masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,207
- 13,839
Wizi ni state of mind.
Kama wewe si mwizi mwenyewe ndani ya VODACOM, basi ni lazima una benefit kutokana na wizi huo.
kwa kweli voda wanaiba hii ni hatari jamaa wamulikwe jamani!
Mkuu ni beneficiary wa makato wanayokata nini...jamaa wanakera sana juzi nimeweka pesa nijiunge ikawa inagoma huku salio linazidi kuisha taratibu mpaka ikabaki zero sasa nimehamia airtel sina wasiwasi.
vodacom ni wezi sana mi nilishawafata hadi oficini kwao ubungo na kuwatishia kuwapeleka Tume ya mawasiliano. yaani wanaiba sana hela zilizo kwenye mpesa, wakikutumia hata msg ya matangazo yao ukiangalia balance kwenye mpsea utakuta wamekuchagi
Sio kwamba nwatetea vodacom ila ukisahau kuswitch off intanet connection kwenye simu yako na labda iko kwenye 3G/HSDPA pesa inalambwa haraka sana, mimi huwa nanunua bando ya cheka na kuhakikisha sina salio kabisa.
Hatuwezi kuhahalilisha ujambazi kwa kutumia ujambazi.....kama watu walikuwa wanaiba kw akutumia PD proxy, basi wachukuliwe hatua......lakini sio kwa njia ya kulazimishana (in this case KUIBA) gharama za service ambayo mteja hatumii/bila dhamira yake
Mkuu kama unaelewa hizi gharama zinachajiwa vipi na Vodacom tusaidie tupate kuelewa.....how do these people charge your phone........huku niliko nikitaka matumizi ya internet kwenye simu yangu nanunua package ya mwezi na wala hii gharama haingiliani na pesa nitakazokuwa naweka kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya mawasiliano ya simu....kwa hiyo najua kabisa how much nina-spend kwenye internet na how much kwenye mawasiliano ya simu....
...sasa kwa maelezo ya Lole Gwakisa....inaelekea yeye aliweka TShs 10K.....na baada ya muda imeisha bila ya yeye kujua imeishaje........watu wengine wanasema eti kwakuwa aliacha ON matumizi ya data!!!......kwanini hivi vitu visitenganishwe? ukiweka pesa yako kwenye simu hata iwe TShs 100K....iwe ni kwa matumizi ya mawasiliano ya simu.....na pale unapotaka kutumia internet unatuma ujumbe/code ili kununua package unayoitaka.......either kununua kupitia salio lako kwenye simu au kununua upya kabisa......
Kinachonishangaza ni kusikia huko bongo ukishaweka pesa yako kwenye simu tu.......ni lazima uhakikishe "eti data iwe OFF kwenye simu yako".....WHY?....hii ni kama kulazimisha gharama kwa mtu hata kama hatumii service yenyewe!......hence huu ni WIZI
Huo ni UONGO unaotumika kuhalalisha WIZI.Sio kwamba nwatetea vodacom ila ukisahau kuswitch off intanet connection kwenye simu yako na labda iko kwenye 3G/HSDPA pesa inalambwa haraka sana, mimi huwa nanunua bando ya cheka na kuhakikisha sina salio kabisa.
Nakubaliana mkuu, malalamiko ya wizi yamekuwepo siku nyingi katika mtandao wa VODACOM ingawaje mimi nimekumbwa hivi karibuni tu.Gwakisa, umesahau kuwa Rostam bado ana hisa Vodacom? Hata watu kama January Makamba hawafai kusimamia sekta nyeti kama ya mawasiliano! January na Boss wake katika wizara ya mawasiliano wanatakiwa kujiuzuru. Pesa tunazoibiwa kila siku na makampuni ya simu ni nyingi mno!
Kuna kitu nadhani watu wengi wanaolalamika kuwa wanaibiwa mnakosea. Kama unatumia smartphone na hujajiunga na bando la internet ni lazima pesa yako itaendelea kuliwa taratibu hadi iishe. Cha msingi kama wewe hutumii inernet nenda kwenye mobile network then iweke off! Otherwise applications ambazo zinafanyakazi katika background zitamaliza pesa yote.