Nilikua naipenda voda Sana.Juzi niliweka muda wa maongezi 2000 na sikujiunga na kuamka ipo 1300.Nikitaka kufanya huduma za Mobile kiganjani ati uweke salio na wakati Airtel ni free.Daah piga chini !!!!!,View attachment 1371003
Sent using Jamii Forums mobile app
Nlitaka nikutumie wewe kufikisha ujumbe my dia. Huoni ujumbe ulivyofika vizuri?
Ili wajirekebisheUlipoanza Kuutumia Mtandao wa Vodacom ulituambia ( ulitushirikisha ) hadi leo hii unauhama rasmi ndiyo unatushirikisha hivi?
Ungehama tu kimya kimya,umuhimu wa kuanzisha uzi haukuwepo
Tunayaona mambo kwa mitazamo tofauti. Linaweza kuwa duni kwa mtu mmoja likawa na maana kubwa kwa mtu mwingine.
Ni vyema kila mmoja kuheshimu maoni ya mwenzie, hayupo mwenye mawazo bora zaidi ya mwingine.
Alisikika manager masoko voda
Pole sana mzeeVodacom now nawashitaki mahakamani kwanini umeniibia salio langu LA simu Mara kadhaa Kwa kuniunga kwenye huduka ambazo sijawahi hata kufikiri kurequest nizitumie? Kama huu ushuzi mlio anzisha uitwao UNSUB?
Hakika mmezoea sasa tutakutana mahakamani Kwa fidia ....nimechoka na usumbufu huu
Vyuma vimekaza harafu hivi hivi mnanyakua visalio Kwa vihuduma vya ajabu ajabu.....hivi Mimi MZEE wa miaka 47 UNSUB ya nini? Harafu ndiyo nini? Hata maelekezo hakun...
Nandaa malalamiko
Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo Vodacom Tanzania namba ya huduma kwa wateja ni majanga, wanataka mufanye mawasiliano kwa mitandao ya kijamii au kuna menu chache za sauti ambazo kuna matatizo kibao hayapo kwenye category za menu zao, sasa ilitakiwa uongee na mhudumu moja kwa moja haupati nafasi hiyo.Ni kweli hata mimi imenitokea mara kadhaa na juhudi za kuongea na customer care hazikuzaa matunda sasa nimeachana nao.
Habari, nilifanya kurejesha laini yangu ya cm iliyopotea Kwa kufuata hata zote lakini mpaka sasa siku ya tatu haijaanza musoma...msaada Tafadhali.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu mteja,
Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?
Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.
Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:
- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.
Karibu
Vodacom Tanzania
Nyie mnaojiita watumishi wa vodacom nashindwa kuelewa hizi mb mnazotoa kwa ajili ya facebook mnamaanisha nn.Sababu ukiangalia mb zenyewe zinatumika kwa speed ya 2G inakuwa haina maana,ni wizi na utapeli tu huo.
Ukiangalia vifurishi vyenu navyo saiv ni wizi wa mchana kweupe,kwa sababu huwezi kunipa kifurushi cha siku halafu ndani ya masaa mawili eti mb zimeisha ma wakati huo labda umeingia google kuangalia rate za dola.Jaribuni kuangalia na kufikiria gharama za maisha ya mnaowahudumia ambao ni wateja wenu.