Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Hizi sms za kushinda 2,000,000 au 5,000,000 zinazotumwa mara kwa mara kutoka mtandao wa vodacom mimi zimenichosha naomba wahusika wasitishe kwani zinaniletea usumbufu sana. Kwa siku wanatuma zaidi ya mara 5. Mimi sijawahi kuomba kuunganishwa kwenye hiyo namba ili kuingia kwenye mashindano yao.

Hii tabia ikiendelea nitaishitaki kampuni kwa kunisababishia usumbufu wa kisaikolojia. Mimi sina hela lakini sitaki mashindano ya kulazimishwa eti mara "mwenye namba 075******* utajipatia 200000000 au Sio ya kukosa: 075******hii ni kamata mpunga ya vodacom. Tuma neno GO kwenda namba 15544 na unaweza kushinda 5,000,000 Kila watuma nafuta lakini baada ya muda kidogo wanatuma tena.

Mtatusababishia ajali jamani
 
Hata mi washaniudhiiiii na leo nawapigia wapuuzi kweli
 
Mimi huwa najisikia raha sana wanaponitumia, maana najua wanataka kunitapeli ila situmi Meseji bali nikiwa kwenye bia najifanya nipo bize na simu kumbe ni Meseji za kuomba hela kutoka vodacom
 
Vodacom wamekuwa ombaomba mkuu
 

Kwani kuna Mtu labda alikulazimisha uwe na line ya Vodacom? Watanzania bhana! Hasira zote hizi zinaonyesha kabisa how stressful you are Mkuu hasa ukizingatia Jamaa kakaba mpaka " kivuli ". Mchezo huu hauhitaji hasira Mkuu!
 
Mimi huwa najisikia raha sana wanaponitumia, maana najua wanataka kunitapeli ila situmi Meseji bali nikiwa kwenye bia najifanya nipo bize na simu kumbe ni Meseji za kuomba hela kutoka vodacom
ukithubutu kujiunga na hiyo kitu mjomba. Wananyonya ka ela chako chote kwa kukutumia vimeseji vya maswali ya ajabu ajabu.

Alafu wakiona huna salio wanakumbia tutakujulisha droo ikishachezeshwa.
 
mie nimeamua kutupa laini yao..kila kukicha wanawaza kuwakamua tu wateja wao hawana huruma hawa...Nashauri wastop mara moja kutuma tuma hovyo hayo ma sms yao
 
Vifurushi vyenu ni wizi mtupu nimehama
Yani MB 1??? Si upuuzi huu.
 
Wife anafanya kazi ya mpesa wakala namba 66062 leo kuna mteja kaja kutoa pesa kabla ya kutoa pesa alikuwa na akiba ya sh 10,020 mteja akatoa sh laki tatu na msg ikaja kwa jina la james baraka ref namba CB610A767 jumla ya balance 310,020 mteja akapewa hela alipokuja mteja mwingine ile laki tatu imeyeyuka imebaki 10,020 tumepiga customer care tunaambiwa hakuna muamala wa laki tatu jwa leo ilhali msg tunayo kwenye simu swali kama hakuna transaction iliyofanyika imekuwaje msg ikaja kwa wakala yenye kiasi sawa na kilichotolewa ikiwa na jumla ya kiasi kilichokuwepo kama ni wizi mwizi huyu alijuaje kwa wakala husika ana balance ya sh kadhaa naomba majibu ili wakati tunaenda kutafuta haki mbele tuwe tunachakuwambia
 
Vodacom ghalama zenu ziko juu mno, na internet yenu sehemu kubwa ya nchi ni 2g! Amkeni mkiendelea kulala na kuridhika HALOTEL anakuja kuwafunika kabisa. Nimeweza kusafiri Dar hadi Dodoma, Dar hadi Mbeya na Dar hadi Songea, Ni sehemu chache sana ambako Vodacom inashika 3g, sehemu kubwa ni 2g na sehemu nyingi haishiki tofauti na Halotel anhalten ni full 3G H+ na internet yao ina speed kama 4G yenu
 
Nipo kwenye ofisi yenu hapa Arusha nataka ni renew line lkn cha kushangaza toka asubuhi tunaambiwa hakuna mtandao, mmetukera kwakweli isitoshe wengine tumetoka mbali .
 


Sent from my TECNO-A7 using JamiiForums mobile app
 


Sent from my TECNO-A7 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…