kila saa wateja wananunua vifurushi hata muda wa usiku sasa unapofikiria kuzimwa si kweli kwa maana kama ndio hivyo basi mtandao utazimwa wakati wote.

Tunalenga kutoa huduma bora kwa wateja wenu na tunakabiliana na changamoto mara tu zinapojitokeza.
 
Habari, mafundi wetu hujitahidi kutatua changamoto ya mtandao mara tu inapotokea kuna tatizo na si kwamba mtandao huzimwa. Kila dakika kila saa wateja wananunua vifurushi hata muda wa usiku sasa unapofikiria kuzimwa si kweli kwa maana kama ndio hivyo basi mtandao utazimwa wakati wote.

Tunalenga kutoa huduma bora kwa wateja wenu na tunakabiliana na changamoto mara tu zinapojitokeza.

Issue sio mtandao mzima issue ni mtandao upande wa internet...mbona ata kama internet lakini bado mtu anaweza kununua kifurushi kama kawaida
Hapa nazungumzia suala la fidia kwa mteja aliyenunua bandle then internet ikapotea takribani masaa matano au sita lakini nyie muda wa ku expire bandle unabaki pale pale hii inakuaje kama c kumdhurumu mtumiaji? Ata kwenye football kuna dakika za nyongeza hii ni kwa vile mpira usimama ktk mipira ya kurushwa, faulo na ata mtu akiumia ndio hufidia muda uo sasa kwa nini nyie muweke fixed time wakati mnajua mitandao yenu bado michanga inayumba yumba tafuteni program itakayokuwa ina adjust tym ya ku xpire muda wa bandle kuisha kila internet inapopotea kutokana na sababu za matatizo ya mitambo yenu kama lisaa limoja basi na kule muda utajiadjust hivyo hivyo yaani muda wa ku xpire uendane na muda internet yenu ipo
 
Kujua salio la bundle za kwenye internet mnatumia code gani au mnatumia namba zipi
 
mwanza mjini mtandao wa inyernrt mbovu sana.kufungua picha tu umetumiwa whatsapp ni issue.kutuma picha au video ni kazi sasa ku download ndio balaa kabisa.mwanza ni jj kubwa jaman jitahidin bas kuweka mtandao wa internrt ambao upo vizuri
 
Vodacom kitunda tu ni shida network sijui ni kwa nini?napenda kutumia line ya Voda bt punde naitupa na kuhamia Airtel Kitunda Internet shiida sasa nitaishije bila Jamii Forums??Mnataka niwe remotely??
 
Kazi imewashinda nyie sms zinachelewa sana kufika kwa wateja wenu nilishawaona mnazingua nikawapiga chini napata shida tu kwa watu ninao deal nao hayo tu
 
Hivi karibuni Signal wilayani
lushoto imekua mbovu sana, niliiweka benchi line yangu ya tigo na airtel sababu ya internet nzuri voda ila sasa ivi naona na huku ni majanga matupu, nanunua MB zina-expire cjatumia hata nusu yake rekebisheni 3g, naipenda voda but ikipita wiki moja hamjarekebisha NAHAMAAA
 
unampigia mtu unaambiwa hapatikani ili hali yupo hewani unatuma msg inafika kwa muhusika kwa kuchelewa yani ni shida tu
 
unampigia mtu unaambiwa hapatikani ili hali yupo hewani unatuma msg inafika kwa muhusika kwa kuchelewa yani ni shida tu
chumvichumvi, inawezekana wakati mwingine pengine mahali alipo mtu huyo mtandao unasumbua. Mama yangu mdogo nikimpigia akiwa sebuleni kwetu haipatikani hadi aende chooni au chumba cha watoto.
 
Last edited by a moderator:
Voda kweli wezi, wamenilia hela kuwapigia wananieleza eti huduma hii inatatizo, kama inatatizo nirudishieni hela yangu naambiwa pesa haiwezi kurudi chakukusaidia labda ujitoe kwenye hii huduma. wizi mwingine wa waziwazi wanatangaza ongea kwa shilingi 2 kwasekunde kumbe sio ni 2.7 kwasekunde ni heri waseme ukweli.

 
Back
Top Bottom