Hatuwezi kuhahalilisha ujambazi kwa kutumia ujambazi.....kama watu walikuwa wanaiba kw akutumia PD proxy, basi wachukuliwe hatua......lakini sio kwa njia ya kulazimishana (in this case KUIBA) gharama za service ambayo mteja hatumii/bila dhamira yake.......
Mkuu kama unaelewa hizi gharama zinachajiwa vipi na Vodacom tusaidie tupate kuelewa.....how do these people charge your phone........huku niliko nikitaka matumizi ya internet kwenye simu yangu nanunua package ya mwezi na wala hii gharama haingiliani na pesa nitakazokuwa naweka kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya mawasiliano ya simu....kwa hiyo najua kabisa how much nina-spend kwenye internet na how much kwenye mawasiliano ya simu....
...sasa kwa maelezo ya Lole Gwakisa....inaelekea yeye aliweka TShs 10K.....na baada ya muda imeisha bila ya yeye kujua imeishaje........watu wengine wanasema eti kwakuwa aliacha ON matumizi ya data!!!......kwanini hivi vitu visitenganishwe? ukiweka pesa yako kwenye simu hata iwe TShs 100K....iwe ni kwa matumizi ya mawasiliano ya simu.....na pale unapotaka kutumia internet unatuma ujumbe/code ili kununua package unayoitaka.......either kununua kupitia salio lako kwenye simu au kununua upya kabisa......
Kinachonishangaza ni kusikia huko bongo ukishaweka pesa yako kwenye simu tu.......ni lazima uhakikishe "eti data iwe OFF kwenye simu yako".....WHY?....hii ni kama kulazimisha gharama kwa mtu hata kama hatumii service yenyewe!......hence huu ni WIZI
Mkuu
Ogah tatizo ambalo naliona hapa ni uaminifu wa wafanyakazi wa VODACOM katika kuhandle transactions za wateja.
Sioni kama tatizo la kuweko ON au OFF data aps na settings kama ndio source ya tatizo.
Hii mimi imenitokea kwa mara ya kwanza kabisa katika kutumia huduma za Voda, kwa salio LOTE kuliwa kwa mkupuo.
Kwamba data services ziko ON ni uongo mkubwa kwani toka jana nilipo lalamika niliweka hizo data settings ON na kucharge salio la Tshs 50,000 na matumizi ni ya kawaida kabisa, hii ikiwa na maana mwizi aidha amedhibitiwa au bado hana access na personal data za wateja.
Nimenote kuwa wizi wenyewe wa Tshs 20,000 ulifanyika tarehe 29/12/2013,jumapili mchana, most probably wakati ambao supervisors hawako kazini
Hapo hakuna lugha rahisi zaidi ya kusema kuna kirusi cha wizi ndani ya VODACOM.
Nimewasiliana na wafanyakazi zaidi ya watatu ndani ya VODACOM , ukiacha wale wa Customer Care, na wamenithibitishia kuwa huo wizi upo,licha ya Front Desk yao kukataa with a wooden face.